Ndugai hajui idadi ya watoto wake Ndugai alitwambia kwamba Yesu na mke wake walikosa chumba Capernaum .Ana tofauti gani na Mpwayungu?mpwayungu village hawezi kua ndughai.
Ndughai Ni mtu na heshima zake na pesa zake.
Huyu mpwayungu anajua madanguro yote Dar na Dodoma na Bei pia anajua.
Mpwayungu hajawahi kua na mwanamke mwenye heshima zake, yeye Ni haya ma lapulapu mitumba kwisha kazi Kama utumbo wa Bata.
Hapo umedandia mtumbwi wa vibwengo🤣Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 16.
Shemeji yangu kiukweli alikuwa na pesa isiyokuwa ya kawaida,hakuwa tajiri sana kiasi ambacho kingemuingiza miongoni mwa matajiri wa pale Mwanza, lakini alikuwa na uwezo na utajiri wa size ya kati!,nyumba aliyokuwa anakaa yeye na mkewe(dada Sarah)ilikuwa ya kwake ambayo aliijenga kwa fedha yake mwenyewe,pia alikuwa akimiliki gari aina ya Nissan Patrol Nyeusi.
Pia alikuwa ni mtu fulani aliyekuwa na viprinsipo vyake ambavyo kama ulikuwa hujamuelewa ungeona kama ni mateso kuishi nae,pesa yake mpaka ifikie hatua umeila basi ilikupasa umenyeke sana na jasho likutoke sana!.Hivyo hata wakati ananipeleka pale mwaloni na kumwambia yule bwana kwamba ningekuwa miongoni mwa wavuvi,nilikuja kumuelewa baadae maana mwanzo nilidhani kama alikuwa akinishushia heshima na kunidharau!.
Kwakuwa tulifika hapo Ijinga mida ya saa 10 jioni,yeye bwana shemeji baada ya kuwapa maelekezo wale jamaa na kuwaachia alicho waachia,aliondoka akatuacha.Sasa nilipouliza jamaa ameenda wapi yule jamaa aliyenipokea akadai anaelekea kwenye miradi yake mingine ambayo hata sikuifahamu!.
Wakati nimefika hapo sikufahamu kumbe kuna eneo jamaa walikuwa wakiendelea na mapishi bhana,sasa jamaa niliyekabidhiwa kwake kama kama mvuvi alinichukua akanitaka tusogee pembeni kidogo ambako kulikuwa na kibanda cha mabanzi na nyasi,nilipofika hapo nikakuta kundi la watu 7 wakiwa na miili iliyokuwa imejengeka vizuri kimisuli!,jamaa walikuwa wamevaa bukta tu huku vifua vikiwa wazi.Mimi pamoja na kakitambi kangu kalikokuwa kameanza kuchomoza kwa ajili ya beer na fedha haramu,nilijiona kwa wale jamaa siyo kitu kabisa kwa namna walivyokuwa wamejazia misuli!.Jamaa mmoja wapo kwenye wale watu nilisikia anamwambia yule jamaa niliyekuwa nae ya kwamba "Waukae angalia usije ukalala njaa!".
Kumbe yule jamaa niliyekuwa nae hilo ndilo lilikuwa jina lake,sasa sikuelewa kama ndilo alilopewa na wazazi wake au lilikuwa jina tu alilopewa na wale jamaa!.
Waukae "Aisee kazi mpya hii!"
Jamaa 1 "Ooh karibu mwanangu,huku ndiko nyumbani kwetu!"
Jamaa 2 "Town tulishakusahau,makazi yetu ni pamoja na samaki mwanangu!"
Wakati huo walikuwa wamekaa wamezunguka sufuria kubwa lililokuwa limefunikwa kwenye sinia kichwa chini miguu juu!,kuna jamaa mmoja alinyanyuka akaelekea ndani kwenye kile kinyumba akatoka na samaki 3 wakubwa ambao walikuwa kambale,samaki wale walikuwa wa kuchoma!,kumbe wao walishindwa kula muda ule walikuwa wakipiga stori wakimsubiri huyo Waukae.Jumla yetu pale ikafanya tukawa watu 9.
Tukauzunguka ule ugali lile sufuria likafuniliwa,aisee sikuwahi kushuhudia ugali wenye ukubwa ule toka nizaliwe,hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuona ugali uliokuwa mkubwa kwa kiwango kile,wale samaki wakaweka chini kwenye mfuko na kazi ya kuanza kufukuzana na matonge ikaanza rasmi!,mimi nilikula sana samaki kwakuwa nilikuwa nina hamu nao sana maana wakati nikiwa Sirari chakula changu kikubwa ilikuwa nyama na kichuri!.
