YNIM
JF-Expert Member
- Aug 29, 2007
- 2,215
- 24
Unaweza pia kupunguza, ‘mungu akipenda’ una acha kabisa. Muhimu ni kubadili mtindo wa maisha.Usipunguze, acha kabisa.
Simba.
Unaweza pia kupunguza, ‘mungu akipenda’ una acha kabisa. Muhimu ni kubadili mtindo wa maisha.Usipunguze, acha kabisa.
Simba.
Tunamalizia mashetani ya Kibuki Unguja, halafu tutaingia vijini vya Kipemba huko Kojani, tukitoka hapo tutaelekea visiwa vya Comoros, huko Njuani, kwenye shina la mashetani ya Kibuki, yatatupeleka mpaka kwa wakuu wa Kabuki huko Japan.Next episode pls
Unampaka mara 1?,ama kama dozi flani hivi kwa siku labda kabla hajalala na pakikucha,kuna kunuia wakati wa hilo zoezi?Mpake dizeli tu.
Simba.
Akipandisha tu. majini ya kishetani na mapepo yanatoka mbio. Kama hajapandisha usimpake.Unampaka mara 1?,ama kama dozi flani hivi kwa siku labda kabla hajalala na pakikucha,kuna kunuia wakati wa hilo zoezi?
Ile kuchukua dizeli na kutaka kumpaka ni nia tosha kabisa, hakuna cha kunuia wala kusema. Kama unajua Qur'an unasema dua hii "Bismillahil-ladhi la yadurru ma'as-mihi shai'un fil-ardhi wa la fis-sama'i, wa Huwas-Sami'ul-'Alim".Unampaka mara 1?,ama kama dozi flani hivi kwa siku labda kabla hajalala na pakikucha,kuna kunuia wakati wa hilo zoezi?
Usipunguze, acha kabisa.Unaweza pia kupunguza, ‘mungu akipenda’ una acha kabisa. Muhimu ni kubadili mtindo wa maisha.
Nimeliona hilo, napitia posts za nyuma na kufanya editing.Kaka unachapia sana.
Sheikh Mittoga, ndugu yangu kwa damu. Kwanini tufikie kwenye uadui? Tusifike kufikiriana hayo, ni roho ya kishetani hio. Mlaani shetani.Hakuna cha ukiboko wala nini, mimi napenda kumsoma adui pia ili kujua nyendo zake na namna ya kumkabili.
Yaani napitia posts mpaka nacheka peke yangu. We bi FF ni mtata sana.Simba, asikusumbuwe huyo, kaishiwa bando tu. Arsis naye kasema nini kuhusu huyo poyoyo, funguka.
Ifrit au shetani au jini au yupo kwa kazi na makusudio maalum ya Allah, ni kiumbe chake.Kuna mtu aliuliza juu ya maana ya haya maneno ninayoelezea kwa mujibu wa quran nadhani ni FaizaFoxy naendelea nilipo ishia.
AFRIT au IFRIT - ni aina ya majini.
Katika maelezo ya Qur'ani na Hadithi, 'Ifrit ni majini wenye nguvu Wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa na mara nyingi wanahusishwa na uovu na uasi. wametajwa katika quran surat Naml aya ya 39
قَالَ عِفْرِيتٌۭ مِّنَ ٱلْجِنِّ أَنَا۠ ءَاتِيكَ بِهِۦ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّى عَلَيْهِ لَقَوِىٌّ أَمِينٌۭ
Tafsir : Akasema Ifrit Mimi nitakuletea kiti chake kabla hujainuka kutoka mahali pako, na mimi nina nguvu juu yake na ni muaminifu.’"
Katika aya hii, Nabii suleyman (a.s) aliwauliza baraza lake na tunajua nabii sulyman alipewa utawala kwa wanadamu na majini na wanyama hivyo aliuliza nani anaweza kwenda kuniletea kiti cha malkia wa sheba aliyeitwa balqis ndiyo huyu ifrit akamjibu mimi naweza kuleta kabla hujanyuka kutoka kwenye kiti chako.
Pia katika kisa maarufu cha Isra na miraj Bwana mtume Muhammad (S.a.w) wakati wapo na jibril mtume aliona kiumbe kuna wafuata mtume akamuuliza jibril ni kiumbe gani hicho ndipo jibril akamwambie mtume huyo ni Ifrit minal jinn nikufundishe maneno ambayo ukiyasema ataacha kutufatilia, Jibril a.s akamwambia sema.
بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Bismillahi alladhi la yadurru ma'asmihi shay'un fil ardhi wa la fis-sama'i,Wahuwas-sami'ul-alim":
Tafsir: Kwa jina la Allah, ambaye hakuna kinachodhuru, iwe kwenye ardhi au angani, naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua."
Baada ya mtume kusema maneno haya jinn huyu akaacha kuwafatilia hii ni dua ya muhimu na inasisitizwa waislamu kuisoma katika adhkari za asubuh na jioni.
Kwa ujumla, Ifrit ni Majini wenye nguvu na waovu, lakini siyo wote wanakuwa na tabia mbaya. Kama majini wengine, wanaweza kuwa na tabia mbalimbali na uwezo wa kuchagua matendo yao.
