Open Space mbele ya Palm Beach Hotel!

Hivi open space za ilala hazikuwa katika lile sakata la kisiasa la William Lukuvi? Au alipambana tu na zile ambazo hakukatiwa mshiko? Au alianzisha lile sakata ili waliokuwa wamenunua wakamkatie mshiko?

...Ule ulikuwa ni mchezo wa kuigiza tu...LUKUVI alikatiwa na kina LONDA ....Baadaye akaja kugundua wamempa PEANUTS ....ndio maana akakasirika ....baada ya kasheshe lake kila aliyeuziwa "VIWANJA" Haramu alienda kumuona Lukuvi kwa muda wake...TUNAOMBA PCCCB Wachunguze upya hili sakata....[au kama wanaogopa kwa sababu baadhi ya viwanja vina mkono wa mkuu waseme wazi..declare interest..ili iundwe tume huru]

Nini hiyo kuna majumba mengine yaliyokwisha kuwa declared kama historical buildings,,,...achana na pale salamander...yamepigwa nyundo ..wote huu ni ufisadi...tunataka ushughulikiwe.....
VIle viwanja pale sea cliff hadi golden tulip ..... watu wanaendelea kujiweka karibu kwa kujiwekea mipaka...ya nguzo na mataiiri ...na wengine wameweka makontena..pamoja na "agizo" la rais kuwataka waondoke...........
 
Lukuvi nae ni fisadi mzoefu toka enzi za mradi wa mabasi wa vijana wa CCM!! Walikula mtaji na hata basi moja halikutembea na bado wanadunda tu!
 
hotelview.jpg



Uwanja wa wazi[open space] ulio mbele ya hotel hii ya kitalii iliyopo upanga ,ALI HASSAN MWINYI ROAD ,ni pale ambako wakazi wa jiji mnafahamu taxi zilikuwa zinapaki .....na kuna kichochoro cha kwenda makao makuu ya jeshi.
Hata wenye hoteli hiyo wamebakiwa na kauchochoro kadogo tu ka kupaki magari......na imeharibu mandhari kabisa ya eneo hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likitunzwa kama eneo la wazi linalotazamana na bustani nyingine ya jiji iliyopo Prsyberian church kwenye mataa ya upanga ......inatia aibu sana ..

Naomba tufuatilie kuona nani ameuziwa pale na tayari ameweka ukuta ..nadhani anasubiri kuanza ujenzi,,,,..ni wazi atakuwa ni mtu ambaye yupo connected ...na ametumia vema muda ambao kila mtu alikuwa busy na habari za uchaguzi kujijengea ukuta haraka haraka.....HII IWE AJENDA YA KWANZA YA MADIWANI WA JIJI WAWE WA CCM AU CHADEMA ..KURUDISHA MAENEO YA WAZI MFANO YA HILI....NI WAZI KUNA UFISADI MKUBWA WA AINA HII.

Siamini, labda kama serikali ya ccm imeamua kujenga uzio kwa ajili ya garden.
 
hiyo ndiyo ccm?
watu walichangia kampeni bwana ndiyo wanjilipa taratibu... !
kwani wewe kofi, tisheti hukupata au ulipewa bendera na picha ya jk 2.....!
 
Mambo ya aibu sana haya yaani wanataka jenga kila mahara uko wanakoenda kuganga njaa ulaya hawaoni open space uko
 
Mlikuwa mnaona Helkopta za CCM hamkuuliza zinalipiwa na nani. ndiyo hao sasa wanarudisha fedha zao
 
Mlikuwa mnaona Helkopta za CCM hamkuuliza zinalipiwa na nani. ndiyo hao sasa wanarudisha fedha zao


tutalipa sana gharama za udalali mwaka huu-power brokers-na hivi gharama za kapeni zilikuwa bilioni 80 bado sana.................
 
Hili ni suala ambalo taasisi kama LEAT na Mtetezi wanaweza kufanya tafadhali wasiliana na LEAT na kama utakuwa na vielelezo vingine vingi kuhusiana na maeneo hayo ya wazi basi tuwasiliane ili kuona namna ya kuweza kupambana na uchafu huu.
 
Hili ni suala ambalo taasisi kama LEAT na Mtetezi wanaweza kufanya tafadhali wasiliana na LEAT na kama utakuwa na vielelezo vingine vingi kuhusiana na maeneo hayo ya wazi basi tuwasiliane ili kuona namna ya kuweza kupambana na uchafu huu.

Rugemeleza...