Baada ya kushiba nilijisogeza kando nikawaacha jamaa wakiendeleza libeneke!.
Jamaa 1 "Mwanangu mbona unakimbia"
Mimi "Mwanangu niko fiti!"
Jamaa 2 "Huyu hana njaa muda bado!"
Ile kauli ya yule jamaa wa pili sikuielewa kwa wakati ule lakini kwa baadae ilikuwa na maana kubwa sana kwangu!.Niliondoka nikaelekea ziwani kwenda kunawa mikono!..
Walipomaliza kula ugali ambao haukubaki hata punje,ndipo kila mtu alinyanyuka na kuendelea na mambo yake,mimi niliendelea kushangaa kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ziwani kabisa na kusogelea maji ya ziwani,mara zote nimekuwa nikiliangalia lile Ziwa Victoria kwa mbali tu na sikuwahi kabisa kulisogelea kwa karibu hadi kuyagusa maji yake!.
Ilipofika mida ya saa 12 jioni niliona wale jamaa wakianza kubeba nyavu pamoja na makarabai na kupelekea kwenye ile mitumbwi,zoezi lile lilifanyika kwa haraka na ndipo wengine wakawa wanavaa masweta na nguo za kazi,kuna jamaa wengine wao walibaki kama walivyokuwa tu hapo awali!. Baada ya muda giza nalo likaanza kutanda,ndipo Waukae akawa ameniambia nivue suruali nibaki na bukta pamoja na tisheti kisha nizame kwenye mtumbwi!.
Sasa kumbe ile mitumbwi mingine niliyoiona ilikuwa ya watu wengine,wale jamaa tuliokuwa nao tunakula,waliokuwa wafanyakazi wa shemeji walikuwa 4,hivyo ukiniweka mimi pamoja na Waukae tulikuwa jumla 6,wale wengine walikuwa wa mitumbwi mingine!.
Tuligawana watu watatu kwa kila mtumbwi na kisha ikawashwa tukaondoka!.Hakuna siku ambayo sitokuja kuisahau kama hiyo maana ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kupanda mtumbwi pia ilikuwa siku ya kwanza kusafiri ziwani,muda huo kiukweli ziwa lilikuwa limetulia sana na hakukuwa na mawimbi.Baada ya mwendo mrefu kuelekea katikati ya ziwa Victoria,nilikuwa nikigeuka nyuma naziona taa za pale kijijini mwaloni kwa mbali sana,pia kwa umbali ule ilifanya tukawa tunaona mianga ya taa kutoka vijiji vingine vilivyokuwa kando ya ziwa!.
Baada ya kufika walipoona panawafaa kushusha nyavu,zile boti zikawa zimezimwa na kulikuwa na utulivu wa hali ya juu,mawazo yangu yalikuwa yanakwenda mbali zaidi na kujikuta nawaza endapo tukizama itakuwaje,lakini kwa upande wa wale jamaa wao hawakuwa na hofu kabisa!.
Zile nyavu zikaanza kushushwa taratibu kutoka kwenye ile boti yetu,nyavu zilipokwisha kushushwa zote,ndipo nilimuona Waukae anachukua kopo moja kubwa la Toss(ambalo lilikwisha sabuni) lilikuwa na maji ndani yake akalifungua kisha akawa anachota yale maji kwa mkono kisha anayatupa ziwani huku akinuia jambo fulani!,sasa kwakuwa nilikuwa mtu mzima niligundua ya kwamba ile ilikuwa ni dawa na alichokuwa kuwa anafanya ni kama vile walipewa masharti na mganga,lile jambo lilikuwa likifanyika siku zote ambazo nilikuwa hapo Mwaloni na ilikuwa ni lazima lifanyike!.Na hata ule mtumbwi mwingine pia lilifanyika jambo hilo!.
Baada ya hapo tulitulia humo ndani ya mitumbwi hadi mida ya saa 10,sasa mimi nilifahamu ya kwamba tukishatupa zile nyavu tungerudi mwaloni hadi kesho yake ndipo kazi ifanyike kumbe haikuwa hivyo!.Ilipofika mida saa 10 ndipo tukaanza kuvuta zile nyavu!,nilichokuja kugundua ni kwamba,wale jamaa hawakujazia ile miili yao misuli kwasababu ya kunyanyua nondo(vyuma vya Gym)bali walijaza kwasababu ya kuvuta zile nyavu!,aisee asikwambie mtu,ingawa kulikuwa kuna baridi na hali ya hewa isiyokuwa ya joto lakini mimi nilichuruzika jasho kama nilikuwa nakimbizwa!.
