Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,684
- 20,580
Ndugu zangu Watanzania,
Mheshimiwa Nape Nnauye waziri wa Habari ,Mawasiliano na teknolojia ya habari amesema ya kuwa serikali haikuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini bali walikwama wenyewe kutimiza mashariti yaliyohitajika kukamilishwanl ili kupewa lesseni.
Kauli hii imekuja kutokana na manung'uniko na kelele nyingi sana za watanzania mbalimbali mitandaoni kuilaumu serikali hususani waziri mwenye dhamana wakati huu ambao mtandao wa internet umesumbua sana na kukwamisha shughuli nyingi sana katika maofisi mbalimbali ya watu binafsi pamoja na serikali yenyewe.
Ambapo watu mbalimbali na wadau mbalimbali wa habari na mawasiliano wameonekana kutoa maoni yao mitaani na mitandaoni kuwa pengine kama Starlink angekuwepo hapa nchini ,suala lililokuwa limejitokeza hapa nchini la kukatika kabisa kwa huduma ya internet pengine lisingeathiri shughuli za watu binafsi pamoja na serikali yenyewe kama ilivyotokea.
Naweka kalamu chini na kuishia hapa. Chanzo cha taarifa yangu Ni clouds. Ukitaka kwa undani sana ingia clouds ujionee video yake kama una Mb au bando la kutosha kiasi.kama huna mb za kutosha basi wewe chukua hii taarifa kuwa serikali haikuwakatalia Starlink kufanya kazi Nchini bali wao ndio walikwama wenyewe kutimiza mashariti ya kupatiwa lesseni.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.