- Thread starter
- #81
Inatokea post namba 67.
Nimekaa kaa muda nikajihisi kama kiusingizi, nikaingia pangoni ndani, nikarekebisha mto wangu wa mchanga nikafunika shuka juu ya mchanga, nikachukua mkebe wangu wa pete nikauweka chini ya shuka, pale pale nilipoukuta mwanzo, nikaiweka bakora pembeni hyangu nikajilaza, ukanipitia usingizi mzito sana.
Katika kulala nikaota kaja mtu ambae sura yake simuoni, ananisemesha, ananambia mimi ndio mwenye hiyo pete ulioivaa, leo saa 9 kamili uwe nje ya pango upande wa mtoni kuna uwanja mzuri, nataka kuongea na wewe. Ndoto ndio ilikua hivyo tu, haina jambo lingine zaidi.
Baada ya muda, nikaamshwa na wanafunzi wa babu, wakanambia bibi yako kishafanya mambo, amka umoge tule. Nikaamka, nikaenda mtoni nikajiingiza kwenye maji, leo nikakwepa kabisa sehemu ya dimbwi la kamba, maana nilipopita nawaona wamejazana hasa. Nikaokoga voizuri nikarudi. Vijana wa babu wakanambia tuweke mambo, leo kuna supu ya kamba hapa na pilau la kamba, Bibi kasema hii ni kwa ajili yako tu. Nikawaambia kama ipo supu, kwanza nitakunywa supu, chakula baadae maana nililala mpaka nikae muda kidogo mwili uchangamke. Ile kabla hawajanitilia supu, babu akaja.
Bwana mkubewa leo nimekija kula na wewe, nasikia vimeletwa vitu sio vya kawaida huku, unanitia wivu bwana. Niakcheka, nikamwabia wewe unavifaidi peke yako hivi. Babu akasema, biboi yako sasa hivi anajitutumua kwa ajili yako, hana nguvu kama za zamani lakini si haba, kwa kula tu, hana hiana.
Tukatia supu tukanywa wote, supu nzuiri kweli kweli, bibi yangu kusema kweli anajua kupika, ilikua na chumvi kwa mbali na ina pili pili manga kwa wingi. Yaani sijawahi kunywa supu ya kamaba nzuri kama ile.Babu nae akaisifia, akasema, hii hata mimi sipikiwi, naona bibi yako leo kaamua. Tukamaliza supu, vijana wa babu wakasema sasa hivi hata pilau haiingii tena mpaka baadae. Tukaamka tukatawadha tukasali woyte pamoja, Babu akasema leo nitakutembelea usiku baada ya kusali isha, kuna wageni wengi wacha nikawaone. Leo babu siku yako ya mwisho kulala pangoni. Ukitembelewa na watu usiogope ni kawaida ya hapa. Nikamwambi nishatembelewa babu. Akasema najua, tutaongea zaidi usiku, leo tegemea kutembelewa sana mpaka kesho. Akatuaga akaondoka zake, akawaambia na wanafunzi wake, twendeni, kuna wageni wengi leo. Mwacheni huyu Bwana Mkubwa, kishapazowea huku.
Kweli nilishpazowea kiasi nilihisi kama kero wakiwepo wanafunzi wa babu, nilikua nataka niwe peke yangu sehemu ile, walipoondoka nikatazama saa, nikaona saa 9 bado dakika tano, nikaona goja niende uwanja wa pembeni kama nilivyoota, karibu ya mto.
Itaendelea.