Mahala popote ukiwa unawaona wavuvi nakuomba wapigie saluti,ile kazi haikuwa ya kitoto kama watu wazaniavyo!.
Basi baada ya kuvuta zile nyavu kwa muda,ndipo na samaki nao waliokuwa wamenaswa na zile nyavu wakaanza kujitikisa na kurukaruka!,kwa upande wangu niliendelea kushangaa sana kwasababu ilikuwa ni kitu kipya!.Hiyo siku tulipata samaki wengi sana na kitu ambacho niliendelea kukishangaa sana ni kitendo cha kumvua samaki aina ya Sangara mwenye ukubwa na kimo kama cha mtoto wa miaka 6.Niliuliza nikaambiwa huyo ni cha mtoto,kuna siku huvuliwa Sangara mwenye kimo cha mtu mzima ingawaje huwa ni mara chache lakini hutokeaga!.
Ilipofika mida ya saa 12 asubuhi baada ya kuifanya ile kazi kwa muda mrefu,mashine ziliwashwa na kurudi mwaloni huku tukiwa na rundo la samaki wakubwa na wadogo!.Tulipofika Mwaloni tulikuta kulikuwa na gari kubwa ambalo lilikuwa rasmi kwa ajili ya kubeba na kuhifadhi samaki!.Haukupita muda nikawa nimemuona na shemeji pia!.
Tuliwashusha wale samaki kwenye chombo kisha wakawa wanapimwa uzito,waliokuwa wakubwa wa size iliyotakiwa waliipakiwa kwenye ile gari,na waliobaki waliwekwa kwenye madumu kisha kuna land-rover lilikuja kuwachukua!.
Baada ya kuifanya ile kazi kwa muda wa mwezi mmoja nikaanza kuizoea,sasa kuna siku nikawa napiga mastori na Waukae ambaye tayari alishakuwa mtu wangu wa karibu sana!.Wao ilipofika mwisho wa Mwezi walikuwa wakilipwa kwa makubaliano walioyafahamu wao,lakini sikulipwa chochote,sasa nikafahamu uenda shemeji atakuwa hela yangu anampatia Dada yangu,uenda alidhani kwa pale kijijini ningeitumia vibaya,kilichokuwa kinanisaidia ilikuwa ni ile hela yangu ambayo bado nilikuwa nayo.
Waukae "Unadhani bila vile utapata samaki!?"
Aliendelea "Utarudi na mitumbwi ikiwa inakukodolea macho!"
Mimi "Kwahiyo ni kila mtu mwenye mtumbwi anafanya?"
Waukae "Ni ujanja wako tu,wapo ambao wanamtegemea Mungu lakini huwa hawasaidii wanaishia kupata hasara na kuuza injini!"
Mimi "Kwani Injini inauzwaje!"
Waukae "Injini ipi sasa,maana kuna hiyo Yamaha na Honda!"
Mimi "Kwani zinatofautiana bei!?"
Waukae "Hiyo Yamaha ina bei yake na Honda pia ina bei yake"
Mimi "Nzuri ni ipi kaka?"
Waukae "Yamaha ina sipidi ila Honda ina nguvu na hata bei yake imesimama"
Ile mitumbwi ya shemeji yeye alikuwa amefunga injini za Honda,lakini mitumbwi karibia mingi ilikuwa na injini za Yamaha!.
Waukae "Yaani hapa bila dawa unadhani unatoboa!"
Aliendelea "Hivi Masangara ni shemeji yako kabisa eti!"
Mimi "Masangara ndiyo nani?"
Baada ya kuuliza Masangara ndiyo nani yule jamaa akaanza kucheka sana kana!.
Waukae "Sisi tunamjua kwa jina la Masangara"
Mimi "Ni shemeji yangu ila hilo jina sikuwahi kulifahamu"
Waukae "Huku watu wanamjua kwa jina hilo"
Waukae alikuwa ni msukuma bila hata kuuliza kwasababu ongea yake na rafudhi yake vilitosha kukuaminisha pasipo shaka!.
Baada tena ya kupiga kazi kwa mwezi mmoja uliofuata wenzangu wakalipwa hela nzuri tu lakini kwangu ikawa hola!.Sikuelewa sababu za shemeji kutokunilipa ilikuwa ni nini wakati nilikuwa nafanya kazi sawa na akina waukae!.Niliamua kuweka vocha kwenye kiswanswadu changu na kumpigia Dada Sarah na kujifanya namsalimia ili nione uenda angeniambia shemeji huwa anamuachia hela yangu!,baada ya mazungumzo nikaona yuko kimya sikutaka kumuuliza maana niliona nikimuuliza na akajua kumbe mumewe anipatii chochote kitu ningewachonganisha,hivyo nikaamua kukaa kimya!.
