Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,268
- 48,617
Hii Nchi kuna vitabia vya kiujamajamaa kwenye mambo ya biashara na masharti ya kipimbimbafuuuu.
Hata huo ujamaa haupo.
Huyu waziri yumkini alihongwa na watoa huduma za internet waliopo nchini, atengeneze mazingira ambayo yatazuia Starlink kuwepo nchini ili kuzuia ushindani. Hayo wanayafanya sana hawa watawala wa nchi hii, tangu zamani.
Namkumbuka waziri mmoja aliitwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee. Nami nikiwa mwalikwa pia. Yeye watengenezaji wa spring, ambao walikuwa chini ya wizara, wamchangie ili naye achangie kwenye harambee kama mgeni rasmi. Ilikuwa ni wakati wa utawala wa Kikwete. Watengenezaji wa spring za magari, wakamwambia waziri amtume msaidizi wake akachukue mchango. Msaidizi akaenda akapewa shilingi milioni 6. Waziri alivyoletewa, akamaka, tena mbele ya sisi wachache tuliokuwa pale tukiongea naye, "hawa wajinga sana. Wananichangia mimi milioni 6, wakati nimezuia spring kutoka nje ili wao wauze, halafu wananichangia milioni 6! Kawarudishie hiyo milioni 6 yao". Dereva akaondoka kwenda kurudisha pesa. Baada ya muda akarudi na pesa nyingi zaidi. Akamwuliza msaidizi wake, wamekupa shilingi ngapi? Msaidizi akasema milioni 12. Waziri akasema, afadhali. Cha ajabu kwenye harambee alichangia milioni 6.