Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Hayo ni mawazo yako; mali inayoibwa Tanzania na makampuni ya Kanada haimsaidii mlipa kodi wa Kanada ambaye ndiye anayetoa dola zake kuisadia Tanzania katika umaskini wetu. Waziri mkuu wa Kanada aliwahi kutamka kuwa Makampuni ya nchi yake yanavuna sana nchini kwetu kutokana na ujinga wetu na wala yeye binafsi na serikali yake hawafurahishwi na hali hiyo, kwa vile inabidi tena wamege fundu kujza bakuli letu kiasi ambacho tungejipatia wenyewe kutokana na raslimali zetu.
Kwa taarifa yako nchi za Magharibi zinataka Afrika iamke haraka sana iondokane na umaskini kusudi isiendelee kutumiwa na CHINA.
Nafikiri muanzisha thread anaposema nchi za magharibi anamaanisha serikali zao - jambo ambalo linayumkinika kabisa. Kama uliweza kumuona Tony Blair akiwa PM wa UK alivyotetea ununuzi wa rada ya Tanzania toka BAE systems akihakikisha kuwa ulikuwa mpango safi kabisa: "above board" kwa maneno yake, unaweza kuelewa jinsi maslahi ya kiuchumi yanavyopewa kipaumbele kwenye nchi hizo. Ni kweli kwamba wananchi wengi wa nchi hizo wanajali haki zetu kuliko hata viongozi wetu wenyewe. Aidha, kazi iliyofanywa na SFO kumthibitisha uongo Tony Blair i wazi kuonyesha baadhi ya watu makini walio tayari kupinga mitizamo ya viongozi wa serikali zao wasiosimamia maadili.