Nini hatma ya nafasi 2 za CHADEMA Afrika Mashariki

Halafu uchaguzi Wa ndani ukifika utaona CHADEMA wanavyojipitisha Zanzibar na ngonjera za UKAWA. wanawaona Wazanzibari Mazuzu yao ya kupitia kutafuta madaraka
Wazanzibar ni mazuzu kwel kwani uongo?! Wanamchagua Seif kila uchaguzi na bado hatangazwi..sio uzuzu huo
 
IMG_20170405_124605.jpeg
 
Mmh na wewe mkuu umekuwa na ujinga wa kibashite na farujoni namna hii?!!!
Ungetafakari kidogo nilichoandika in respect to alichoandika mleta mada na hulka zake ungeelewa maana "iliyomo". Hukujipa muda kutafakari Kiongozi. Mwanzisha uzi unamfahamu vizuri lakini? Au u mgeni hapa jamvini?
 
Wazanzibar ni mazuzu kwel kwani uongo?! Wanamchagua Seif kila uchaguzi na bado hatangazwi..sio uzuzu huo
Anatangazwa mshindi, siyo kila aliyechaguliwa? Hata Taslima jana alichaguliwa lakini alitangazwa Mnyaa ambaye alishinda
 
Wazanzibar ni mazuzu kwel kwani uongo?! Wanamchagua Seif kila uchaguzi na bado hatangazwi..sio uzuzu huo
Anatangazwa mshindi, siyo kila aliyechaguliwa? Hata Taslima jana alichaguliwa lakini alitangazwa Mnyaa ambaye alishinda
 
Nauliza tu maana kila mmoja anasema lake.
Uchaguzi wa nafasi hizo utarudiwa baada ya kesi mahakamani iliyofunguliwa na Mbowe kumalizika. Hii inaweza kuwa ni baada ya mwaka mmoja au zaidi. Si unajua tena taratibu za kimahakama eg upelelezi haujakamilika, hakimu kapata udhuru, DPP kaweka pingamizi, wakili wa mlalamikiwa anaumwa, kesi ndogo ndogo ndani ya kesi ya msingi, rufaa mbali mbali na kadhalika. Yote haya ni kwa manufaa ya mawakili kwani kila siku chadema inabidi iwalipe pesa ya kutakata. Mawakili hao hawatapungua 9 akiwemo Kibatala na Tundu Lissu. Usione kuwa Tundu Lissu akishupalia kushauri chama kiende kudai haki mahakamani, hivi hivi tu. Ni kwamba anakuwa amejitengenezea kazi ambayo chama kitamlipa kwa kusimamia hiyo kesi mahakamani. Haijalishi kesi wanashinda au wanashindwa. Wajinga ndiyo waliwao.
 
Kwanza tukubaliane, uchaguzi wa wabunge wa EAC jana haukuwa strictly partisan, vinginevyo Masha na Wenje wangepata kura 40 za CHADEMA wenzao peke yao.

Kwa hiyo kama C.C.M. kwa kiasi kikubwa waliweza kuweka vyama pembeni, kuna nini kingine kilichosababisha kukataliwa kwa wagombea wa CHADEMA?

Nataka kujikita kwa Lawrence Masha, Waziri na mtumishi wa umma mstaafu, mwanasiasa mzoefu, mwenye elimu na exposure kutoka ndani na nje ya nchi, mwenye uwezo mahiri wa kujieleza Kiingereza ( bahati mbaya sana bado tunatumia hii litmus test kupima weledi wa Mtanzania), na pia mtaalam mwanasheria wa moja ya most prestigious law firms in the nation (IMMMA), na pia mtu mwenye political pedigree, yani uzao wenye historia ya utumishi na uongozi (Baba yake Lawrence Masha ndie alikuwa Nape Nnauye wa Nyerere, msemaji wa TANU wakati wa kipindi kigumu cha kutangazwa, kuenezwa na kupingwa Azimio la Arusha, kabla hajafukuzwa kundini kama Nape.)

Sasa kwa nini Masha akataliwe kwa kura iliyosema "bora tusipeleke mtu EALA kuliko wewe"?

Ukipima kwa vigezo, uzoefu wa kisiasa, kiutawala, kitaalam, kibiashara, Lawrence Masha ana credentials ndefu kupita wote waliohojiwa jana pale in my book. Na katika kujieleza alinivutia kuliko hata kijana wa Maghembe aliyewakuna wabunge kwa Kiingereza laini na utani wa kusema ana sura changa kwa sababu ya vinasaba vyake. Utoto ambao Masha hakuufanya. Masha muda wote ali get to the issues, akiwa very serious minded na akawaomba wamchague japo ni CHADEMA, kwa sura ngumu lakini kwa unyenyekevu mkuu.

Tatizo lililomwamgusha Masha, ukiacha siasa za vyama, ni matatizo ya ujana siku za nyuma, Uwaziri wa Rose Garden!

Watu hawajasahau alivyodharau uongozi aliopewa na JK akageuza ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa ni kwenye ki restaurant cha Rose Garden. Au ki saloon cha Mikasi, kuhojiwa mambo ya nchi kwenye TV huku unafanyiwa pedicure na manicure na haircut. Sijawahi kuona hata huko nje kwenye uhuru wa kila kitu na ma fashion yanakotokea ukakuta Waziri anajibu masuala ya nchi yuko salon anafanyiwa pedicure and manicure na haircut. Unageuza ofisi kuwa vijiwe vya vijana wenzio na wapiga dili wa mjini wakati ule wa Kikwete, mmezungukwa na michepuko yenu mnakula Heineken na makange ya Tilapia wa Kienyeji. Mida ya kazi.

Angalizo kwa vijana madarakani, umesoma au hukusoma, umechaguliwa na wananchi au umependwa na kulindwa na mamlaka za uteuzi, mkumbuke kuna kesho na kesho kutwa, na watu wanakumbuka, basi mjiheshimu wenyewe na kuheshimu dhamana zenu na Wananchi.
 
Ha ha ha! Kama ni kweli, hata Bashite hajafikia level hii na ubashite wake. Labda kwa kuwa CEO wa taasisi yoyote ndiye huwa dira na mhimili wa culture ya taasisi. CEO akilegea tu, kila mtu huingiza culture na dira yake. Hata kwenye familia ni vivyo hivyo.
 
Tangu Chadema wayalambe matapishi yao walijirudisha hatua nyingi sana nyuma!

Dr. Slaa ndio alikuwa mtu smart pale ila hii ya sasa imepwaya sana!

Lisu yuko vizuri tu kwenye sheria na ila kwa mbinu alitakiwa bado ajifunze zaidi kwa Dr. Slaa!
 
Watu wengi hawavifahamu hivyo vitu ulivyovieleza kilichomuangusha ni ccm kukosa akili za kuweka taifa mbele badala ya uchama..Tanzania bado sana kuendelea...

Keep in mind kuna mwenzao wa C.C.M. wamempa kura 23, kundi la Tanzania Bara C.C.M, his presentation was so horrendous mpaka wakasema hawataki hata kumuuliza swali hata moja. Hawakuweka u-chama mbele

Masha amepata kura 126, Wenje 124. Hapa C.C.M wangeleta uchama kina Masha wangepata kura za kina Mnyika na Mbowe na Heche, hazifiki 40. Ma rekodi machafu ofisini na mtaani ndio yamewaangusha.
 
Back
Top Bottom