Ndani ya mwezi huo nilipokuwa nimejifunza na kuielewa ile kazi na namna ilivyokuwa inapesa ndefu,niliamua kumpigia simu Mwanangu Mtatiro.
Mpwayungu ni Umughakampwayungu village hawezi kua ndughai.
Ndughai Ni mtu na heshima zake na pesa zake.
Huyu mpwayungu anajua madanguro yote Dar na Dodoma na Bei pia anajua.
Mpwayungu hajawahi kua na mwanamke mwenye heshima zake, yeye Ni haya ma lapulapu mitumba kwisha kazi Kama utumbo wa Bata.
Wakati mwingine huwa wanajua kabisa unapotezewa muda na ndugu yao.lakini wanavyokuchangamkia kiunafiki wakikuona..Mashemeji sio watu wa kuwaamini hata kidogo
mpwayungu village hawezi kua UMUGHAKA. Mpwayungu akiona demu Ni muda huo huo anataka, Hana simile ndio maana mabibi zake Ni ma barmaid, mama ntilie na wahaya wa Mwananyamala. Umughaka Ni MTU mwenye subira, kwanza anampima demu, akiridhika ndio anauza lugha.Mpwayungu ni Umughaka
Inategemea ushemeji wenyewe. Yaani mjanja Nani nikimaanisha Nani kamuolea mwenzake.Mashemeji sio watu wa kuwaamini hata kidogo
Mkuu Hoaxer umefanya nicheke kwa sauti kubwa kama mwehu!mpwayungu village hawezi kua UMUGHAKA. Mpwayungu akiona demu Ni muda huo huo anataka, Hana simile ndio maana mabibi zake Ni ma barmaid, mama ntilie na wahaya wa Mwananyamala. Umughaka Ni MTU mwenye subira, kwanza anampima demu, akiridhika ndio anauza lugha.
Umughaka hanunui ngono wakati mpwayungu Hadi umri huu hajawahi kua na girl friend.
Yeye Ni Meeda, Kona bar, Mikasa, Kimboka na Sewa (sewage bar Buguruni)
Umughaka amesema pesa yake nyingi inaishia kwenye pombe na pamba,natamani sana life style ya hiv lakin kuiweza ni mtihani maana kuwaepuka chuma ulete hawa wasasa ni ngumu mno,siku hz wanakaa hata uchi ili uone upagawe,sijui Umughaka anawezaje kuwakwepampwayungu village hawezi kua UMUGHAKA. Mpwayungu akiona demu Ni muda huo huo anataka, Hana simile ndio maana mabibi zake Ni ma barmaid, mama ntilie na wahaya wa Mwananyamala. Umughaka Ni MTU mwenye subira, kwanza anampima demu, akiridhika ndio anauza lugha.
Umughaka hanunui ngono wakati mpwayungu Hadi umri huu hajawahi kua na girl friend.
Yeye Ni Meeda, Kona bar, Mikasa, Kimboka na Sewa (sewage bar Buguruni)
alisema Ni misosi na pamba sio pombe mkuuUmughaka amesema pesa yake nyingi inaishia kwenye pombe na pamba,natamani sana life style ya hiv lakin kuiweza ni mtihani maana kuwaepuka chuma ulete hawa wasasa ni ngumu mno,siku hz wanakaa hata uchi ili uone upagawe,sijui Umughaka anawezaje kuwakwepa
aroooo! ukifika kuree ure ugari na rijisato ra rewo rewo mweee! utamu mpaka machoni!...rire rikuu ra mukowa rimeamua kujenga hukooo kabisaaBinafsi Kwenye fikra zangu hua nahisi Mara/Musoma ni mapori tu na vijiji hakuna mjini.
Siku moja Inabidi nifike huko mura
Jamaa alifukuzwa sheleni night kali kwakuwa alimtaka binti wa ticha 😅😅😅😅😅mpwayungu village hawezi kua UMUGHAKA. Mpwayungu akiona demu Ni muda huo huo anataka, Hana simile ndio maana mabibi zake Ni ma barmaid, mama ntilie na wahaya wa Mwananyamala. Umughaka Ni MTU mwenye subira, kwanza anampima demu, akiridhika ndio anauza lugha.
Umughaka hanunui ngono wakati mpwayungu Hadi umri huu hajawahi kua na girl friend.
Yeye Ni Meeda, Kona bar, Mikasa, Kimboka na Sewa (sewage bar Buguruni)
Kuwa na subira mbona episode ni ndefu tu 😂😂😂Bora niache kusoma mpaka umalize tu..
Arosto