Ni changamoto gani unayokutana nayo unapokutana na marafiki waliofanikiwa katika maisha?

Haha hahaha

nadhani na wewe mmoja wapo

ila unajua kinachoudhi sana unakuta mtu mlikuwa mnaongeaga sana sana kwenye simu. mara anapata kazi wala hakuambii chochote sijui anaogopa vibomu. sasa cha ajabu akishapata anakaa kimya na maongezi yanapungua kabisa.

tatizo tukishapata kazi tunajiona next level tunatafuta wa level za juu hawa wa chini tunawaacha hawana faida kabisa. lakini sishangai sana ndo waafrica tulivyo

husangai wengine wakipata kazi na nyumbani kwao wanapasahau kabisa na wala hataki apasikie kule kwenye misonge ya kwao
Rafiki yangu kuna kazi zengine zinastress mtu unachoka sio tu kiakili hata mwli unachoka, kama mimi kazi yangu inabidi nideal sana na watu ambao wanaudhi kiasi kwamba nikitoka kazini sitaki kabisa kudeal na mtu nataka nipumzike tu mpaka kesho kuanza kupambana tena kazini.
 
Rafiki yangu kuna kazi zengine zinastress mtu unachoka sio tu kiakili hata mwli unachoka, kama mimi kazi yangu inabidi nideal sana na watu ambao wanaudhi kiasi kwamba nikitoka kazini sitaki kabisa kudeal na mtu nataka nipumzike tu mpaka kesho kuanza kupambana tena kazini.

Kabla sijabadili taaluma maana mimi nilikuwa napenda u-injinia ila nikaangukia afya.

kilichonikuta nilikuwa nawahudumia wanawake. aisehhh usiombe kabisa tena ukute ni wa mama walioenda age kidogo hapo utakom.

wengine wanakuja wanaanza kukuelezea alipoamka, akafagia, akapika n.k n.k mpaka akuambie anaharisha duhh ushasikiliza ushudu wake wote non sense. mwingine kidogo nigombane naye, anakuuliza unajua naumwa nini? mwingine ukimweleza kula hivi, acha pombe maliza dozi hataki yaani bora nilikimbiaga kule
 
Always. Ukiona aliyefanikiwa usiogope. Be inspired. Tambua kwamba kumbe inawezekana. Kila mtu Mwenyezi Mungu alimpangia riziki yake. Kosa kubwa katika maisha ni kujilinganisha na mtu mwingine. Ndo kosa kubwa. Limegharimu wengi. Unaweza hata ukapata pressure au depression.

Mafanikio in dhana pana. Kila mtu amefanikiwa kwa njia tofauti.

Cha kufanya.....ukikutana naye jitambue uwezo wako. Be humble. Usijifanye much know. Onesha kiu ya kujifunza. Ulizia diferent opportunities ambazo zinakufaa na zinaendana na uwezo wako. Na usionyeshe any expectation ya msaada toka kwake. Sana sana omba contacts and promise to keep in touch. In baada ya kuwa na mawasiliano Mara mbili tatu unaweza kuanza kugusia Yale unayoona anaweza kukushauri. Kwa njia hii atakuheshimu hata Kama huna kitu.

Usiogope mafanikio ya mwenzako. Piga moyo konde and say even I can succeed. Say Amen.
Mkuu nimekuelewa sana hapo kwenye kujilinganisha na wengine, nahisi hata mimi ilianza kunicost ila nashukulu umenifumbua.
 
Kuna mwingine huyo tulikuwa vry close, mpk wengine wakawa wanasema tunapendana kma mapacha. Kuna wkt nilipata matatizo ofisin yaliyopelekea mimi kupelekwa police. Kuna ndugu yake mmoja, ambaye mimi nilifahamiana nae kwa kupitia yeye, akamuuliza, "ebana ishu ya mshkaji inaendeleaje? Akajibu "mi sijui anajua mwenyewe". Yule ndugu yke akasema lakn yule si mshkaji wako utasemaje hujui?? Alichokifanya akanitafuta kimyakimya kuniuliza kma tumegombana nikamwambia hapana. And its true sikuwahi kugombana na jamaa kwa lolote.

