Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 27,929
- 27,149
Ni muhimu sana kwa vijana na wazee kwa pamoja katika siasa, graduate na wasio graduates kua makini mno na kuepuka kukubali kirahisi kuhamasishwa na kubebwa ufala kifikra na viongozi wa kisiasa waliopoteza uelekeo nchini, na kutumbukizwa katika kutenda mambo au matendo haramu ambayo ni kinyume cha sheria, na hatimae kujikuta unamizwa au kupoteza maisha kilofa kabisa, na kupeleka huzuni nyumbani kwako na kusababisha utegemezi au umaskini wa kutupwa kwenye familia yako.
Usikubali kutumika kisiasa kama chambo au platform ya kisiasa kwa wanasiasa ambao wamekosa agenda, Lakini kabisa wamekosa maono. Ni fedheha msiba wako kufanywa jukwaa la kisiasa na majeraha au ulemavu wako kama mtaji wa kupata huruma kwa jamii ambayo haina faida yeyote kwako na kwa familia yao.
Tunza na kuitumia vyema zawadi ya uhai, afya na karama ya utashi na akili alizokujalia Mungu kutambua kwa haraka jema na ovu unalohamasishwa kutenda na muovu, na kuasess chapchap hasara na faida za kubebwa ufala, kwako binafsi na kwa familia yako.
Epuka kufanywa Lofa na vibaka wa kisiasa.๐
Mungu Ibariki Tanzania