Nimepigwa na wanaojinadi wanauza sure bets fixed matches, hakuna kitu kama uhakika kwenye kubeti, ni mbinu ya kula pesa zetu tunaoingia tamaa

😂 ila unahonga laki
Mkuu wewe ni mnufaika wa hizo ''fixed'' nini? Hakuna mwenye uhakika na betting, na ingekuwa hivyo basi betting ingesha collapse siku nyingi. Hizi za wachezaji kupanga, zinatokea mara moja moja tu, na hakuna mtu mwenye akili timamu atakeyewashirikisha watu wengi.
 
Nilitembelea website flani wanaposti mikeka imetiki yani sure odds fixed matches, nikalipa dola 30 takribani shilingi elf 80 kuungwa kwenye group, humo ndani ni upuuzi mtupu game wanazoweka ni chache zenye odds za 1.01 yani ukiweka laki ushinde buku lakini ukija kwenye website zao wanadanganya wanaweka mikeka ya mechi zilizokuwa na odds kubwa kwamba imetiki.

Nikaja hapa bongo kuna mdau alikuwa anapost hizi sure bets na mikeka, na kuna watu wanasifia kabisa wameshinda kumbe ni yeye mwenye anajichatisha, nililipa elf 15 ili niungwe group, muhuni sana huyu anapost odds baada ya mechi kuisha ukienda page yake anaweka mikeka imetiki itakuwa ana edit
Mbona mnaliwa fedha kizembe hivi? Huu ni utapeli kama utapeli mwingine wowote. Yaana unaamini kuna mtu anaweza kupatia odds na hataki kupiga fedha bali anataka kusaidia wengine wapige? Ni yale yale ya mganga wa kienyeji anayeishi kwenye kibanda cha nyasi kuuza dawa ya kuwafanya watu kuwa matajiri.
 
Katika ku bet kuna jamaa mmoja namuona X jinsi anavyomkong'ota muhindi. Jamaa hasemi ni fixed matches ila ana bahati ya kula mkeka kwa kiwango kikubwa sana japo stake zake ni za kibabe sana. Kuhusu fixed match niliona kama mara mbili akisanua watu kuwa hii ni fixed matches katoa katika vyanzo vya kuaminika na anatoa code hapo hapo X bure bila hata malipo. Na mwisho wa siku anafurahi na wana waliofuata.
Fixed huwa zinatoka mara chache chache sana.
 
Mkuu wewe ni mnufaika wa hizo ''fixed'' nini? Hakuna mwenye uhakika na betting, na ingekuwa hivyo basi betting ingesha collapse siku nyingi. Hizi za wachezaji kupanga, zinatokea mara moja moja tu, na hakuna mtu mwenye akili timamu atakeyewashirikisha watu wengi.
Sijawahi kupata sure fixed kwa kununua ila kuna ambazo zinakuwa leaked nazipata na huwa zinatoa.

Kununua sinunui maana wengi wanauza fake lakini fixed game zipo mkuu.
 
Tupe mifano zilivuja lini mitandaoni mfano humu jamiiforums kwenye jukwaa la michezo ?

Hapa bongo penyewe tunajua kuna wachezaji wanacheza hii michezo ya kujifungisha huwezi kuzikuta hizi siri zinazagaa mitandaoni, ikitokea hivyo Fifa wakijua wanaweza kufungia mpaka timu.
IMG_1288.jpeg
IMG_1289.jpeg
 
Katika ku bet kuna jamaa mmoja namuona X jinsi anavyomkong'ota muhindi. Jamaa hasemi ni fixed matches ila ana bahati ya kula mkeka kwa kiwango kikubwa sana japo stake zake ni za kibabe sana. Kuhusu fixed match niliona kama mara mbili akisanua watu kuwa hii ni fixed matches katoa katika vyanzo vya kuaminika na anatoa code hapo hapo X bure bila hata malipo. Na mwisho wa siku anafurahi na wana waliofuata.
Fixed huwa zinatoka mara chache chache sana.
Real Niger huyu

Jamaa hana baya
 
Jiulize na ufikirie mara 10..

Mtu anakwambia anauza 5 odds za uhakika, nawewe kwa tamaa zako unatoa pesa yako kununua odds.
Kama ana uhakika na hizo odds 5, kwanini asiweke 10 million ili ashinde 50 Million..?
Au unafikiri anakujali sana...? Kama anakujali sana kwanini asikupatie hizi odds for free...?
 
Unakuta mtu anakuonyesha mikeka yake ya jana ameshinda 2M, leo ana odds 200 ni fixed anashawish watu wanunue lakin yeye mkeka huohuo anastake elfu 20, na jana yake ameshinda 2M, kwann asiweke angalau 500K apate 100M.... hesabu ndogo km hiyo
 
Ndio huyo huyo. Jamaa kwenye betting ana ufalme wake yeye odds zake ni mbili tu ila stake zake ni heavy na sio mchoyo kushea na washikaji. Sio wengine wanasubiri mechi iishe ndio wakuoneshe wameshinda mkeka.
kama ni uhakika kwanini hautumii hela yako yote kuweka mzigo ili upige hela
 
Back
Top Bottom