SoC02 Ni wakati sasa wa kumaliza vita hii ya vijana dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Jul 25, 2022
221
197
VITA YA VIJANA DHIDI YA MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

Chemsha bongo!
Je! Umewahi kujiuliza kuwa licha ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kusaidia katika kuboresha maisha ya binadamu kiujumla lakini bado yameacha malumbano makubwa dhidi ya vijana mbalimbali?
Ukweli ni kwamba vijana wengi hususani wanaotaraji kuajiriwa, walioajiriwa na hata ambao wamejiajiri wamezua vita baridi dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia katika sekta mbalimbali wakiamini kuwa ukuaji huo umekwenda kuchukua nafasi zao walizokuwa wakitaraji kuzitumikia.

Je! Ni kweli kuwa kitafika kipindi ambacho kutakuwa na mapinduzi makubwa ya kisayansi na teknolojia ambayo yataondoa watu wote katika nyanja mbalimbali huku kazi zote zikiendeshwa na mashine zenye teknolojia ya hali ya juu?
Haya ni baadhi ya maswali yaliyoacha sintofahamu kwa baadhi ya vijana mbalimbali ambayo yanahitaji ufumbuzi ili kuwaweka huru na kujenga imani kwa vijana ili waweze kuona manufaa na uhitaji wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Hivi sasa mapinduzi ya sayansi na teknolojia yamefanikiwa kuathiri karibu kila sekta huku yakiwaacha nyuma watu wengi ambao baadhi yao hugeuka na kutupa lawama zao katika mapinduzi hayo ya sayansi na teknolojia pasipo kujali manufaa tele yaliyoletwa kwao.

Je, ni kweli kuwa mapinduzi ya sayansi na teknojia yamesababisha wimbi kubwa la vijana wasio na ajira mtaani?
Ukweli ni kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia yametia chachu katika ukuaji wa maendeleo nchini hususani katika maboresho ya utoaji wa huduma mbalimbali ambapo imechangia pia kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa ajira mbalimbali. Lakini pia mapinduzi hayo yameongeza wimbi kubwa la upotevu wa baadhi ya ajira za vijana katika sekta mbalimbali. Lakini ni dhahiri kuwa bado maendeleo hayo yameleta matokeo chanya zaidi kuliko athari hasi.

Tazama picha zifuatazo kwa umakini kisha ung’amue dhamira kuhusiana na athari ya maendeleo ya sayansi na teknolojia katika jamii.
IMG_202208216_134727533.jpeg

Picha ikiwaonesha matabibu wakitoa huduma kwa mgonjwa.
(Melnick Medical Museum)

Tazama pia picha ifuatayo kisha jaribu kuhusianisha na picha iliyoainishwa hapo juu.
IMG_202208216_012453731.jpeg
Picha ikimuonesha mtoa huduma ya afya akiwa na mgonjwa. (Picha yangu, Chuo cha Afya, Muhimbili)
Je! umegundua nini kutoka kwenye picha hapo juu?
Dhahiri utagundua kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yameweza kuboresha urahisi wa utoaji huduma yenye ubora wenye kiwango cha hali ya juu lakini ikiambatana na upunguzaji wa uhitaji wa watoa huduma katika sekta mbalimbali kama ilivyooneshwa katika picha. (matabibu watano hadi tabibu mmoja kwa mgonjwa).

Mapinduzi ya sayansi na teknolojia yameweka wimbi kubwa la maswali hususani kwa vijana ambao wameweka imani na matumaini yao juu ya kuajiriwa katika sekta mbalimabali. Mfano mzuri huonekana hata katika baadhi ya makampuni yaliyokuwa yakiajiri watu wengi kupunguza idadi ya waajiriwa kwa kiwango fulani , kwasababu baadhi ya kazi zikionekana kurithiwa na nguvu kazi mashine badala ya nguvu kazi watu.

Je! umewahi kufikiria, jinsi kamera za ulinzi (kamera za CCTV) zilivyopunguza idadi ya walinzi katika taasisi au kampuni fulani? Mashine za kufanyia usafi zilivyopunguza idadi ya wafanyakazi katika sehemu husika?
Matumizi ya mitandao katika kupakua filamu mbalimbali yalivyo athiri soko la Mikanda ya filamu/video CD(Compact Disc).
Haya ni baadhi ya maeneo machache yaliyoacha sitonfahamu juu ya watu waliokuwa wakiyatumia kama chanzo kikuu cha mapato yao katika maisha yao ya kila siku.

