Kwa heshima kubwa na taadhima nawasalimu katika hali zote
Mimi ni kijana wa miaka 27, elimu yangu ni ya kidato cha sita, niko Dar es salaamn. Nilisoma chuo kikuu, sikufanikiwa kumaliza kwa sababu ya changamoto za kiuchumi.
Ninaomba kazi ili nipate japo pesa ya kula na ya mahali pa kuishi kwani sasa hivi nalala mtaani na kwenye vijiwe vya kahawa na daladala.
Ninaweza kufanya kazi yoyote iliyo halali, yoyote ile, ninaweza kuandika document nyingi za kisheria, kufanya case research, kufanya typing, translation na interpretation
Kulima
Kufagia
Kulisha kuku
Kusajili kampuni na jina la biashara
Ninaomba kazi maisha ni magumu niko bila kazi na mbaya zaidi sina pa kuishi kwa sasa naishia kukesha kwenye vijiwe vya kahawa na stand, leo nimepata pesa kidogo nimekuja internet cafe niweze kuandika huu ujumbe mfupi ili yoyote atakayeguswa anisaidie.
Kwa mwenye mchango wowote wa hali na mali karibuni sana na Mungu awabariki.
Natanguliza shukrani.