Magari ya usiku kutokea Moshi niliyopanda yanatembea 80kms sijaona linalokimbia zaidi hivyo ni mwendo salama kabisa kwa usiku.Kwema wakuu?
Kwa Hali ilivyo usalama barabarani nyakati za usiku ni mdogo madereva hawazingatii sheria barabarani wakati wa usiku maana hamna polisi. Malori nayo ndio mida Yao ya kukimbia so ajali ni nyingi mno. Madereva pia usiku wanasinzia barabarani sababu ya uchovu.
Kuna siku nimesafiri na basi la Frester kwenda Dar es Salaam, kufika Morogoro usiku kama saa nane, dereva anataka kugonga semi za mafuta sababu anaovetake pia hamna polisi barabarani.
Hivyo hivyo gari la Abood juzi tumetoka Dar dereva anaendesha kwa kasi pia tulilipanda pale mbezi saa kumi na moja alfajiri gari haikufanyiwa service maana ilikuwa inatoka mkoani na watu wanashuka pale Mbezi na sisi tunapanda sababu hawana muda wa service.
Chonde chonde serikali sitisheni hizi safari
Labda ungeshauri wamiliki wa mabasi wahakikishe, wanaoendesha usiku ni wale wasio na upungufu wa nguvu za macho (uoni hafifu); kwani hilo ndilo laweza kuwa tatizo