Niko addicted na Mlima Kilimanjaro! I love this Mountain...

huwa Napata shida sana kutoka Stella hadi Barafu aisee...
Kushuka ni raha zile amsha amsha za maguide mnajikuta mnaseleleka tu, mie kutoka Stella hadi barafu nilishuka kwa msaada wa watu wa mlima Kilimanjaro
 
Safi sana Mkuu!!
Big up...
 
Safi sana, 1989 nilipanda mlima kama mzalendo halisi. Ila shida niliyopata mpaka kileleni sitarudia tena, naacha kama mtoto anavyoacha kunyonya. Nashukuru nilirudi salama
 
Safi sana bro! Unatutia hamasa nasi ya kuufurahia uumbaji wa Mwenyezi Mungu
 
Hzo njia za Marangu na Rongai ni rahisi mno ni za viongoz na wamama.kidume pita machame, Lemosho, londrosi, au Umbwe, na kwa mbeba mizigo (mgumu)anatambaa na kg25 begani.
Kweli mkuu tulikuwa tunapishana na Wazee wa kizungu tu

Ila niliipenda sana Ile njia
Nitarud Tena nikiwa na muda mwezi wa kwanza nafkiri ndo best season
 
Umechangia pato la taifa,kwa miaka kumi tunaona namna huu mlima ulivyotuingizia mapato
Mapato mengi sana...
Mkuu mlima Kilimanjaro unaingiza Pesa nyingi sana Kuliko kivutio chochote ndani ya nchi yetu
 
Ulifika kileleni mkuu? Hebu waambie wanajukwaa ladha ya huu mlima, binafsi nimeukwea kama mara nne hivi...Two Times Marangu Route...
Mara moja Machame na Mara moja Londorosi...

Mkuu hongera sana. Mimi nashiriki Killy Marathon (21km) toka 2007, ila mlima sijawahi kupanda.

Umenihamasisha sana mkuu. Mungu akijalia mwaka huu lazima niukwee.

Karibu na wewe Killy Marathon mkuu.
 
Mkuu hongera sana. Mimi nashiriki Killy Marathon (21km) toka 2007, ila mlima sijawahi kupanda.

Umenihamasisha sana mkuu. Mungu akijalia mwaka huu lazima niukwee.

Karibu na wewe Killy Marathon mkuu.
Nilishiriki ya KIA marathon mkuu
 
Nilishapanda mlima mara mbili na kufanikiwa kufika peak kwa kupitia Marangu route, real ni big adventure lakini inahitaji ujasiri na uvumilivu mkubwa sana kupanda huo mlima.

Ni issue kufika Uhuru Peak. Kama ndiyo mara ya kwanza hakuna rangi ambayo utaacha kuiona. Lakini kuna kitu cha ajabu nilichojifunza kule nacho ni nguvu gani wanayotumia wale mapota??? Ni nguvu peke yake au kuna ziada???
 
Nilishiriki ya KIA marathon mkuu

Hongera sana mkuu; ila Kilimanjaro Marathon ndiyo kongwe, na ni well organised kuliko Kia. Mwaka uliopita nadhani washiriki walikuwa zaidi ya 10, 000.

Jaribu kushiriki hii, utaona tofauti kubwa sana na Kia Marathon.
 
Ndani ya miaka 2 naplan kupanda hebu nipe hints miezi ipi ni kizuri nikipanda nitakuta barafu nyingi?
Issue kubwa ni kufanya mazoezi sana kabla hujaenda ili kujenga stamina na kuwa mvumilivu kwa kiwango cha juu ili uweze kufika peak.

Kama utatumia Marangu route kwa siku tano inabidi ujipange sana.

1. Siku ya kwanza unatoka Marangu - Mandara 8kms

2. Siku ya pili from Mandara - Horombo 12kms

3. Siku ya tatu ndiyo kiyama kwa mpandaji mlima huo.

Unatoka Horombo to Kibo 9kms. Unatakiwa ufike mapema ili upumzike na uanze maandalizi ya kusummit yaani kwenda kileleni ambapo ni 6kms from Kibo.

Mazingira ya Kibo ni magumu kwa maana ya baridi kali na upepo.

Ukiwa na akili za kusummit 6kms unasahau kwamba kuna kurudi. Unaweza kujitahidi ukafika peak issue inakuwa kurudi. Hivyo 12 + 6 + 6 za kurudi = 24kms hapo unakuwa tena na kibarua cha kurudi Horombo kama utatumia siku 5 ambapo 24 + 12 ni 36kms hizo unazitembea ndani ya siku mbili ambazo kutokana na ratiba ni kama siku moja tu.

Anyway kupanda mlima ni issue, nisiongee mengi ila nendeni mkajionee maajabu ya uumbaji wa Mungu
 
Tusisahau Mapota(wagumu hawaendi peak)
 
Hongera sana mkuu; ila Kilimanjaro Marathon ndiyo kongwe, na ni well organised kuliko Kia. Mwaka uliopita nadhani washiriki walikuwa zaidi ya 10, 000.

Jaribu kushiriki hii, utaona tofauti kubwa sana na Kia Marathon.
Asante sana Mkuu...Mwaka huu inaanza lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…