figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,660
- 55,492
Na Sam Ruhuza
Naomba ufafanuzi!
Nimeupitia mkataba wa Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai.
Dubai ni state kwenye Nchi ya UAE (United Arabs of Emirates) na ndio tumeingia nayo mkataba ikiwa ni yenyewe tu na sio UAE.
Tupate ufafanuzi kwanza kwenye huo uhalali wa kuingia mkataba mkubwa wa Nchi kati ya Jamuhuri na Jimbo.
Pia mkataba unahusu Bandari za Bahari na Ziwa katika Jamuhuri ya Muungano Tanzania ambayo Zanzibar ni ndani ya Tanzania.
TPA (Tanzania Ports Authority) inafanyakazi upande wa Tanganyika tu.
Zanzibar ipo ZPC (Zanzibar Ports Corporation) ambayo ni kwa ajili ya Zanzibar tu.
Kila mmoja TPA na ZPC anamajukumu yake na huru kimaamuzi kujitegemea.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inatambua Bandari zote ni ndani ya Muungano.
Kwa TPA kuwa na Mkurugenzi Mkuu na kufanya kazi Tanganyika tu, na Zanzibar kuwa na ZPC na kuwa na Dg na kufanya kazi Zanzibar tu, hapo tayari kuna uvunjifu wa Katiba na ni kosa kubwa.
Nalo ni vizuri tupate ufafanuzi wake.
Kulingana na mkataba kuitaja Jamhuri ya Muungano Tanzania, je Dubai akiamua kuingia Zanzibar na kuhudumia Bandari za huko kwa mwamvuli wa JMT wakati Zanzibar wanautaratibu wao, je kutakuwa na makosa?!
Hapa napo tunahitaji ufafanuzi wa Serikali.
Kilichopitishwa Bungeni ni mkataba wa Bandari ya Dar Port, wakati mkataba uliosainiwa ni wa Bandari zote, mbona hapo Bunge wamepitisha kitu tofauti na kilichosainiwa Oct 2022?! Je itafuta ule mkataba ambao tayari unatekelezwa?!
Hili nalo tupate ufafanuzi.
Mkataba haionyeshi mwisho wa uwekezaji, je Dubai itakuwapo kwa mwaka mmoja, miwili, kumi, milele, ... inabidi tupate ufafanuzi wa kina ili tuelewe malengo na uwajibikaji wa mkataba kwa pande zote.
Kwenye uwekaji saini,
Kwa Tanzania ameweka saini Waziri wa Ujenzi na Usafirishaji, jambo ambalo ni sahihi kabisa.
Upande wa Dubai ameweka saini CEO wa Bandari Dubai.
Mkataba kati ya Nchi na Nchi halafu Upande mmoja aweke saini Waziri na Upande mwingine CEO, hapo tu panaanza kutia wasiwasi wa uhalali wa mkataba, kama ndivyo ni kwani DG TPA ndio asiweke yeye saini?!
Hili nalo tunahitaji sana ufafanuzi toka Serikalini.
Kwenye mashuhuda,
Upande wa Tanzania shuhuda ni Katibu Mkuu Wizara, ni sahihi kabisa.
Upande wa Dubai, shuhuda hajulikani!
Kuna saini tu bila jina wala nafasi yake.
Hii haijulikani imefanyika maksudi au vipi maana hata asiye mwanasheria mtaalam wa Mikataba angeshtukia mapema!
Inaelekea Dubai walisaini mkataba bila maandalizi hadi wakasahau jina na cheo cha shuhuda!
Hili nalo tunahitaji ufafanuzi, labda kuna jambo hapo sijaelewa.
Naomba pia kufahamu, katika huu mjadala wa Mkataba Bungeni na mtaani ni kwanini Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo kimya??!!
Bungeni kazi ya AG alifanya Spika Tulia maana yeye ndiye alikuwa kama anajibu na kutoa ufafanuzi. Mwanasheria Mkuu ukimya wake kwenye jambo nyeti kama hili linatupa mashaka sana!
Mwingine ambaye yupo kimya ni Profesa Paramagamba Kabudi. Huyu Mheshimiwa tuliambiwa na Mheshimiwa Rais atamsaidia kwenye masuala ya mijadala ya mikataba yaani Chief Negotiator, lakini nae amekuwa kimya!
Nimehoji kupata ufafanuzi huu ili angalau nipate na wengine tupate uelewa mzuri wa haya makubaliano ambayo mkataba tayari umesainiwa October 2022 na Bunge limebariki June 2023, sijui kwanini Bunge limejadili baada ya mkataba kusainiwa, japo Dg TPA alitueleza kilichosainiwa ni MoU ambayo inaisha baada ya mwaka, lakini kilichosainiwa ni IGA (InterGovernmental Agreements. Inawezekana kwenye ufafanuzi wa Serikali nalo hili litatolewa ufafanuzi.
Natumai Watanzania wengi wanapenda uwekezaji. Binafsi sina shida na mwekezaji yeyote, muhimu akidhi vigezo na kutumiza malengo.
Tatizo lipo kwenye uandaaji wa Mikataba na kinachopitishwa na Bunge, hapo ndipo wengi tunaachana!
Tukumbuke tunapotea sana Mikataba mingi na ndio sababu kubwa ya woga wa kupotea.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, njoo utoe ufafanuzi mzuri wa kueleweka kwenye hùu mkataba.
Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿 🤝💪