Operesheni wahamiaji haramu kazi imeanza, vilio vyatanda, wachina wagoma

Wako pia Waturiki weengisana wanaishi kinyemela,Uhamiaji tembeeleeni makasino makubwa posta kama Princess cassino na maduka na viwanda vya feicha kama Anaoli.
 
Hapa Kazi tu. kuna kampuni mmoja hivi kuna foreigners kama 500 hapa TZ..... nasikia atleast 40% wametimuliwa.... kazi kweli kweli
 
Tena Manji anaweza kuwa Mtanzania wa kweli kuliko wewe.


Wa kweli by besi au necherolaizesheni?
 
leo mtoto aliyezaliwa kwenye maungano ya mngoni na msukuma utamwita kabila gani?
kwani mtoto wa kitanzania hurithi kwa mama au baba...?mbona swali unalouliza ni rahisi sana....kila jamii ina taratibu zake za kurithi...so km unarithi kwa baba basi chukua kabila la baba...
 
Kuna dada mmoja mzimbabwe anafanya ofsi moja posta kazi ya clearing and forwarding ukimuona huwezi mshutikia sio mbongo maana anaongea kiswahili kwa ufasaha mno pia ana kampuni yake inapiga hela ndefu but cha ajabu wafanyakazi wake ambao ni wabongo anawalipa hela ndogo mno kulingana na kazi wanayomfanyia
 
hiyo operation iende na kwa watu weusi waliopo nchini...kuna wakenya wengi sana kwenye makampuni ya hapa nchini, unakuta eti mkenya ni mhariri wa Radio ya Kiswahili?

kuna kampuni kubwa ya Media imeajiri wakenya wengi sana, unakuta eti mkenya ni msomaji wa habari za kiswahili kwenye radio hiyo.

Kwa ufupi huyo mwenye kampuni kaajiri RAIA wa kigeni zaidi ya 30.

mmoja eti ni mhasibu.., IT, Waandishi wa habari, Moja anafanya Clearing and forwarding ni wakala na ni mkenya, yaan ni wengi sana, kuna jamaa anafanya kwenye hiyo kampuni anasema yaan ni shida sana...
Hili ndio tatizo la Watanzania,si uitaje hiyo kampuni na hao wageni?hapa ni JF kila kitu huwekwa wazi.
 
Kuna dada mmoja mzimbabwe anafanya ofsi moja posta kazi ya clearing and forwarding ukimuona huwezi mshutikia sio mbongo maana anaongea kiswahili kwa ufasaha mno pia ana kampuni yake inapiga hela ndefu but cha ajabu wafanyakazi wake ambao ni wabongo anawalipa hela ndogo mno kulingana na kazi wanayomfanyia
Anaitwa nani na jina la kampuni Yake tafadhali.
 
kwa kweli hili nampongeza sana Magufuli, jamani ilifika hatua hii nchi ikawa shamba la bibi angalia wachina wanauza mpaka mahindi ya kuchoma, wanauza mama lishe, hao hao wanatuibia na kuua wanyama wetu, nafikri serikali inatakiwa kuwapiga marufuku wachina wote na wageni wengine wanao fanya kazi zetu.
 
viva Magufuli kwa hili nakuunga mkono maana wachina wamejaa wanafanya kazi mpaka za kuchoma mahindi, na kuuza mama lishe, tunahitaji wachina wenye technology na siyo mama lishe na wachoma mahindi, pili raisi usisahau kwenye maeneo ya migodi wamejaa wachina wanatuibia kila kukicha anzia shinyanga kuna wachina wana migodi uchwara mpaka tunashangaa vibali walivitoa wapi? wameharibu mazingira na kutililisha taka kwenye makazi ya watu na mtoni.
 
Makampuni yote ya wahindi yamulikwe.
Kuna wengine wanafanyakazi na hawaruhusiwi kwenda mjinj KWA kuogopa kukamatwa.
Vyuo na mashule ya Wahindi yamulikwe

Viwanda vya nondo pia kuna wahindi wengi sana hawana vibari, wakitoka mwisho getini.
 
Dah. Kama kigezo ni kiswahili basi wengi si watanzania. Vijijini kule wengi hawajui kiswahili

Sijamaanisha kiswahili Peke yako mengi Lugha ni moja wapo...wee unaweza kwenda huko uGABACHOLINI ukajiita Muhindi acheni ujinga wa mshumaa
 
Tena Manji anaweza kuwa Mtanzania wa kweli kuliko wewe.

Typical African!! Huyo Mtanzania wa kweli kuliko mwingine ni yupi au ana nini zaidi!!?

Tunapenda kuhangaika na wageni weusi ........ tena weusi wenzetu!! Hata RSA ilikuwa hivyo hivyo!!

Hata JF utakuta watu wanapiga kelele, Oh, Wakenya, Waganda ....... wanawasahau Wahindi na Wachina!!
 
Back
Top Bottom