Kama kuna mahali LEAT has failed ni hili suala la OPEN SPACES.....sio wao wala sio HAKIARDHI.....vipi hazina project funding bado? mbona UN Habitat na hata Google/Bill Gates wamemwaga nyingi???? Ama bado hazijawa mtaji mkubwa kisiasa na akili za LEAT sasa zimegubikwa na maslahi ya kisiasa?

Interesting kusikia "wnaharakati" nao wanaongea lugha ya "lete vielelezo" na sio kuwa wao ndio wainue miguu kutoka katika AC zao na kutafuta vielelezo..........
 
Ama kweli Jasiri haachi asili...! Yaani wanafisadi hadi hapo usoni kabisa mwa Jiji...! Hii kali kwa kweli...!
 
Rugemeleza...

Kama kuna mahali LEAT has failed ni hili suala la OPEN SPACES.....sio wao wala sio HAKIARDHI.....vipi hazina project funding bado? mbona UN Habitat na hata Google/Bill Gates wamemwaga nyingi???? Ama bado hazijawa mtaji mkubwa kisiasa na akili za LEAT sasa zimegubikwa na maslahi ya kisiasa?

Interesting kusikia "wnaharakati" nao wanaongea lugha ya "lete vielelezo" na sio kuwa wao ndio wainue miguu kutoka katika AC zao na kutafuta vielelezo..........

Nakushukuru ndugu yangu. Siku zote vielelezo ndiyo imekuwa nguvu yetu kama huna vielelezo kama vile barua za kugawa viwanja hivyo huna kesi na huwezi kufanya harakati nzuri na yenye mafanikio. Kitu kingine ni ramani za mipango miji kuonyesha jinsi maeneo ya jiji yalivyotengwa kisheria.

LEAT imepitia kipindi kigumu na mabadiliko mengi. Wengi wameondoka ikiwa ni pamoja na mimi (ni mjumbe wa bodi) na kibaya niko nje ya nchi. Lakini ili mtu kama mimi niweze kuwa wa msaada kupata vielelezo ni muhimu. Ni vizuri kutumia watu ambao hawafahamiki katika harakati kupata vielelezo. Kuhusu pesa katika nyanja hii bado si nyingi ila ni eneo ambalo watu wengi wanaweza kushirikishwa. Kama unakumbuka jinsi suala la bustani ya Mnazi Mmoja lilivyotatuliwa kwa nguvu ya watu kwani baada ya Kitwana Kondo kutofautiana na Mrema, Wamachinga walivamia na kuezua mabati yote pale wakisema wanamuunga mkono Mrema. Ule uwanja upo pale kutokana na nguvu ya watu.

Sasa kama watu wana ushahidi jinsi Lukuvi na wengine walivyohusika na uchafu huu basi nitapenda kuupata niangalie vipi taasisi kama LEAT, Mtetezi, LHRC, Nola na wengineo tunaweza kushirikiana kupambana nao. Narudia vielelezo (ushahidi) ni muhimu sana ili kuweza kupambana na watu hao.
 
hii thread ipo tayari na inachakachua majina kama ridhiwani, mucaddam jr. nk nadhani hata lukuvi ametajwa

hebu Mangi ifanyie uchunguzi kidogo
 
As long as tunaongozwa na wapumbavu, maisha yetu yataendelea kuwa ya kipumbavu.
 
As long as tunaongozwa na wapumbavu, maisha yetu yataendelea kuwa ya kipumbavu.

Kuna ukweli ndani yake.....nadhani wahusika hawafahamu kuwa hata "open space" ni matumizi ya ardhi! Wao kwa akili zao matumizi ya ardhi ni kusimika jengo kila eneo!
 
Kuna ukweli ndani yake.....nadhani wahusika hawafahamu kuwa hata "open space" ni matumizi ya ardhi! Wao kwa akili zao matumizi ya ardhi ni kusimika jengo kila eneo!

MoD ondoa neno TETESI......this is proven..ingekuwa hakijawekewa hata uzio tunasikia tu basi tungeita tetesi...lakini sadly wameshaweka hadi na ukuta mfupi wa kozi 8 wa kuzugia na kupiga plaster na rangi..what else....si wanasubiri ujenzi uanze...then itakuwa ngumu kuwaondoa,....wiki ijayo tu launch kampeni ya kuwaondoa pale ikianzia haapa hapa JF kama kawaida!!!.......si walikuwa wanabeza siasa za mtandaoni...hawajuwi ndizo zimeleta hili joto??
 
naungana na major kile kilikuwa si kiwanja cha wazi bali ni kwa ajili ya ujenzi ila vipi kuhusu sheria ya kuendeleza ndani ya miezi 36 inasemaje kwani kiwanja kama kile nadhani kilipimwa toka miaka ya sabini.
 
Back
Top Bottom