Je, ni nani atakayeibuka mshindi katika vita hii?
Hadi sasa kumekuwa na vita baridi juu ya pande mbili zinazolumbana (watu wasio na ajira dhidi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia). Lakini, Kitu kikubwa tunachopaswa kufahamu ni kuwa kamwe mapinduzi yote haya yakiteknolojia bado yanahitaji uwepo wa nguvu kazi watu.

Pia tukumbuke kuwa mapinduzi yote haya ni matunda yanayozalishwa kutoka katika fikra zetu wenyewe, hivyo kwani hata wahenga walisema “usiogope kivuli chako kwakuwa kinyago ulichochonga mwenyewe hakiwezi kukutisha.”

Ukweli utabaki kuwa, mapinduzi ya sayansi na teknolojia hayana budi kutujia kwahiyo ni wakati wetu sahihi wa kuhakikisha tunakwenda sambamba na mabadiliko hayo ili tuweze kufaa na kubaki katika mifumo stahiki itakayo tuwezesha kufanya kazi katika mazingira hayo ya makuzi ya sayansi na teknolojia. Hivyo basi, ni wakati sahihi kwetu kutafakari njia thabiti zitakazotuwezesha kufikia tamati ya vita hii baridi baina ya sayansi/teknolojia dhidi ya vijana wenye kusaka ajira katika sekta mbalimbali.

Nini kifanyike kumaliza vita hii?
  • Ni wakati sasa kwetu kutambua na kushiriki fursa au matukio mbalimbali yahusuyo vumbuzi mbalimbali zenye kuleta tija na manufaa kwa jamii. Mfano katika sekta ya afya, uvumbuzi wa “mkanda salama” uliofanywa na wanafunzi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili, kama ilivyoainishwa katika picha hapa chini.​
image_search_1659552812640.jpg

Picha inayoonesha wanafunzi wa chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi wakielezea kuhusu uvumbuzi wa mkanda salama unavyoweza kuzuia tatizo la kutokwa na damu nyingi kwa wanawake wanaojifungua.(picha kutoka mtandaoni)


image_search_1659552998445.jpg

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Usafirishaji (NIT) wakionesha gari walilobuni jinsi linavyofanya kazi.teknolojia.(picha kutoka mtandaoni)
Haya ni baadhi ya maeneo machache yanayoonesha jitihada za vijana dhidi ya ukuaji wa teknolojia.

  • Pia, ni wakati sahihi kwetu kushiriki matamasha au makongamano mbalimbali yanayohusu uelimishaji dhidi ya mabadiliko na ukuaji wa sayansi na teknolojia. Mfano, katika sekta ya afya, kongamano la kisayansi lililofanyika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili tarehe 14-15/07/2022. Hii husaidia kuandaa fikra zetu dhidi ya mabadiliko mbalimbali yahusuyo mapinduzi ya sayansi na teknolojia, kwani ni heri kuitangulia teknolojia kuliko ikufike ukiwa hujaandaa fikra zako kuhusu mabadiliko hayo maana hata wahenga walisema “zimwi likujualo halikuli likakwisha”.​
  • Lakini pia, kitu muhimu zaidi ni kuruhusu au kufungua akili zetu kupokea mafunzo mbalimbali bila kujali kiwango chako cha elimu au aina ya elimu tuliyoipata. Mfano, unaweza kuwa umesomea masuala yahusuyo afya, elimu, sheria, kilimo n.k lakini pia ukajihusisha na mafunzo mbalimbali kuhusu tehama. Hii itasaidia kupata ujuzi mbalimbali utakaowezesha kuendesha baadhi ya shughuli za kiteknolojia katika sekta zetu husika, kama vile ufundishaji kwa kutumia kompyuta (tarakilishi) mfano vipindi kupitia mtandao (Zoom), matumizi ya nyenzo bora za kisasa katika kilimo, utumiaji wa mitandao katika biashara n.k. hivyo kumfanya mtu kufaa katika maeneo mbalimbali.​
  • Sambamba na yote kitu kikubwa zaidi ni kuwa kamwe hatuwezi kufikia tamati ya vita hii kama hatutakubaliana na hali halisi ya dunia ya sasa hivyo ni wakati sahihi sasa wa kukubaliana na ukweli uliopo, ni lazima tuendane na mabadiliko hayo kwani tusipo ambatana nayo ni dhahiri kuwa tutaachwa nyuma mwishowe tunaweza kuondolewa katika mifumo mbalimbali ambayo tumekuwa tukifikiria kila siku.​
Mwisho wa yote, japo si kwa ubaya tunaiomba pia serikali itambue vipaji mbalimbali vya vijana wenye uthubutu katika vumbuzi mbalimbali za kiteknolojia kwa kuwashika mikono ili kuwatia moyo kwa kutambua jitihada na uthubutu wao ili waweze kutimiza malengo yao. Mfano, kuwapatia mafunzo endelevu katika nchi zilizoendelea ili kuendana na mifumo halisi ya jinsi dunia inavyokwenda na mahala ilipofikia.
 
