Nyalandu ahusishwa na Kampuni Inayotuhumiwa Kwa Ujangili

Kwa mujibu wa jamuhuri waliotungua ni majangili na waliotunguliwa nao ni majangili,Ni kama hawakujuana na wa Helkopta walikuwa wakijificha kwenye kivuli cha ulinzi wa tembo.
Hii inaitwa mbwa kala mbwa. Ila sasa uchunguzi wa kina ufanywe juu ya mahusiano ya waziri wa zamani na hayo makampuni. Tuache kabisa kuoneana aibu
 
Nadhani watunguaji walikuwa ni Majangili local sasa walihisi kuwa Helkopta ile ilikuwa inawafuatilia kumbe na Helkopta ilikuwa inafanya Ujangili, so, Majangili wale local wakawawahi wenzao wakiwahisi kuwa huenda ni askari.
 
nyalandu na maliasili tutasikia mengi saana

Kabisa, huyu jamaa tokaa aingie maliasili maisha yake yalibadilika sana kifedha. Sina ushahidi, ila Anecdotal evidence inathibitiha. Ndio maana alihaha sana alipoukosa uwazir, na kuhangaika sana ili apate hata kamati yake bungeni. kweli tusubiri tutasikia mengi. Ndio maaana nampenda magufuli, atamtumbua tu....
 
Alikuwa mtu wa kwanza ku tweet kuhusu kifo cha yule rubani hata kabla ya wizara kutoa tamko,Aliongea na vyombo vingi vya habari fasta fasta,Sasa naanza kupata picha kwa nini JPM alimbwaga kwenye baraza ingali bado ni kijana mbichi
 
We
Je mtumbua majipu anava gloves au anatumbua kavu kavu maana yana mtindo wa kuamia msishangae mkasikia mtumbuaji nae....

We, mtumbuaji keshaapa atatumbua kila pande jipu litakapohamia. Magu sio wa hivyo, angekuawa anataka majipu yaote, angeotesha alipokuwa ujenzi miaka yote hii. Leo kamng'oa Dau, angekuwa aliotesha jipu nae wakati anajenga daraja la kigamboni asingemtumbua, maana NSSF ndo walifund,.
 
Mambo mapya yameibuka Kuhusu kampuni ya kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helkopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani wake raia wa wingereza Ronger Gower.

FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd,Tanzania Game Trackers safari Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati Helkopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili. Kumbukumbu zilizopo Wizara ya mali asili na utalii zinaonyesha kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni wa watuhumiwa wa ujangili.

Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa aliyekuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ana uhusiano wa karibu na kampuni hizo na hata kwenye kampeni zake za kusaka urais na hatimaye ubunge, Nyalandu alitumia Helikopta ile iliyolipuliwa.

Chanzo: Jamhuri
Hivi ccm kila mtu ni jizi la rasilimali?
 
Wanyama wetu wanalindwa na wageni ?????????????????.Hii mpya inapatikana Tanzania pekee yake.
 
Tanzania bana, yaani majangili yanavuruga pori kuliko wanyama mpaka yanatobozana inakuwa hamna namna tena, ni kuuwana tu.
 
Mambo mapya yameibuka Kuhusu kampuni ya kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helkopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani wake raia wa wingereza Ronger Gower.

FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd,Tanzania Game Trackers safari Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati Helkopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili. Kumbukumbu zilizopo Wizara ya mali asili na utalii zinaonyesha kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni wa watuhumiwa wa ujangili.

Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa aliyekuwa Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu ana uhusiano wa karibu na kampuni hizo na hata kwenye kampeni zake za kusaka urais na hatimaye ubunge, Nyalandu alitumia Helikopta ile iliyolipuliwa.

Chanzo: Jamhuri
na huko.mwiba uchunguzi ufanyike wa kina. inavyoonekana.wanayama wanawindwa.sana maana kila wakati wanyama wako nervous. jicho la ziada linahitajika
 
Sijaelewa ulichoandika, ni kwamba helicopter iliyotunguliwa ndiyo ya majangili? Hau walioitungua ndio majangili?
 
Haya yanawezekana hapa Tanzania tu,kama flow meter hazifanyi kazi miaka 5 na waziri anatuma meseji kuwapa taarifa wahusika chochote chawezekana hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom