mose
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 404
- 387
== Jinesesia: Mwanzo wa DHAMMA==
ALRIGHT
HAKIKA, vitu vyote vimefanyika kwa ishara na alama…
View: https://www.youtube.com/watch?v=Slt45rz-OUY
AKILI ni chombo cha ‘kufahamiana’ kiishara na alama – ishara na alama kwa ajili ya ufahamu katika ‘miili ya uweza’ na kujichagulia kwake kiwakati kupitia ‘Roho ya Utambuzi’; hili ndilo hukadirisha ukweli wa kusema ‘Asiye na Akili’ hana ‘Dini’.
Usentienti, Konsayansi na Ufahamu ni ‘Chaji ya Uweza-nguvu-utukufu’ katika ‘muktadha akilifu’ wa ‘Kujiwazia Utu’.
[(1) Hisia na Kujisikia--‘Usentienti’, (2) Akili ya Udhamirifu wa Mambo--‘Konsayansi’, na (3) Mwanga wa Nuru ya Utambuzi/Kujitambua--‘Nuru ya Ufahamu’]
Muktadha ni dhana ya Kiuno na Ufikirifu mifumo ambavyo ‘Vina vya tafsiri’ na ‘Udhamirifu wa Mambo’ hupelekea ‘Utashi’ kwa ajili ya kujichagulia ‘Sura na Utukufu’ wa (1) Kuwa ama (2) Kuja-Kuwa—Maisha daima ni mchakato… Mchakato wa ‘Mageuzi’ ilivyo ni safari ya UTU-MAISHA-UISHO.
‘Roho ya Utambuzi’ ni mambo ya ‘Jaala’ na ‘Kumbukumbu Uzoefu’; kuwa kwamba, UTU-MAISHA-UISHO ni ‘mafumbo ya Imani’ ambavyo ‘Kujiwazia UTU’ hupata jamvi la hatma za kimageuzi ili kuakisi muktadha akilifu wa ‘Kuwa ama/na kuja-kuwa’… Kwa rizayati ya Elimu 3.0, haya ndiyo yenye kuja na mashauri ya Mtume Paulo kuhusiana na ‘Kuwa Mtoto—Kufikiri kama mtoto’ na halafu Kuja kujijua kama vile ‘Mungu’ anavyomjua ‘mtu/’kujulikanavyo na Mungu’.
Kujiwazia Utu, ndiyo chanzo cha ‘Ontolojia ya Taasisi’ na basi akili ni chombo cha nasibu ya fizikia na metafizikia ya uzima wa miili ya uweza. Mwili wa mwanadamu, mwili wa nyama, ni mwili wa uweza—mwili wa uweza katika fiziki na hali kupitia akili una metafizikia yake. Na basi fiziki, ulimwengu wa maumbile na metafizikia ni ulimwengu wa maumbile yaliyositirika na huku yakishiriki uweza, nguvu na utukufu na mwili-fiziki.
Katika lugha za kimazungumzo—mazungumzo ya Jamii ya Waswahili, maarifa yasiyo rasmi, lau kujaribu kuotea otea habari za mawezekano ya ‘uweza, nguvu na utukufu’—mambo ya metafizikia ya mtu/utu ndiyo hutajwa kama ‘Nyota’--’Mambo ya Nyota’ tena yale yenye kufungamana ama/na kuingiliana na ‘Bahati’ ama ‘Mikosi’ ya mtu katika muktadha akilifu wa UTU-MAISHA-UISHO.
‘Kujiwazia Utu’ na tena muktadha akilifu wa UTU-MAISHA-UISHO ndiyo asili ya Dhahiri-Macho na Dhahiri—Kiini Macho ya yote yaikadirishayo jamii na mambo yake—mambo ya nyakati zake kwa kuwa ili jamii isimame huwa na ukadirifu wa ‘Ontolojia ya Taasisi’ yenye kujenga mambo ya ‘Ushawishi’ na ‘Hisia’ kwa Mapana ya Hisia ya ‘Utu’ wake.
Mapana ya Hisia ya Utu ndiyo khasa asili ya ‘Mifumo’ kwa kuwa matendo ya jamii na hatma zake hukadirisha ‘Sura na Mienendo’ ya fahari ya utamaduni wake. Matendo ya jamii huja kwa mila, desturi na jadi ambavyo hutokana na miongozo ya jamii husika. Basi ndiyo kuwa ‘Matendo’ na ‘Miongozo’ huakisi ‘Udhamirifu wa Utu’. Zao la ‘Taasisi’ na ‘Wakati’ ni ‘Mifumo’…
Kwa Jamii ya Watanzania, tuseme, jamii ya watanzania kama Jamhuri ya Watu; Katiba ya Nchi ndiyo Muungozo mkuu wa Sura ya Nchi na Tawala. Kwa mintarafu ya hili, Katiba kimsingi hubeba ‘Tamko la Kujiwazia Utu-Jamii’--kubayanisha asili ya Miundo ya Utendaji, Kujitengenea na Vinasaba vya Mwiili wa Uweza wa Nchi-dola—mambo ya Dola, Vyombo vya Dola na nguvu zake, na Mkataba kati ya ‘Watawala’ na ‘Wataliwa’ kwa ‘Siasa za Uwakilishi’.
Hayo ndiyo kwa wenye kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza huyataja kama ‘Governing Structures’, ‘Nation-State Organization’ na ‘Specific Institutional Guidelines’; Pia ndiyo ‘State Institutionalization’, ‘State Instruments and Mandates’ na ‘Civil Contract’ na basi ‘Representative Liberal Democracy-- democratic Institutions/institutionalization’.