Andiko zuri lakini siyo kwa ubaya ningependa kufahamu labda nijue wewe kama kijana umegundua nini kwenye sayansi ?
 
Andiko zuri lakini siyo kwa ubaya ningependa kufahamu labda nijue wewe kama kijana umegundua nini kwenye sayansi ?
Asante kwa swali zuri Mr. Moris, aidha mpaka sasa nimefanikiwa kushirikiana na wanafunzi wenzangu katika uvumbuzi wa Artificial Intelligence AI kufny quick diagnosis (ugunduzi wa mapema wa saratani ya kizazi) inayoongozwa na Mr. Sang'udi Sang'udi kutoka chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Pia nimefanikiwa kuwasilisha mawazo pamoja na mapendekezo mbalimbali katika symposium zinazohusu maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kujifunza na kuongeza maarifa kama kijana.

IMG_20220703_151930_258.jpg
 
Asante kwa swali zuri Mr. Moris, aidha mpaka sasa nimefanikiwa kushirikiana na wanafunzi wenzangu katika uvumbuzi wa Artificial Intelligence AI kufny quick diagnosis (ugunduzi wa mapema wa saratani ya kizazi) inayoongozwa na Mr. Sang'udi Sang'udi kutoka chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

Pia nimefanikiwa kuwasilisha mawazo pamoja na mapendekezo mbalimbali katika symposium zinazohusu maendeleo ya sayansi na teknolojia ili kujifunza na kuongeza maarifa kama kijana.

View attachment 2317748
Hongera sana, hiyo saratani ya kizazi mmegundua au mmefundishwa darasani ?
 
Hongera sana, hiyo saratani ya kizazi mmegundua au mmefundishwa darasani ?
Kuhusu saratani ya kizazi tumefundishwa darasani lakini njia tulizofundishwa kufanya ugunduzi wake ni zile ambazo zimekuwa zikitumika katika hospitali zetu kama vile "Pap Smear" lkn hii Saratani AI ni application au program maalumu tuliyofanikiwa kubuni kwa kuingiza taarifa za mgonjwa then inatoa prediction ya Kuwepo au kutokuwepo kwa viashiria vya awali vya saratani. Hivyo mpaka sasa katika test kwa watu tuliowajaribu imeonekana kuleta matokeo mazuri hata hivyo test hii sio confirmatory.
 
Kuhusu saratani ya kizazi tumefundishwa darasani lakini njia tulizofundishwa kufanya ugunduzi wake ni zile ambazo zimekuwa zikitumika katika hospitali zetu kama vile "Pap Smear" lkn hii Saratani AI ni application au program maalumu tuliyofanikiwa kubuni kwa kuingiza taarifa za mgonjwa then inatoa prediction ya Kuwepo au kutokuwepo kwa viashiria vya awali vya saratani. Hivyo mpaka sasa katika test kwa watu tuliowajaribu imeonekana kuleta matokeo mazuri hata hivyo test hii sio confirmatory.
Nani mlimfanyia upasuaji ?
 
Nani mlimfanyia upasuaji ?
Labda niliweke sawa hili Mr. Moris......Hii haihusu kufanya upasuaji bali ni application kama zilivyo application nyingne lakini yenyewe ni special kwa ajili ya kugundua dalili za Saratani......hivyo haikuwahi kutumika kama njia ya kuchunguza Saratani hivyo ndio tumeanzisha kama njia mbadala wa njia zingine zilizokuwa zikitumika awali.
 
Karibuni, wanajamii Forum tuendeleze mjadala huu ili kumaliza vita hii.......
 
Back
Top Bottom