Nimelima nyanya heka 1 nimepata faida ya Tsh. Milioni 9 ndani ya miezi minne

Kwa faida ya wanataka kulima

SHAMBA.

Mimi shamba ni la nyumbani ni Bure Pamoja na mbolea samadi ilikuwa Bure pia.

Uaandaji pamoja na kulimiwa ni Bure pia Kuna ng'ombe kwetu na jembe la kukokotwq na ng'ombe (pirau)

MBEGU :-Nilinunua mbegu ya nyanya kutoka Epinavi nitaweka picha zao na mawasiliano Yao hapa chini.

Awali niliambiwa gram 50 kama ingeota vizuri ingetisha kupanda Heka1 yote.

Hivyo nilinunua gram40 ya mbegu aina ya Tanzanite F1
Nikanunua gm10 Dhahabu F1
Nikanunua gm10 imara f1

Bado hazikutosha Kwa heka moja
Hivyo nilitafuta Kwa mkulima mwenzangu Ambae aliniambia yeye ana mbegu inaitwa Onex kama sijakosea na aliikamua tu sio pure.

Kwa vile nilitaka kupanda na zisipishane nikanunua kwake jamaa na kupandikiza

Mnamo trh7/3/2024 nikianza uhamishaji wa Miche kutoka kitaluni na Hadi trh 13 zoezi la upandaji liliisha.

Palizi nilitumia vijana wangu wa kazi ambao wapo4 tu

MBOLEA YA VIWANDANI:-nimeweka mara5 na Kila kuweka nilikuwa natumia mifuko2 au 2 kasoro.

(Hapa mbolea zinatofautiana kulingana na umri wa nyanya)

VIUA TILIFU/KUVU:-Nimetumia kadiri inavyohitajika Sina idadi sahihi.

VIFAA :-Majembe,solo nk pia.

MAVUNO RASIMI NA MAKUBWA :-
Mchumo wa kwanza tray 47 garde1
Grade2 try4
Mchumo wa 2 box 63¹
Grade2 box9
mchumo wa3 grd1 try54
Chenga13

BEI:- Awamu ya 1 niliuza grad1 Kwa 45k chenga32k

Awamu ya pili grd1 niliuza Kwa 53 chenga42 nyanya ilipanda bei

Awamu ya 3 bei grd1 48k
Chenga25k.

Kwa ujumla wake nilipata Tsh8,800,000 na Hela kadhaa mesahau

Baada hapo nikianza kuuza Kwa bajaji
Na kwenye matenga hapa Sasa ni changanyikeni tu maana sikuwa shambani na kupigwa nilipigwa na vijana pia sikuwa na jinsi kutokana na kubanwa na kazi na hata kuandika idadi nilishindwa.

Mara kadhaa mzee wangu ndo alihusika na mauzi akiwapo shambani

Na pesa ilikuwa unatumiwa kulingana na mauzi maana ilikuwa Kila siku natumiwa Hela ambayo Kwa ujumla ni nilipata 5,378,000/= maana msg nilikuwa sifuti.

Ukija jumlisha zote Ni Tsh 14,178,000/=

Wafanyakazi ni4 Kila mmoja 500k Jumla 2,000,000/= zilibaki ni dhana za vilimo madawa na mbegu nk.
Hongera sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom