Nimeupitia mkataba wa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai. Naomba Ufafanuzi

Tatizo la haya maandishi yako ni uoga ule ule wa kitanzania.
Wakati mwingine kujipambanua kuwa na ujuha wa kiasi hiki uwe unawafanya msite kuuonyesha mbele za watu.

Kwa mtu kama wewe huna kumbukumbu kabisa ya mikataba ya IPTL na mingine mingi tu michafu; ambayo waTanzania hawakupaswa kuwa na "uoga" juu yake!
Hopeless Kabisa.
 
GUSSIE, Lord denning, Faizafoxy and co. wanakuja kutolea ufafanuzi juu ya hili!!
Sidhani kama mwanasheria mkuu atakuja na kauli tofauti na ile ya bosi wa TCAA aliyeshughulikia hili suala kwa kina.
Tatizo la haya maandishi yako ni uoga ule ule wa kitanzania.
Nchi inakuwa na watu wenye akili za namna hii, na kwa bahati mbaya ndio wanashika madaraka ya kuendesha nchi unadhani nchi hiyo itabaki salama?
 
Nchi inakuwa na watu wenye akili za namna hii, na kwa bahati mbaya ndio wanashika madaraka ya kuendesha nchi unadhani nchi hiyo itabaki salama?
Kauli ni suala lako binafsi. Tatizo kuna tafsiri potofu kwamba nchi inauzwa, ni ya kishenzi sana kuweza kusikilizwa na vijana wanaokua miaka ya sasa.

Mnajenga chuki mkitumia nguvu nyingi kupinga mradi ambao Hayati JPM alitumia nguvu nyingi katika kuujengea msingi wake kwa maana ya ujenzi wa SGR inayokula matrilioni ya pesa.
 
Wakati mwingine kujipambanua kuwa na ujuha wa kiasi hiki uwe unawafanya msite kuuonyesha mbele za watu.

Kwa mtu kama wewe huna kumbukumbu kabisa ya mikataba ya IPTL na mingine mingi tu michafu; ambayo waTanzania hawakupaswa kuwa na "uoga" juu yake!
Hopeless Kabisa.
Ujuha ni kukariri maisha ya jana ukadhani na kesho itakuwa hivyo hivyo. Ujuha ni kujiona unajua kinachofanyika kumbe unahitaji kuelemishwa kwa mapana.
 
Kauli ni suala lako binafsi. Tatizo kuna tafsiri potofu kwamba nchi inauzwa, ni ya kishenzi sana kuweza kusikilizwa na vijana wanaokua miaka ya sasa.

Mnajenga chuki mkitumia nguvu nyingi kupinga mradi ambao Hayati JPM alitumia nguvu nyingi katika kuujengea msingi wake kwa maana ya ujenzi wa SGR inayokula matrilioni ya pesa.
Nimehitimisha, katika watu 'bogus' niliowahi kukutana nao humu JF, wewe upo kati ya 'top ten'; na hili sitanii.

Kuna wakati mwanzoni nilifikiri unatetea msimamo unaouelewa vizuri; kumbe huna kitu kabisa unachokielewa?
Haya yanayofanyika kwenye mkataba huu wewe huoni chochote kabisa cha kuhojiwa?
Kuna msimamo wowte hapa wa kuushupalia na kujiondolea hata heshima ndogo tu?

Hata kama unalipwa kwa kazi hiyo, si ni bora kula hela hizo na kunyamaza kuliko kujionyesha kuwa mtetezi wa jambo lisilokuwa na utetezi wa kueleweka.

Angalia hapo mwisho unavyojidhalilisha kwa kuhusisha Magufuli katika ujinga huu ambao asingeweza kamwe hata kuusikiliza.
Angerudi leo hii akute msaidizi wake mkuu, Makamu wa Rais ndiye anayesimamia madudu haya, si na ukichaa wake ule angetamani hata kuwacharaza viboko hadharani?
 