Baada ya mwaka kma mmoja nikiwa nimesafiri, nikapigiwa simu kwmb nyumbani kwangu nyumba ilikuwa inawaka moto. Nikawaza haraka haraka nani aliyepo jirani na kwangu na nina namba yake ya simu ninayeweza kumuomba anisaidie kwa sababu mimi nipo mbali na pale kuna watoto. Ikabidi nimpigie huyo jamaa. Kweli akaenda kwa sababu kutoka kwao mpk kwangu ni mwendo wa dakika kma 4 tu kwa miguu. Alipofika akanipigia na kuniambia jinsi watu wanavyookoa vitu, na kwmb familia yote ipo salama, kisha akakata simu. Alipokata nikampigia tena nikamuuliza kuna mabati yangu kma 130 yalikuwa store ndani, je yameungua au yameokolewa? Akanijibu "NGOJA NIRUDI NIANGALIE. NILIONDOKA KWENDA DUKANI KUNUNUA MAYAI". Daaah, nikapigwa na butwaa. Nikamuuliza yan mimi nyumba yng inaungua moto na mimi sipo, wewe unasema unaenda dukan kununua mayai..?? Nikakata simu. And believe me, machozi yalinitoka cz sikuamini nilichosikia kutoka kwa "best friend".

Nilichokifanya nikampigia fundi gereji mmoja aliyekuwa anatengeneza gari yng mara kwa mara, akaniambia yupo ofisini. Nikamwambia kama hutajali naomba uache unachokifanya uende kwangu kuna matatizo. Muda huo ilikuwa ni saa 11 jioni, yule fundi alienda pale akasimamia show nzima na kuhakikisha vitu vilivyookolewa vipo salama. Akatafuta gari familia na vitu vilivyookolewa ikapelekwa kwa ndugu yng. Akaondoka eneo la tukio saa 3 usiku.

Huyo "best friend" sikuwasiliana nae tena mpk leo, na ni zaidi ya mwaka sasa. Ila huwa tunapishana tu na hata niliporudi hakuja kuniona na nilirud kesho yake tu. Niliona bora nikae kimya.

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
Dah aiseeh kuna watu makauzu jamanii.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Daaah kumbe watu wanakwepaga na watu masnitch, nimecheka sana...duniani kuna mambo....
Yupo mmoja huwa kila akitaka kujipima maendeleo yako, anapiga simu mida ya saa mbili usiku kupima kama utakuja na gari au daladala, kali zaidi ukionana naye analeta stori za madili makubwa makubwa kukupima kama upo level hiyo au la...
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Wengi waliofanikiwa hawapendi kukeep intouch na watu wasiofanikiwa.Ni ngumu sana yatakuwa ni mawasiliano ya kujikomba sana.

Naamini..kama nina shida ndo mwenye jukumu la kumtafuta aliyefanikiwa. Mfano nimeenda kwenye conference nikakutana na wafanya biashara/academics/viongozi wenye nafasi..kama nikibahatika kupewa business card...naona ni jukumu langu ku-keep in touch. Hata asiponijibu email ya kwanza, ya pili, ya tatu..naamini iko siku atajibu. Wengine hawajibu si kwa nia mbaya lakini kwa sababu wanakuwa busy na majukumu. Unajua mawasiliano ni kipaji pia. I have tried it and it worked wonders for me.
 
Daaah kumbe watu wanakwepaga na watu masnitch, nimecheka sana...duniani kuna mambo....
Yupo mmoja huwa kila akitaka kujipima maendeleo yako, anapiga simu mida ya saa mbili usiku kupima kama utakuja na gari au daladala, kali zaidi ukionana naye analeta stori za madili makubwa makubwa kukupima kama upo level hiyo au la...
Huyo MSHAMBA
 
MKUU SIDHANI KAMA WANAJULIKANA MANAKE KAMA WANAJULIKA MBONA HAWASHITAKIWI???!
 
Back
Top Bottom