Ni changamoto gani unayokutana nayo unapokutana na marafiki waliofanikiwa katika maisha?

Alafu hii cjui huwaga inakuwaje, unakuta wale vilaza darasan ndo wanatusuaga maisha kinyama! Ukikutana nae adi aibu maana ulikuwa unamtesa kwa class yaan huwa ni kinyume huwez amin
Ni rahisi kuyashinda maisha kwa sababu hana anachopoteza kila hatua atakayo kuwa anaifanya, haogopi au haoni aibu kufanya shughuli yoyote iliyo mbele yake. Hafikirii kutafuta ajira yenye security tofauti na aliye soma. Yeye ni rahisi kujilipua ili mradi apate anacho kitaka kuliko msomi
 
Mleta mada anazungumzia urafikinwa tangu mnasoma wote mlikuwa kiwango sawa na baadae mnakutana wengine wapo vizur kwa maana wana ajira nzuri alafu wewe hujapata ajira au upo kwenye idara za kichovu kama ualimu.
Hahaa,Idara ya Afya vp mkuu..nayo ya kichovu?
 
Katika makuzi yangu nlikuwa na marafiki wa damu, hawa kiukweli hatujatupana japo wapo walotoboa na wasiotoboa, nikikutana nao huwa full story,,

Ila wale walokuwa mbalimbali nami aaaah huwa ni ukauzu kwenda mbele labda anichangamkie,

Alafu mi nlikuwa mwanasport footballer, nkikutana nao sanasana wanaulizaga vipi soka uliacha, nawajibu nliacha kitaambo, nlikuwa nawasugua bench hahahahah,ila kiwango kilipotea sababu za kupga kitabu kujumlisha na chuo.

Ila ndo ivo,,,,
 
Hakuna kuona aibu kwa sababu maisha bado yanaendelea.Marafiki wa kweli hukupa hata 'kasoda' kuonesha uimara wa urafiki.japo wengine waliofanikiwa hukwepa marafiki zao ili wasiombwe 'mpunga'
 
Kuna mwingine huyo tulikuwa vry close, mpk wengine wakawa wanasema tunapendana kma mapacha. Kuna wkt nilipata matatizo ofisin yaliyopelekea mimi kupelekwa police. Kuna ndugu yake mmoja, ambaye mimi nilifahamiana nae kwa kupitia yeye, akamuuliza, "ebana ishu ya mshkaji inaendeleaje? Akajibu "mi sijui anajua mwenyewe". Yule ndugu yke akasema lakn yule si mshkaji wako utasemaje hujui?? Alichokifanya akanitafuta kimyakimya kuniuliza kma tumegombana nikamwambia hapana. And its true sikuwahi kugombana na jamaa kwa lolote.

Baada ya mwaka kma mmoja nikiwa nimesafiri, nikapigiwa simu kwmb nyumbani kwangu nyumba ilikuwa inawaka moto. Nikawaza haraka haraka nani aliyepo jirani na kwangu na nina namba yake ya simu ninayeweza kumuomba anisaidie kwa sababu mimi nipo mbali na pale kuna watoto. Ikabidi nimpigie huyo jamaa. Kweli akaenda kwa sababu kutoka kwao mpk kwangu ni mwendo wa dakika kma 4 tu kwa miguu. Alipofika akanipigia na kuniambia jinsi watu wanavyookoa vitu, na kwmb familia yote ipo salama, kisha akakata simu. Alipokata nikampigia tena nikamuuliza kuna mabati yangu kma 130 yalikuwa store ndani, je yameungua au yameokolewa? Akanijibu "NGOJA NIRUDI NIANGALIE. NILIONDOKA KWENDA DUKANI KUNUNUA MAYAI". Daaah, nikapigwa na butwaa. Nikamuuliza yan mimi nyumba yng inaungua moto na mimi sipo, wewe unasema unaenda dukan kununua mayai..?? Nikakata simu. And believe me, machozi yalinitoka cz sikuamini nilichosikia kutoka kwa "best friend".

Nilichokifanya nikampigia fundi gereji mmoja aliyekuwa anatengeneza gari yng mara kwa mara, akaniambia yupo ofisini. Nikamwambia kama hutajali naomba uache unachokifanya uende kwangu kuna matatizo. Muda huo ilikuwa ni saa 11 jioni, yule fundi alienda pale akasimamia show nzima na kuhakikisha vitu vilivyookolewa vipo salama. Akatafuta gari familia na vitu vilivyookolewa ikapelekwa kwa ndugu yng. Akaondoka eneo la tukio saa 3 usiku.

Huyo "best friend" sikuwasiliana nae tena mpk leo, na ni zaidi ya mwaka sasa. Ila huwa tunapishana tu na hata niliporudi hakuja kuniona na nilirud kesho yake tu. Niliona bora nikae kimya.

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 
Dah!!!.....I'm speechless
 
Aisee! Hakuwa na moyo wa kusaidia huyo...angeweza kutafuta namna ya kukusaidia na wengine...huyo fundo siyo wa kumtupa tena ameiokoa familia yako
 
kama una elimu yako genuine wao ndiyo watakuwa wanakukimbia - sababu hata ukikaa nao hawajui kujenga hoja badala yake wanatumia vicenti vyao kama ngao. Nitawafuata waliko kama wakiniita hata kama nitatumia badaboda ila wakati wa kuondoka kila mtu atajipendekeza kuni-drive nilipopanga wa 4 x 4 zao sababu nina akili.

Kuwa na akli ni mtaji tosha hata kama huna mia mfukoni - You will fear nothing... mwenye akili hujiamini na mbumbumbu hutumia hela zake kuji-defend.
 
Mbona Wa Kolomije alikuwa kama wewe na katusua...kusoma sio kila kitu juhudi zako na mipango na MUNGU akitupia kajicho kwenye harakati zako weeee mbona watakuita freemason!
 
Hili naliafiki kwa asilimia mia moja, kuwa na maarifa ya kutosha kwenye kujenga hoja ukichanganya na maarifa ya maisha na mambo mengine na busara alizokujalia Mungu aaah hapo unasimama pazuri sana...
 
Sasa hapa wa kulaumiwa si wewe mwenyewe au? Kufeli ilifeli halafa ukawadanganya! Umegundulika unadai wao ndo wabaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…