Ujuha ni kukariri maisha ya jana ukadhani na kesho itakuwa hivyo hivyo. Ujuha ni kujiona unajua kinachofanyika kumbe unahitaji kuelemishwa kwa mapana.
Kuelimishwa na juha wa aina yako?
Sijawahi kusoma chochote ulichoweka humu JF kikanifanya nifikirie nijifunze kutoka kwako. "Maisha ya kesho" ni kupora mali za taifa na kuwaacha wananchi hawana wanachoambulia. Hiyo ni akili toka wapi?

Hao wanaokukaririsha hayo, huwezi hata ukakaa chini na kuyachambua ukaona yapi yanayofaa nchi yako?
Wewe ni kasuku tu, au 'robot' linalokuwa 'programmed' basi?
 
Hakufafanua lolote. Alijiuma uma tu kuashiria kuwa hajui lolote. Na hiyo ndio tabia ya propaganda. Inafika mahali utajichanganya tu..!
Kweni ule muungano wao wa zile Emirati saba sio kwamba kila Emirati inaweza kuingia mkataba kivyake?

Au muungano wao ni kama huu wetu wa "sambulamaduku"?.
 
Hebu msikilize Dr Muchunguzi anavyofafanua mimi nimemuelewa vizuri

Ana hoja ila kawa kimya kufafanu Ibara au Vifungu vya IGA vilivyo na utata. Ametumia muda wote kusifia kwa jinsi ile ile ya CHAWA na Wabunge. Km Ibara ya 5 inayotoa "exclusive rights" kwa DPA kwa mambo yaliyoainishwa kwenye Appendix 1, ambayo kimsingi ndio yanahitajika kuiweka Bandari katika ushindani
 
M
Na Sam Ruhuza

Naomba ufafanuzi!

Nimeupitia mkataba wa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai.

Dubai ni state kwenye Nchi ya UAE (United Arabs of Emirates) na ndio tumeingia nayo mkataba ikiwa ni yenyewe tu na sio UAE.

Tupate ufafanuzi kwanza kwenye huo uhalali wa kuingia mkataba mkubwa wa Nchi kati ya Jamuhuri na Jimbo.

Pia mkataba unahusu Bandari za Bahari na Ziwa katika Jamuhuri ya Muungano Tanzania ambayo Zanzibar ni ndani ya Tanzania.
TPA (Tanzania Ports Authority) inafanyakazi upande wa Tanganyika tu.
Zanzibar ipo ZPC (Zanzibar Ports Corporation) ambayo ni kwa ajili ya Zanzibar tu.
Kila mmoja TPA na ZPC anamajukumu yake na huru kimaamuzi kujitegemea.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inatambua Bandari zote ni ndani ya Muungano.
Kwa TPA kuwa na Mkurugenzi Mkuu na kufanya kazi Tanganyika tu, na Zanzibar kuwa na ZPC na kuwa na Dg na kufanya kazi Zanzibar tu, hapo tayari kuna uvunjifu wa Katiba na ni kosa kubwa.
Nalo ni vizuri tupate ufafanuzi wake.

Kulingana na mkataba kuitaja Jamhuri ya Muungano Tanzania, je Dubai akiamua kuingia Zanzibar na kuhudumia Bandari za huko kwa mwamvuli wa JMT wakati Zanzibar wanautaratibu wao, je kutakuwa na makosa?!
Hapa napo tunahitaji ufafanuzi wa Serikali.

Kilichopitishwa Bungeni ni mkataba wa Bandari ya Dar Port, wakati mkataba uliosainiwa ni wa Bandari zote, mbona hapo Bunge wamepitisha kitu tofauti na kilichosainiwa Oct 2022?! Je itafuta ule mkataba ambao tayari unatekelezwa?!
Hili nalo tupate ufafanuzi.

Mkataba haionyeshi mwisho wa uwekezaji, je Dubai itakuwapo kwa mwaka mmoja, miwili, kumi, milele, ... inabidi tupate ufafanuzi wa kina ili tuelewe malengo na uwajibikaji wa mkataba kwa pande zote.