MALAIKA - Kwa mujibu wa Qur'ani, malaika ni viumbe wa kiroho walioumbwa na Allah kwa nuru kwa ajili ya kutekeleza amri zake na kusimamia masuala mbalimbali ya ulimwengu. Malaika wana sifa maalum ambazo zinawafanya kuwa viumbe wa kiroho tofauti na wanadamu na majini.
Sifa za malaika
Wapo wengi sana ila kubwa zaidi kwao hawamuasi Allah wanatekeleza wanaloamrishwa tu wametajwa sana katika quran na hadithi kuna Jibril, Mikael, Israfil, Munkar, Nakir n.k na wanamajukumu tofauti tofauti na wapo wengine wao wanafanya ibada tu na kumtukuza Allah.
- Viumbe wa Kiroho : Malaika ni viumbe wa kiroho
- Wanawajibika kwa Amri za Allah : Malaika hutekeleza amri za Allah na wanapokea maagizo kutoka kwake. Hawana uhuru wa kuchagua kama wanadamu; wao huishi na kutekeleza amri ya Allah kwa utii kamili.Sura ya 16 aya 49-50.
- Wanaweza Kujidhihirisha : Malaika wanaweza kujidhihirisha kwa watu kwa umbo maalum au kwa njia ya kiroho.
Nakusoma vizuri sana,Akipandisha tu. majini ya kishetani na mapepo yanatoka mbio. Kama hajapandisha usimpake.
Elewa kua majini ambayo sio ya kishetani hayapandi kichwani kwa mtu, kabisa. Akija jini au pepo hata akijifanya mwema vipi lakini kapanda kichwani kwa mtu elewa kua huyo ni muongo tu, ni shetani.
Kila Mwenyezi mungu anapotujaalia kuendelea na hivi vionjo vya Arsis, tutaelewa kidogo kidogo tofauti za shetani na jini. Ni nyembamba sana kama unene wa unywele mmoja.
Simba.
Qur'an ipo wazi kwenye hilo;Nakusoma vizuri sana,
Swali lingine,nna kitu nimeweza kukigundua kwa muda mrefu sasa,nikipanga jambo kwa umakini sana na lenye tija napofikia kulianza tuu either linaharibika,au haliendi kwenye mafanikio,au linakufa kabisa,ama litaenda tararibu sana kwa case ya vitu vya maendeleo(kutoka mwezi/miezi mpaka miaka),hata upande wa kauli tuu pia nna hio kasumba.
Samahani, ndio kwanza nauona ujumbe wako.Simba naomba tuletee episode ya kulalia.
Ni mtu ambae alikosa ustahamilivu kabisa, haijui hata heri yake iko wapi.Dereva njaa kali
Si mwenyewe nishawahi kumsoma anakiri hilo. Au nimechanganya jamani?FaizaFoxy ni jini...?!
Simba, ninakusoma na ninakusoma tena...
Mambo ya 'Chapter/Chapters'....
Huu ukumbi ni wako; sema kila unachoandika 'kinapimika' ama/na 'kutathminika'--kwa kheri lakini.
Siyo kwamba hauna unayoyakosea ama vipi--ila unayo liberti ya kushiriki kusudi lako; ni vema hili kusudi lifanywe safi, safi tena safi iwezekanavyo...
Wakati mmoja, yote ambayo umewasilisha humu lakini 'hayajafanyika bora' yanaweza kuja kuboreshwa na wewe mwenyewe kwa 'msaada utakaopata isivyo moja kwa moja'...
'Moyo Mkunjufu' ni silaha ya ulinzi katika 'Rehema na Fadhili'...
Hmmm
Nani asiyekuwa jinni hapa JF?Si mwenyewe nishawahi kumsoma anakiri hilo. Au nimechanganya jamani?
Simba.
Kubwa sanaNi mtu ambae alikosa ustahamilivu kabisa, haijui hata heri yake iko wapi.
Tuna somo kubwa sana la kujifunza hapo.
Simba.
sasa mkuu hio dizeli unamaanisha mafuta ya gari anunue mapya kabisa sheli au aliyotumika atoe kidogo kwenye gari na hiyo dizeli anampakaje je,kichwani tu,usoni au mwili mzima.? na kama aliyepandisha ni mwanamke baadhi wana misitu ya nywele kichwani inakuwaje.?Akipandisha tu. majini ya kishetani na mapepo yanatoka mbio. Kama hajapandisha usimpake.
Elewa kua majini ambayo sio ya kishetani hayapandi kichwani kwa mtu, kabisa. Akija jini au pepo hata akijifanya mwema vipi lakini kapanda kichwani kwa mtu elewa kua huyo ni muongo tu, ni shetani.
Kila Mwenyezi mungu anapotujaalia kuendelea na hivi vionjo vya Arsis, tutaelewa kidogo kidogo tofauti za shetani na jini. Ni nyembamba sana kama unene wa unywele mmoja.
Simba.
Jini kwa muktadha upi...?!Nani asiyekuwa jinni hapa JF?