Pawaga
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 1,349
- 1,011
Mkuu twende taratibu....ni utoto tu kumbuka nlikuwa std 5 kipindi hicho.Sasa na wewe una mambo ya ajabu sana. Unaachaje nguo mtoni?mbona smetme unafanya mambo ya ajabu?unaachaje nguo mtoni then kesho yake unaenda beba hata hukagui?hayo mambo ya ajab sana....ungesababisha maafa na leo hii tusingesoma post yako. Umenikwaza sana.
Haya elezea vizur kuanzia mwanzo ilikuaje mpaka kufikia hapo.
Ok basi alivyotoka kweny zile nguo baada ya harufu ya m/taa akawa kakasirika balaa maana mafuta ni sumu kwao hivyo akajihami kwa kukimbilia uvungun mwa kitandan ( kama ujuavuvyo kijijini jiko,stoo,kuku,kitanda humu humu) hivyo ikawa shida kumuua. Anahamia hapa mnarukia huku ikawa mbilinge mpaka kama saa 7 hivi jamaa angu akakosea step-akachomwa mguuni na mwiba wa mkiani(huyu nyoka ana kamwiba kadooogo chini ya mkia kana sumu kali sana wanasema bora akugonge na jino kuliko mkia)
Hapo hapo tukaahirisha zoezi la kummua tukatafuta wazee wanaojua tiba. Sasa uzur pale kijijin kuna wataalam wa hizo tiba yaan ukitaja tu jina la nyoka aliekudhuru utaambiwa mzee fulan ndo mtaalam wa dawa za huyo nyoka,tukampeka jamaa kwa mzee husika (good luck mzee Hugo yupo mpaka leo pale kijijin nkienda mapumziko namkuta)
Mzee alimpa dawa lkn jamaa mpaka navyoandika hapa hakupona kwa 100% maana mguu wa kulia ulikuwa kama mfupi hivi yaana anatembea kwa kuchechemea toka 1995 lilivyotokea hilo tukio.
Tukaambiwa huyo nyoka bora akung'ate na mdomo kuliko akuchome na mwiba wa mkiani