Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 609
Nafikiri hata majirani zetu pia wamefurai. Nchi nyingi zinapenda kushirikiana na sisi kwa sababu viongozi wetu hawajali rasirimali zetu. Dr. Slaa ,kampeni zake lazima ziliwatingisha wanyonyaji, alisema anagombea urais wa Tz sio Africa mashariki, Tanzania kwanza mengine baadaye na rasirimali zetu zinufaishe Tz kwanza. Msimamo kama huu lazima utaogopwa na wanyonyaji. Na nchi nyingi za magharibi ni wanyonyaji na 1.
Umenena, na ungetaja kabisa KENYA. Kichuguu bwana, amezaliwa mwezini huyo. NI TANZANIA PEKEE DUNIANI ambapo utaifa na uzalendo ulikufa siku nyingi. Wenzsetu hata kama ni wafanyabiashara binafsi wanachuma nchi zingine na kupeleka kwao. Na serikali zao zinawahakikishia ulinzi wa mali walizochuma na usalama wao. Wachina wanafanya kwa uwazi kuliko nchi nyingine duniani, maana wao wanakuja kama idara za serikali zao. Usidanganyike Kichuguu, hakuna msaada wa bure! Mzee Matsushita wa Japan ni mfanyabiashara binafsi lakini anatumia pesa nyingi kushawishi Bunge na Serikali yake itoe misaada Tz, halafu anakuja huku anawahi na makampuni yake kibao ya ujenzi nk kuchukua hizo kazi. Hivyo hivyo waswede. Ukiona msaada umekuja ni mtu binafsi ana-loby serkali yake isaidie Tz na kwa ajili hii anakuja huku kufanya hio kazi. Kuna kitabu kizuri unapaswa kusoma wewe 'Rich Dad' - nitakupa full citation baadae Nd Kichuguu- maana wewe ni lazima upigwe darasa la nguvu kweli kweli