hewizet
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 2,409
- 1,507
we suni au shia kwanza?? tuanzie hapaWana bodi habari za usiku.
Mimi ni mkristo wa kuzaliwa na kubatizwa, mwaka 2000 nilipata kipaimara yangu kama taratibu za kanisa letu zilivyo.
Sitaki kuwachosha sana kuna mambo ambayo yamenivutia sana na kupelekea kuamini kuwa dini ya kiislam ni dini ya kweli. Mimi ni mzaliwa wa kaskazini tena kijijini haswa, nimezaliwa na mpaka naanza shule ya msingi na kumaliza elimu ya msingi nilikuwa sijui kama kuna uislamu duniani, nilipoanza form one ndiyo nikaanza kusikia kwenye kipindi cha dini kuwa kuna dini ya kiislamu, nimesoma mpaka namaliza chuo sikuweza kuamini kabisa kuwa waislamu nao ni wacha Mungu kama dini zingine.
Baada ya kutoka chuo nilipata mkataba wa kufundisha shule ya kiislamu form one na two (math) kwa mkataba wa miezi sita, shule hiyo walimu zaidi ya 90% tulikuwa wakristo na wanafunzi zaidi ya 75% walikuwa wakristo, walimu wa math tulikuwa wawili wote wakristo, mkataba wangu ulianza mwezi July lakini baada ya miezi 2 tulibadilishwa mimi nikaanza kufundisha form III – IV.
Baada ya kama miezi 3 BAKWATA(W) walianza kuhoji kwanini shule ni ya kiislamu lakini walimu wengi ni wakristo? Shehe wa (W) sitaki kumtaja maana mpaka sasa hajahama pale alituita ofisini kwake walimu wote na kutueleza madai ya BAKWATA lakini yeye akasema tufanye kazi bila tatizo na yupo tayari kututetea popote pale. Baada ya mkataba wangu kuisha Dec Shehe alinitaka niongeze mkataba pamoja na kuongezewa maslahi kitu ambacho sikutaka sababu lengo langu ilikuwa kupata mtaji wa kuanzia maisha na kujikita kwenye mambo mengine. Kwa heshima ya Shehe nilikubali kuendelea bila mkataba pindi wakipata mwalimu mwingine wa math mimi niondoke, nilikaa miezi 4 hatimaye mwalimu mwingine akapatikana lakini shehe akasema nisiondoke mpaka shule ikifungwa mwezi May. Muda wote huo nyumbani kwetu hawakujua nafanya nini sababu nilijua nikisema home mambo yatakuwa mengine kulingana na mtazamo wa home juu ya uislamu.
Nimejaribu kufikiria matendo ya hawa ndugu zetu waislamu ukilinganisha na wakristo wenzangu hakika naona waislamu ni watu wa haki sana kuliko sisi wakristo. Nitatoa mifano michache,
1. Mhe Mwinyi amewahi kuzabwa kibao mbele za watu akasamehe.
2. Mzee JK kama siyo yeye mimi na jamaa zangu huku kijijini tusigepata hiyo elimu kidogo tulionayo sababu wazazi wetu ni mafukara sana.
3. Mzee JK wapinzani walimtukana sana lakini aliwaita Ikulu wakakaa, wakanywa na kuongea.
4. Mzee JK Maaskofu walimsema lakini kwenye harambee ndiyo alikuwa anaziendeshaa bila kujali maneno yoyote.
5. Mzee JK aliteua mpinzani ambaye ni mkristo kuwa mbunge.
6. Mzee JK alimsaidia mama mmoja kumpeleka mtoto wake India alipata ajali ya bodaboda, mama huyu anasema siku moja akiwa India JK alienda kumsalimia yeye pamoja na Watanzania wengine, mama huyu ni jirani yangu huku kijijini kwetu.
7. Mzee JK tukio lolote lilipotokea alikuwa mstari wa mbele bila kujali hadhi yake.
8. Mhe Buhari na Macky Sall wameamua kumwondoa Rais wa Gambia ambaye ni muislamu mwenzao baada ya kuona anataka kudhulumu haki ya wananchi.
9. Shehe Ponda amekuwa akitetea maslahi ya watu wote bila kujali rangi wala dini zao.
Hayo ni machache kati ya mengi, nikiangalia matendo ya wakristo wenzangu(Kagame, Nkurunziza, Mseveni, Kabila, Mugabe, Askofu Mokiwa, Mzee wa upako n.k) mpaka nakata tamaa kabisa kwa matendo yao. Kumbe dini ni matendo na siyo maneno.
Mtanisamehe kwa uandishi usio na mpangilio mzuri sababu mimi siyo mtaalamu wa fani hii. Pia huu ni mtazamo wangu binafsi
Nawasilisha jamani