Kikojozi
JF-Expert Member
- Mar 24, 2009
- 331
- 2
System haifanyi kazi? Hawa jamaa wa Early Worning Systems wako wapi? Meteolorgical Argency? Kitengo cha maafa PMO?, TISS wanafanya nini? paid for nothing DCs? National granary? Ministry of agriculture, MKUKUTA, MKUZA, PADEP,ASDP afu tuwe na njaa jamani wote hao taasisi zizo plus natural resource abundancy afu tuwe na njaa jamani?
Kwa mfano Marekani, wakulima na wafugaji ambao ni asilimia isiyozidi 3 ya watu wote huko, wanalisha taifa zima, wanajaza maghala ya serikali ya chakula cha akiba na kinachobaki wanauza nje ya nchi.
Hii inawezekana huko kupitia utafiti na matumizi ya science na technologia (mfano matumizi ya mbolea, matrekta, combines, umwagiliaji, nk)
Nchi maskini kama Tanzania, asilimia zaidi ya 80 ya watu wanajishugulisha na kilimo kwenye "vibustani" na wengi wao hawajui kusoma wala kuandika.
Tunategemea nini hapo?