Nyaraka za Lawi Nangwanda Sijaona (1928 - 2005)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,997
32,146
NYARAKA ZA LAWI NANGWANDA SIJAONA (1928 - 2005)

Katika utafiti wangu wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimebahatika kuona nyaraka kadhaa za wazalendo wenyewe na waasisi wa vuguvugu la kudai uhuru.

Nimeona Nyaraka za Sykes hizi sasa ni maarufu sana hazihitaji maelezo mengi kwani ndizo nilizotumia kwa kiasi kikubwa sana kuandika kitabu cha Abdul Sykes na historia ya TANU.

Nimeziona Nyaraka za Mzee Jumbe Tambaza, Mohamed Kajembe wa Tanga, Germano Pacha na Bilal Rehani Waikela wote wawili wa Tabora, Tewa Said Tewa wa Dar es Salaam na nimeona na kusoma mswada wa kitabu alichoandika Dr. Vedasto Kyaruzi, ‘’The Muhaya Doctor.’’

Mswada huu wa Dr. Kyaruzi una mengi sana katika yale yaliyotokea mwaka wa 1950 pale Dr. Kyaruzi alipochaguliwa kuwa President na Abdul Sykes Secretary wa TAA.

Pamoja na nyaraka hizi nimebahatika pia kuona picha za nyakati wa kudai uhuru kutoka kwa baadhi ya wazalendo hawa.

Katika picha ambazo nimeziona ukitoa picha kutoka Maktaba ya Picha ya Sykes, mkusanyiko wa picha ambazo kwangu mimi zimeweka historia ya pekee ni picha nilizoonyeshwa na watoto wa Ali Msham wa Magomeni Mapipa.

Picha hizi zinaeleza nathubutu kusema historia nzima ya Ali Msham na wananchi wa kawaida waliofungua tawi la TANU Magomeni Mapipa mwaka wa 1954, tawi ambalo lilihamasisha wakazi wengi wa Magomeni na sehemu jirani kujiunga na TANU na hivyo kuongeza nguvu harakati za kupigania uhuru.

Baadhi ya picha hizi zimepigwa kwenye nyumba ya Ali Msham ambako ndiko lilipokuwa tawi la TANU na mahali ambako Mama Maria Nyerere akishinda katika kiduka chake kidogo cha kuuza mafuta ya taa.

Hizi zilikuwa nyakati ngumu sana kwa viongozi wa TANU walioacha kazi kama Julius Nyerere ili kupigania uhuru.

Baada ya mimi kuona picha hizi za Ali Msham na nyaraka nyingi katika historia hii ya uhuru wa Tanganyika nilidhani ndiyo nimefika mwisho.

Katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikiwasiliana na Adam Sijali Sijaona, mtoto wa Lawi Nangwanda Sijaona (1928 – 2005).

Nimefahamiana na Sijali toka miaka ya 1970 tukiwa vijana hapa Dar es Salaam kwa kujulishwa kwake na rafiki yangu Abubakar Kirundu mtoto wa mtoto wa Mbunge wa Dar es Salaam na Meya Omari Ramadhani Kirundu.

Sijali amenionyesha baadhi ya nyarakaza na picha za baba yake zinazokwenda nyuma miaka ya 1950.

Nimesisimkwa, nimepatwa na majonzi na halikadhalika nimefurahi.

Nimesisimkwa kwani kwa kupitia nyaraka hizi nimerudishwa miaka mingi nyuma kuanza kujifunza upya historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kusoma nyaraka na kuangalia picha.

Nimepata majonzi kwa kule kutambua kuwa wazalendo waliojitolea kupigania uhuru wa Tanganyika wengi hawatambuliki na ni suala la muda tu hizi nyaraka na picha za marehemu Mzee Lawi Nangwanda Sijaona zitapotea na nchi itabaki masikini wa historia yake na historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Nimefurahi kwa sababu angalau hizi kumbukumbu zimehifadhiwa mahali ingawa si pake khasa lakini tukizitaka zitapatikana na zikipatikana labda wahusika wa historia ya urithi wetu watachukua hatua ya kuzihifadhi kwa manufaa ya kizazi kijacho.

Nina kawaida kila nipatapo jambo jipya hufanya rejea katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kuangalia nieandika nini katika jambo hilo?
Hayo hapo chini ndiyo niliyoandika:

TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakati uongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama cha siasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifa kudai uhuru.

Suleiman Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa.

Baada ya Vita Kuu ya Pili Mnonji alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katika mashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika.

Vilevile aliwakusanya wapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao.

Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama.

Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta Nangwanda Sijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.

Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chama cha wafanyakazi bandarini Dockworker's Union chini ya uongozi wa Mussa Athumani Lukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyama vya wafanyakazi.

Angalia kadi ya TAA ya Lawi Sijaona hapo chini.
Mimi nilikuwa sijapata kuiona kadi ya TAA:

345419535_912936529778812_7573204646692054672_n.jpg

Lawi Nangwanda Sijaona
345236876_966031821093582_8494332315506471648_n.jpg

1683348931607.jpeg

Kulia Lawi Nangwanda Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz
Hafla ya kumuaga Nyerere Arnautoglo Hall safari ya pili UNO 1956
 
View attachment 2611641
Kulia Lawi Nangwanda Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz
Hafla ya kumuaga Nyerere Arnautoglo Hall safari ya pili UNO 1956
Vema.
Nazama tena hapa baadae nitaibuka na ukoko wa kutosha kutoka ndani ya hili jungu kuu.
 
T14...
"The Muhaya Doctor," hakikuchapwa.
Inasikitisha sana.
Mkuu sasa vipi hizi historia unaweka kwenye archives yani namna gani unazitunza. Miaka 50 ijayo ambapo hautokuwepo una imani zitakuwa zinapatikana. Maana ninachoamini kwenye historia kuitunza ni muhimu kuliko kuitafuta
 
Kila nilichoandika kipo kimehifadhiwa.
 
Lawi Nangwanda sijaona alikuwa anafanya nini nachingwea mpaka kuja kuitwa kutoka huko kwasababu yeye ni mzaliwa wa mnyambe wilaya ya newala
 
Mna...
Sijui.
Lakini mwaka wa 1955 alitoka Lindi akaja Dar es Salaam kama anavyoneka kwenye picha akiwa na Abdul Sykes, Nyerere na Dossa Aziz.

Mzaliwa Mnyambe kafikaje Dar-es-Salaam?
 
Nimeuliza hivyo kwakuwa nimejaribu kuulizia wazee hapa mnyambe wanaomjua vizuri Mzee Nangwanda wanadai hawana kumbukumbu kama aliwahi kuishi nachingwea
 
Niloyoandika yanatokana na historia ya TAA Southern Province kama nilivyoelezwa na Salum Mpunga na Yusuf Chembera wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.

Labda nikuulize swali.

Katika historia ya Lawi Sijaona kuna picha yuko na Abdul Sykes, Nyerere na Dossa Aziz wanamuaga Nyerere Arnautoglo Hall 1956 safari ya pili UNO.

Hili ndilo muhimu katika historia ya TANU na historia ya Nyerere mwenyewe lakini hakuna popote historia hii imeelezwq.

Imekuwaje wewe kilichokushughulisha zaidi ni alikotokea Sijaona na isiwe alifikaje hata akawa katika kundi la Abdul Sykes na Dossa Aziz?

Hao wazee mwaka wa 1953 wakati Sijaona anakwenda Lindi wao walikuwa na umri gani?
 
Shukrani sana mzee wetu. Ni matumaini yangu wenye mamlaka wataona umuhimu wa kutunza hizi kumbukumbu.
 
Back
Top Bottom