Nyalandu ahusishwa na Kampuni Inayotuhumiwa Kwa Ujangili

Inadaiwa Helikopta iliyodunguliwa ilikuwa ya kampuni ya Friedkin Conservation Fund ya kimarekani inayojishughulisha na uwindaji wa kitalii. Taarifa ya serikali ilisema chopa hiyo ilikuwa ya doria ikatunguliwa na majangili ambao walikamatwa miongoni mwao wakiwemo askari gemu.

Tangu huko nyuma kumekuwa na tuhuma dhidi ya kampuni hiyo kujihusisha kisiri na uwindaji haramu.
Swali:
1. Hii chopa ilikuwa ya doria tangu lini na kwa idhini ya nani?

2. Ilitunguliwa na majangili na askari ikifanya ujangili au doria?

Isijekuwa hao askari na wananchi ndugu zetu wanatolewa tu chambo na kubambikiwa kesi ya mauaji makusudi ili kuficha siri fulani.
Hata mimi ndio kilichinijia akilini...
Hao wenzangu na mie wanaweza kuwa wamebambikiwa kesi ili kutupumbaza....haikawii kuwa walikuwa kazini
 
Hiiiiii....sasa tafsiri yake ni nini hapa...
Wale wanaoshitakiwa kwa uuaji walimuua jangili...walikuwa kazini kuwind majangili ila wamegeuziwa kibao or what????!!!!! au mi ndio sielewi elewi...
Mimi nilijiuliza huyu Mwingereza alikuwa mlinzi wa mbuga zetu toka lini???? Chopa ilikuwa inafanya nini kwenye mbuga yetu? nikasema labda ni ulinzi wa wanyama pori kwa msaada wa watu wa UK...
Friendly fire mama... halafu wengine wote tukajazwa mikenge

Hata ile haraka ya hukumu, lengo ni kufunika kombe mwanaharamu apite

Take it from me, mtu akiweza kukaa na wale waliofungwa ataambulia facts zitakazowaumbua sana wazungu na mabwana zao wa kitanzania wanaoongoza kwa ujangili
 
Friendly fire mama... halafu wengine wote tukajazwa mikenge

Hata ile haraka ya hukumu, lengo ni kufunika kombe mwanaharamu apite

Take it from me, mtu akiweza kukaa na wale waliofungwa ataambulia facts zitakazowaumbua sana wazungu na mabwana zao wa kitanzania wanaoongoza kwa ujangili
Hee!! Hivi wameishafungwa tayari? Kama ndivyo mbona kuna kosa linatuongoza kwenda kwenye ukweli?
 
Kuna taasisi nyingi za kibinafsi zinazojihusisha na uangalizi wa wanyama pori in TZ. Tasisi hizi zimesajiliwa na zinafanya kazi kwa karibu sana na wizara au idara husika za serikali. Kwa mfano, kila kampuni inayojihusisha na shughuli za uwindaji wa kitalii ni lazima (this is a government directive) iwe na kitengo cha kuzuia na kupambana na ujangili katika vitalu walivyokodishiwa na serikali. Kampuni hizi zinakuwa na wafanyakazi (kama rubani muingereza) na vitendea kazi kulingana na uwezo wa kampuni. Wanapoingia kwenye hizi mbuga hawaendi peke yao ni lazima waambatane na mfanyakazi wa idara ya serikali kuhakikisha sheria zote zinafuatwa na pale mhalifu anapokamatwa aweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Hiiiiii....sasa tafsiri yake ni nini hapa...
Wale wanaoshitakiwa kwa uuaji walimuua jangili...walikuwa kazini kuwind majangili ila wamegeuziwa kibao or what????!!!!! au mi ndio sielewi elewi...
Mimi nilijiuliza huyu Mwingereza alikuwa mlinzi wa mbuga zetu toka lini???? Chopa ilikuwa inafanya nini kwenye mbuga yetu? nikasema labda ni ulinzi wa wanyama pori kwa msaada wa watu wa UK...
 
Mambo mapya yameibuka Kuhusu kampuni ya kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helkopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani wake raia wa wingereza Ronger Gower.

FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd,Tanzania Game Trackers safari Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati Helkopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili. Kumbukumbu zilizopo Wizara ya maliasili na utalii zinaonesha kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni wa watuhumiwa wa ujangili.

Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ana uhusiano wa karibu na kampuni hizo na hata kwenye kampeni zake za kusaka urais na hatimaye ubunge, Nyalandu alitumia Helikopta ile iliyolipuliwa.

Chanzo: Jamhuri
Chadema someni comments zenu hapo juu kuhusu Nyalandu halafu mjiuulize
 
Hakuna mambo mapya yaliyoibuka,bali ni upumbavu mambo Leo.Je hiyo kampuni imeanza leo?Je huyo Nyalandu ndiye aliyesaini mkataba kama mmiliki wa kampuni?Je kwanini haikuchukuliwa hatua toka mapema?Je watuhumiwa wengine waliyopo bado ndani ya ccm mbona hatuoni mayowe yakipigwa dhidi yao?Kwanini Nyalandu ameanza kuchunguzwa rasmi baada ya kuhama chama?Je ni wangapi wenye mambo ya hovyo waliopo ndani ya ccm?Inamaana wasipohama chama wataendelea kuachwa bila hatua za kisheria dhidi yao?Je kwa mwendo huu nchi itapiga hatua? Kwakweli upumbavu mambo Leo unalitesa taifa.
 
Tatizo la watanzania wengi nikufanya au kupokea mambo pasipo kutumia logic.
 
Back
Top Bottom