Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 1,679
- 4,647
Habari kaka, mimi ni mama wa mtoto mmoja mwenye miaka 7 sasa. Nina miaka 2 tangu kuondoka kwa mume wangu, na niliondoka huku nikimuachia mtoto na kila kitu. Sababu ya kuondoka kwangu ni kwamba nilimpata mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Kwa sababu alikuwa na pesa, alinidanganya na nikamuacha mume wangu.
Nimekaa na yule mwanaume, na ameshanipeleka mpaka kwao. Mama yake ananipenda sana. Lakini nimekuja kugundua kuwa hawamtaki mke wake kwa sababu ya kabila ila mwanaume bado anaendelea naye. Sasa nataka kuondoka hapa nirudi kwa mume wangu kwani nasikia amejenga nyumba mbili na kuna mwanamke anayeishi naye.
Mimi nina ndoa ya kanisani, hivyo bado ni mke wake kwa kuwa hajanipa talaka. Sababu ya kuja kwako ni kwamba, najua mume wangu atanisamehe kwa kuwa hawezi kuniacha ninapokuwa karibu naye. Shida ni mama yake, ambaye alichukua jukumu la kulea mtoto wangu baada ya kuondoka kwangu. Sasa yeye ndiye mwenye sauti nyumbani.
Yule mama ananichukia sana, na najua atakataa nikitaka kurudi. Nimejaribu kwa waganga ili achanganyikiwe na aondoke nyumbani, lakini imeshindikana. Nataka tu unipe ushauri wa nini nifanye ili mama mkwe aondoke, nipate uhuru na mtoto wake. Hapa nilipo, nimechoka kudanga, mwanaume haachani na mke wake na ananizees
ha tu!