- Thread starter
- #41
Sijaelewa, marejesho? Wapi?Mkuu vipi umepeleka marejesho nini?
Sijaelewa, marejesho? Wapi?Mkuu vipi umepeleka marejesho nini?
Kaka unachapia sana.Ilikua ni siku chache kabla sijatimiza miaka 18. Nilipelekwa Tanga, kijiji kimoja kipo karibu sana na mpaka wa kwenda Kenya. Kabla ya kuingia huko kijijini ndani kuna kimji kinaitwa Duga. Ilikua sio mara yangu ya kwanza kupelekwa huko kwa mambo ya kimilla na jadi.
Lakini hii ya safari hii ilikua kidogo yakutisha. Kijiji chenyewe kipo ufukweni kabisa na kina miti miwili inapita, mmoja Kaskazini ya kijiji, huu mkubwa kiasi na mmoja mdogo uanpita Kaskazini ya kijiji. Kwa hio kijiji ni kama kimezungukwa na maji, maana mashariki yake ni bahari ya hindi, Kaskazini mto na kusini mto. Magharibi tu ndio kuna njia ya kwenda mpaka barabara kjiubwa ya lami, ambayo ipo kama kilomita 3 au 4 kutokea hapo kijijini.
Safari hii ilikua ni nzito kidogo kwa sababu niliambiwa unaweza kukaa kijijini huko wiki moaja au mbili itategemea na "babu" huko ataamua kama mambo yako tayari au bado.
Nilifatana na Baba na Mama yangu kwenye gari la nyumbani mpaka hapo barabara kuu kutokea Tanga, hapo nikakuta vijana wawili wakubwa kwangu, wananingoja na baiskeli mbili, moja ya kunipakia mimi na moja ya kupakia mizigo yangu.
Mizigo yangu kweli ilikua mingi, yangu binafsi lilikua ni begi kubwa na racksack ya mgongoni, lakini kuna mabiksi kama matatu makubwa yalia ya mama akanambia haya yote mkabidhi babu yako mifika.
Basi tukaagana pale, wao wakanambia ukimaliza kazi yako watakuleta hapa barabarani utapanda gari za kuja Tanga, sisi utatukuta Tanga, tutakuja baada ya wiki mbili, kama utakua umemaliza kabla ya wiki mbili ukifika Tanga tusubiri. Wakaondoka zao, na mimi kapakiwa kwenye baiskeli kama abiria, na nyingine ikafungashwa ile mizogo yetu yote ikatangulia.
Hatukuchukua muda sana, tukafdika kijijini, moja kwa moja mpaka kwa babu yangu. Babu yangu tunajuana sana, na alikua ni sahiba yangu sana, ni mtu ma story ya kizamani na mimi nilikua mdadisi sana. uzuri wa babu alikua hakwepi swali lolote utalomuuliza na alikua hamumunyi maneno, anakujibu mpaka likuingie. Nilikua namshangaa sana, kwani hakuna swali lilililokua gumu kwake. Hata niwe na swali, mwenyewe naliona gumu kweli, nikimuuliza bau ananijibu huku ananisifia "swali zuri sana hilo", ananijibu kiurahisi kabisa, mengine huwa anavhukua muda kuyajibu, mtindi wake wa kuibu ulikua kama anakusimulia hadithi, anaweza akatpka kabisa nje ya swali ulilomuuliza lakini atakuhadithia mpaka utalipata jibu. Mara nyingi akikujibu basi lazima utakua na maswali mengine mawili matatu ya kuuliza. Kwa ufupi alikua anaelewa kufungua "kichwa" kwa mujibu baba yangu.
Tutaendelea baadae.
Nimerekebisha.Kaka unachapia sana.
Jaribu kupunguza yasiyo ya maana sana kama mihogo na magendoNimerekebisha.
Na inspiration quotes kama mia hiviafu anapost God Did
🤣🤣🤣🤣HoyeeéeeeeeWashirikana hoyeee..
Alisikika Makongoro Nyerere
mti mmoja unapita kaskazinikina miti miwili inapita, mmoja Kaskazini ya kijiji, huu mkubwa kiasi na mmoja mdogo uanpita Kaskazini ya kijiji.
Muandishi❌mti mmoja unapita kaskazini
Niliposikia miti inapita nikaishia hapa😂😂
kwan muandishi ulikua unakimbilia wap
🤣🤣🤣🤣Kiongozi kwanini usituambie tu hicho ulichokiona baada ya kufumbuliwa macho. Dah, unatuzungusha kichizi. Be straight to the point
🤣🤣🤣🤣🤣Kiongozi kwanini usituambie tu hicho ulichokiona baada ya kufumbuliwa macho. Dah, unatuzungusha kichizi. Be straight to the point
Kwahiyo mihogo haina maana😅😅Jaribu kupunguza yasiyo ya maana sana kama mihogo na magendo