Kwenye uwekaji saini,
Kwa Tanzania ameweka saini Waziri wa Ujenzi na Usafirishaji, jambo ambalo ni sahihi kabisa.
Upande wa Dubai ameweka saini CEO wa Bandari Dubai.
Mkataba kati ya Nchi na Nchi halafu Upande mmoja aweke saini Waziri na Upande mwingine CEO, hapo tu panaanza kutia wasiwasi wa uhalali wa mkataba, kama ndivyo ni kwani DG TPA ndio asiweke yeye saini?!
Hili nalo tunahitaji sana ufafanuzi toka Serikalini.

Kwenye mashuhuda,
Upande wa Tanzania shuhuda ni Katibu Mkuu Wizara, ni sahihi kabisa.
Upande wa Dubai, shuhuda hajulikani!
Kuna saini tu bila jina wala nafasi yake.

Hii haijulikani imefanyika maksudi au vipi maana hata asiye mwanasheria mtaalam wa Mikataba angeshtukia mapema!
Inaelekea Dubai walisaini mkataba bila maandalizi hadi wakasahau jina na cheo cha shuhuda!
Hili nalo tunahitaji ufafanuzi, labda kuna jambo hapo sijaelewa.

Naomba pia kufahamu, katika huu mjadala wa Mkataba Bungeni na mtaani ni kwanini Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo kimya??!!
Bungeni kazi ya AG alifanya Spika Tulia maana yeye ndiye alikuwa kama anajibu na kutoa ufafanuzi. Mwanasheria Mkuu ukimya wake kwenye jambo nyeti kama hili linatupa mashaka sana!
Mwingine ambaye yupo kimya ni Profesa Paramagamba Kabudi. Huyu Mheshimiwa tuliambiwa na Mheshimiwa Rais atamsaidia kwenye masuala ya mijadala ya mikataba yaani Chief Negotiator, lakini nae amekuwa kimya!

Nimehoji kupata ufafanuzi huu ili angalau nipate na wengine tupate uelewa mzuri wa haya makubaliano ambayo mkataba tayari umesainiwa October 2022 na Bunge limebariki June 2023, sijui kwanini Bunge limejadili baada ya mkataba kusainiwa, japo Dg TPA alitueleza kilichosainiwa ni MoU ambayo inaisha baada ya mwaka, lakini kilichosainiwa ni IGA (InterGovernmental Agreements. Inawezekana kwenye ufafanuzi wa Serikali nalo hili litatolewa ufafanuzi.

Natumai Watanzania wengi wanapenda uwekezaji. Binafsi sina shida na mwekezaji yeyote, muhimu akidhi vigezo na kutumiza malengo.
Tatizo lipo kwenye uandaaji wa Mikataba na kinachopitishwa na Bunge, hapo ndipo wengi tunaachana!
Tukumbuke tunapotea sana Mikataba mingi na ndio sababu kubwa ya woga wa kupotea.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, njoo utoe ufafanuzi mzuri wa kueleweka kwenye hùu mkataba.

Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿 🤝💪
Mwambie aliyekupatia akupe na majibu ya hayo maswali yako ya hovyo kilaza wewe
 
Nyinyi muliweka wabunge 400 + kazi yao ni kujadili mambo haya kwa niaba yetu, inakuaje tunaumiza vichwa?
Serikali ina jopo la wanasheria bobezi na washauri wa uchumi nguli, hawa wote kazi zao ni kutazama maslahi ya Taifa kwa niaba yetu, Kuumiza kichwa kwa nini?
Comments reserved
 
Kuelimishwa na juha wa aina yako?
Sijawahi kusoma chochote ulichoweka humu JF kikanifanya nifikirie nijifunze kutoka kwako. "Maisha ya kesho" ni kupora mali za taifa na kuwaacha wananchi hawana wanachoambulia. Hiyo ni akili toka wapi?

Hao wanaokukaririsha hayo, huwezi hata ukakaa chini na kuyachambua ukaona yapi yanayofaa nchi yako?
Wewe ni kasuku tu, au 'robot' linalokuwa 'programmed' basi?
Tatizo uelewa mdogo halafu hujui kama hujui maskini ya Mungu. Bandari yako imepata muwekezaji mpya na hana tofauti na kina TICTS.

