incredible terminator
JF-Expert Member
- Aug 1, 2016
- 2,495
- 4,155
Habari Wakuu. Binafsi sijaleta mada hapa kama njia ya kutetea watu kuishi maisha yanayohatarisha afya zao. Ila nakumbusha tu kwamba hapa JF kufikia 20100, wote hatutakuwepo pasipo kujali wanaolinda Afya na wasiolinda.
Binafsi mimi napenda kuishi katika maisha yanayonipa furaha ila licha ya yote naogopa sana kuwa kikwazo katika maisha ya mtu, kutumika kumkwamisha mtu kwa namna yoyote kwangu mimi naamini ndio Dhambi kubwa ambayo naomba mwenyezimungu anitenge nayo. Ila linalohusu maisha yangu binafsi huwa sipendi kushauriwa.
Ni wazi kuna watu wanajishaurisha kama hamna kifo mbele yao na kujikuta wakijiweka mbele kutabiria wenzao maisha.
Kimsingi ni kwamba unywe pombe kali, unywe soda, Unywe maji, usitumie chochote cha kiwandani bado sio njia ya kukwepa kifo,
Kifo ni asili na maradhi pia kwa namna yoyote ile haviepukiki lazima utaenda tu. Hii ni sawa na miaka hiyo tukiwa Shule mwalimu akianza kutoa adhabu ya vivobo tulikuwa tunakimbia nani wa kuanziwa na hata tukajisahau kwamba wote tupo kwenye foleni ya kuchapwa kwa zam na hakuna aliepo salama kuliko mwenzie.
Kuna watu wanatumika kuharibu Biashara za watu. Wakidhan kuwa wao wako salama kwa kuepuka matumizi ya bidhaa fulani ila linapokuja swala la kifo kama asili n ukamilifu huwa hawakwepi kwa lolote.
Ushauri wangu kila mtu aishi maisha yake yanayompa furaha wala msitishwe tishwe.