Entreprengineer
Member
- Jan 22, 2020
- 27
- 35
Kutokana na mtindo wa maisha niliokua nao (ulevi) nilijikuta kwenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU mara nne baada ya kufanya ngono zembe au kupata ajali ya kinga kupasuka etc. Kila baada ya kupata ajali nilikua nakimbilia dawa za PEP, sasa mara ya mwisho kuna mhudumu aliniambia dawa za PEP sio nzuri kutumia mara kwa mara kwa sababu zinaweza kukujengea usugu au kuzoea mwili, hii ikanijengea hofu kwamba kwa sababu nimeshazitumia huko nyuma what if nikipata risk nyingine siku za mbeleni je dawa za PEP zitanisaidia?
Je, dawa za PEP zina limit ya matumizi? Naomba ushauri wa kitaalamu maana nimejikuta nawaza sana mpaka napata depression. Natanguliza shukrani...🙏
Je, dawa za PEP zina limit ya matumizi? Naomba ushauri wa kitaalamu maana nimejikuta nawaza sana mpaka napata depression. Natanguliza shukrani...🙏