Ofisi ya Spika yakanusha uvumi juu ya afya ya Spika Job Ndugai

Huwa wanakanusha hivi, halafu baadaye .........! Hali ya baba wa taifa imebadilika ghafla!
 
Sasa mtu yuko India kwa matibabu halafu mnasema yuko bukheri wa afya? Na angekuwa Kongwa tungesemaje?
 
Haswaaaaaaaaaaaa mkuu ni maajabu hapo

Alafu hapo hapo tunatakiwa eti tuone ni jambo jema na la kawaida, ukizingatia hali ya uchumi ya taifa letu hili, mtu mwenye afya njema kabisa eti aende india kwa mda wote huo kwa ajili tu ya checkup...
Alafu hizi ajira ambazo akina jesca wanagaiwa kwenye kiganja, ni moja ya sababu kuu za huu umaskini wetu... Embu ona sasa huyu jesca alivyoandika barua bila kutumia mantiki, kiswahili chenyewe kibovu (iimalike*), yani ni aibu na kudhalilisha ofisi ya bunge kwa kwenda mbele.
 
Mbona la Jesca halitolewi majibu wakati naona kama ndio lina umuhimu kuliko kutudanganya spika mzima wakati yupo hospitali. Au ndio mnataka tuamini wapinzani wamemroga
 
Jana nimepata sms kwamba jamaa kadanja ila nikamlia kavu mtumaji.

Afadhali afanyiwe uchunguzi na maombi afya yake ikiwa njema.

Maana angepelekwa India kwa kukuumwa tungejulishwa kama hivi.

Hii ndiyo Tanzania yenye Maziwa na Asali.

Unaenda hospitali unaumwa, unaombewa upone.unafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu huku ukiwa na afya NJEMA.
 
Wakuu Spika yu bukheri wa afya, huko India anaendelea vyema na ametutakia sisi wa Tanzania wenzie Mfungo mwema wa Ramadhan akitengemaa atarejea nyumbani

View attachment 354732

Hivi Tanzania hatuna madaktari? Tunawasomesha ili wawe spare, siyo? TUtaendelea kuwa vichwa vya wendawazimu mpaka lini? Mpaka sasa bado hatujajifunza lolote?! Hatujui kuwa kama Mungu amekuandikia kufa, hata ungeenda kutibiwa, nini nchi, sayari yoyote utakufa tu? Rais wetu alione hili pia.
 
Mbona la Jesca halitolewi majibu wakati naona kama ndio lina umuhimu kuliko kutudanganya spika mzima wakati yupo hospitali. Au ndio mnataka tuamini wapinzani wamemroga
Mkuu kama ni uchawi basi umetoka ndani ya ccm wenyewe maana hata kama iweje spika hawezi kutoka upinzani ( kulingana na idadi ya wabunge )
 
Sijaelewa walicho kanusha hapo ni nini! Wanaanza kwa kusema hali yake ni njema kabisa, kisha wanaeleza kwamba anafanya uchunguzi wa afya yake huko India kadiri ya maelekezo ya daktari wake, kisha wanamalizia kwa kututaka tumwombee ili afya yake iweze kuimarika mapema ili aweze kurejea nchini!!! Hiyo syllogism imekaaje?
Hata mimi nimeshindwa kuelewa! Wanawaomba Watanzania waendelee kumwombea ili afya yake iimarike haraka!
 
Back
Top Bottom