DP World sio mwekezaji wa kwanza kuja Tanzania, kwanini anapingwa kwa nguvu zote hizi?. Ni ukosefu wa uzalendo wa watanzania kama ilivyo sifa yetu kuu.

Hiyo treni ya SGR imejengwa kwa trilioni 14, pesa nyingi mno. Inarudije hiyo pesa iliyotumika?. Hayati JPM kufikiria tu kujenga hiyo reli tayari kwetu ni changamoto nzuri sana.

Hakuna anayepora mali ya mtanzania, ni mtanzania mwenye kuwa na upeo wa kubadilisha maisha yake ya kesho, sio kuishi kwa kukariri kule kule kwa jana na juzi.
 
Nimehitimisha, katika watu 'bogus' niliowahi kukutana nao humu JF, wewe upo kati ya 'top ten'; na hili sitanii.

Kuna wakati mwanzoni nilifikiri unatetea msimamo unaouelewa vizuri; kumbe huna kitu kabisa unachokielewa?
Haya yanayofanyika kwenye mkataba huu wewe huoni chochote kabisa cha kuhojiwa?
Kuna msimamo wowte hapa wa kuushupalia na kujiondolea hata heshima ndogo tu?

Hata kama unalipwa kwa kazi hiyo, si ni bora kula hela hizo na kunyamaza kuliko kujionyesha kuwa mtetezi wa jambo lisilokuwa na utetezi wa kueleweka.

Angalia hapo mwisho unavyojidhalilisha kwa kuhusisha Magufuli katika ujinga huu ambao asingeweza kamwe hata kuusikiliza.
Angerudi leo hii akute msaidizi wake mkuu, Makamu wa Rais ndiye anayesimamia madudu haya, si na ukichaa wake ule angetamani hata kuwacharaza viboko hadharani?
Povu jingiii jikite kwenye hoja ya kina. Hao waarabu wana biashara yao kule DRC na Rwanda, wanatumia njia ya kisasa ya logistics kuutoa huko na kuufikisha kwao Dubai.

Jielimishe kwanza kabla ya kuanza kutukana usiowajua humu JF, nchi yetu inataka kufaidika na the whole logistics chain ya huyo mzigo ambao utatulipa mabilioni ya pesa.

Kwa mwaka mmoja tu tunaweza kuvuna mpaka trilioni 20 na hayo ni makadirio tu, wakati gharama nzima ya hiyo reli ya kisasa ya SGR ni trilioni 14 kuijenga.

JPM kutafuta wawekezaji kuja kuijenga hiyo reli lengo ije itumiwe na wawekezaji wa aina hii ya DP World, ambao pia wanakuja kuifanya bandari yetu iendeshwe kidigitali, meli kwa sasa inakaa pale nangani kwa siku mpaka sita kwa teknolojia za kisasa za upakuaji na upakiaji wa mzigo haitakaa zaidi ya saa 24 mpaka 48 inakuwa imeshahudumiwa na kuondoka.

Ni suala linalokwenda kupunguza gharama za kuziweka nangani meli nyingi, kumbuka muda ni mali na katika uchumi ni mali kubwa zaidi.

Ondokana na hayo mawazo ya uoga kwamba eti nchi imeuzwa, upuuzi mtupu. Mwarabu asinunue nchi zote za afrika zenye utajiri wa mafuta kama Somalia au Sudan aje aichukue Tanzania!, kwa kipi cha ziada tulichonacho?.
 
Ana hoja ila kawa kimya kufafanu Ibara au Vifungu vya IGA vilivyo na utata. Ametumia muda wote kusifia kwa jinsi ile ile ya CHAWA na Wabunge. Km Ibara ya 5 inayotoa "exclusive rights" kwa DPA kwa mambo yaliyoainishwa kwenye Appendix 1, ambayo kimsingi ndio yanahitajika kuiweka Bandari katika ushindani
Kwenye ile hoja ya kwamba Dubai haiwezi kuingia mkataba mimi naona ameifafanua vizuri amesema hata Emirate ya Ras Al Khaimah wanaweza kuingia mkataba kivyao.
 
Back
Top Bottom