Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine

Sina hakika kama Makonda anawajua harafu Mama na vyombo hawajui.

Pengine ni njia ya kuwatisha kwamba tunawafahamu mnaompa hela Mange
 
Nikizingatia historia ya utofauti wa damu kati ya mawaziri hawa na huyu "jasiri" Makonda, nahisi watatajwa siku ya jumatatu:-
1. Waziri wa umbea.
2. Waziri wa maokoto.
3. Waziri wa shughuli.
4. Waziri wa ujirani.

Hasa hasa huyo namba 1 na namba 3, sijui!!!.
 
Makonda smart, kama ni kweli anawajuwa au hawajui lakini kauli ile inamfanya mtu kuhisi jiwe limempiga. Makonda ni content na anajuwa kutumia zile nafasi. Kwenye siasa ukitaka kuwa maarufu wewe leta kauli tata tu utaongelewa lakini ukijifanya unahutubia kama uko kanisani hutoboi nchi hii. Si umeona kina Kingangwala wameanza kutoka hadharani kumtetea Mange.
 
Nikizingatia historia ya utofauti wa damu kati ya mawaziri hawa na huyu "jasiri" Makonda, nahisi watatajwa siku ya jumatatu:-
1. Waziri wa umbea.
2. Waziri wa maokoto.
3. Waziri wa shughuli.
4. Waziri wa ujirani.

Hasa hasa huyo namba 1 na namba 3, sijui!!!.
MAKONDA NI MCHONGANISHI NA UCHONGANISHI HAKUANZA LEO AMEWACHONGANISHA VIONGOZI NA WATU WENGI KWA MAGUFULI
 
Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Makonda hajifunzi, kilichomtoa uenezi ni hiki hiki, na akiendelea hivyo
Nikizingatia historia ya utofauti wa damu kati ya mawaziri hawa na huyu "jasiri" Makonda, nahisi watatajwa siku ya jumatatu:-
1. Waziri wa umbea.
2. Waziri wa maokoto.
3. Waziri wa shughuli.
4. Waziri wa ujirani.

Hasa hasa huyo namba 1 na namba 3, sijui!!!.
jtatu itafika na utakuwa suprised, hato mtaja yoyote zaid vitaongelewa vitu vingine. Siasa za bongo ziache kama zilivyo
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kauli iliyotolewa na Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda ni nzito kwelikweli,imeitetemesha nchi,imeleta sintofahamu kwa wananchi ,imeleta amsha amsha na kila mtu na neno lake.ni kauli ambayo imeacha maswali mengi kila mtu na majibu yake.kila mtu anawaza ni akina nani hao wanaomhujumu Rais wetu na nini dhamira yao.kwanini walipe watu kwa ajili ya kumtukana Mheshimiwa Mitandaoni? Dhumuni lao wanataka nini? Wanataka Rais Samia akichafuka kwa matusi wao wapate nini? Wana malengo gani?

Nini malengo yao baada ya kuwa Rais ametukanwa sana? Wanataka wampindue Rais uchaguzi ujao? Wanataka kumhujumu? Kwanini wamhujumu? Je ikiwa hao watu wataacha kuwalipa kuwalipa hao watu wanomtukana Mheshimiwa Rais mitandaoni,unafikiri ni njia ipi ya pili au mipango gani mingine watafanya kuendelea kumuhujumu Mheshimiwa Rais? Je ndio utakuwa mwisho wa wao kuachana na mipango wao ovu? Je usalama wa Rais upo kiasi gani kwa yeye kuendelea kuwa na kufaya kazi na watu ambao amewaamini lakini wao wameshindwa kuwa waaminifu kwake mpaka kufikia kulipa watu pesa ili Rais atukanwe na kuhujumiwa kupitia mitandao? Je watu hawa ni vipi wanaweza kufanya kazi kwa weledi wakati hawampendi Rais? Ni vipi wanaweza kutunza siri za baraza la mawaziri? Ni vipi wanaweza shindwa kuvujisha siri za vikao?

Kauli hiyo ni muhimu vyombo vyetu vya usalama kuifanyia kazi kauli hiyo na kumshauri Mheshimiwa Rais kufanya maamuzi ya haraka.maana haiwezekani Mh Rais awe na watu ambao hawapo pamoja,hawana mawazo ya pamoja.ni hatari sana.kwa sababu watu hao watatoa na kuvujisha siri zote za baraza la mawaziri,watavujisha nyaraka za serikali,watavujisha mipango na mikakati yote ya serikali,watamhujumu Rais na serikali yake na nchi kwa ujumla.watafaya kazi chini ya viwango ili Rais alaumiwe na kutukanwa zaidi na zaidi.watafanya maamuzi na kutoa kauli zitakazokuwa zinajenga chuki na kuichongaisha serikali na wananchi.watafanya kila linalowezekana ili Rais Samia aendelee kuchukiwa zaidi na zaidi.

Huwezi ukalala na nyoka ndani na ukasema nyoka hatakuwa na madhara kwako kwa sababu tu unalala juu ya kitanda.kwahakika utakuwa unajidangamya. Nyoka mmoja aliye ndani ya nyumba yako ni hatari zaidi kuliko koboka aliye nje pamoja na Kundi la Simba walio nyuma ya nyumba yako.kama kuna nyoka ndani ni bora upambane kumtoa haraka sana ili ndani kuwe na amani na usalama.

Kauli ya Mheshimiwa Makonda siyo ya bahati mbaya na haiwezi kutolewa kwa bahati mbaya wala kisiasa.hivyo naamini anafahamu anachokizungumza na alichozungumza na mawaziri wanaomhujumu Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais hawezi kufanya kazi na kuwa pamoja na watu ambao viapo vyao wameshavisigina na kuingia kazini kumhujumu. Ni lazima hatua zichukuliwe haraka ili kujenga imani na kuaminiana ndani ya baraza.hakunaga jambo dogo na la bahati mbaya katika siasa. Ni hatari sana kuendelea kuishi na shetani kwa matarajio kuwa atabadilika na kuwa malaika mkuu.chui hata aloane hawezi kubadilika na kuwa kondoo wala nyoka akijivua gamba habadiliki na kupunguza sumu yake.atabaki kuwa nyoka yule yule mwenye sumu ile ile na tabia zile zile za nyoka.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Back
Top Bottom