Nape hajawahi kuteuliwa kwa ajili ya uwezo wake, bali kwa heshima ya baba yake Moses Nnauye; hivyo asijisahau!

Nafasi za kupewa kwa hisani,niza kipumbavu,nazo zimejaa kwenye bara la kiza,hasa kusini mwa Sahara desert.Afrika hatuendelei sababu ya upumbavu wetu wenyewe.
 
Kwa hiyo tuna mtu ambaye hana vigezo kwenye hiyo nafasi
Nadhani kwa sasa tatizo letu ni kubwa kuliko suala la Nape kwenye nafasi aliyonayo. Ukitafakari sana, unafikiri hata Raisi Samia angependekezwa kuwa mgombea uraisi katika hali ya kawaida, kama sio kifo cha Magufuli? Yaani kwa mfano, baada ya Kikwete, tungeweza kusema raisi anaetufaa baada ya Kikwete awe Samia kutokana na rekodi yake hadi wakati huo?

Sifa za mgombea mwenza sio sifa ambazo tutazitumia kumteua mtu kuwa raisi wetu. Katika kuteua mgombea mwenza, tuna taratibu ambayo mgombea mwenza ni mpango wa kusawazisha mambo na Zanzibar, a political rather than pragmatic process. Kwa hiyo tunaweza kuweka mtu yeyote pale, sifa za uongozi sio kigezo bali U-Zanzibar wake. Na hakuna alietarajia kwamba Magufuli angekufa mgombea mwenza wake awe raisi. In fact, mgombea mwenza huwa anatakiwa mtu ambae hapaswi kuonekana ni makini kuliko raisi, asije akamfunika raisi. Mara ngapi umemsikia Dr. Mpango aki -shine?

Sasa swali ni kwamba, kama tungejua Magufuli angekufa akiwa raisi na makamu wake kuwa raisi, tungemteua Samia kuwa mgombea mwenza? Jiulize hili swali na uniambie jibu la Watanzania wengi kwa swali hili litakuwaje.

Ningependa Pascal Mayalla aje hapa ajibu hii issue kikatiba
 
Nape lini amewahi kuwa na uwezo ndugu?

Ndio huyu huyu somo la uraia alifeli?

Elimu yake baada ya hapo ina mazonge , najiuliza hivi hakuna taasisi inayoweza kufanya uchunguzi juu ya elimu za viongozi zenye mashaka ?

Maana wapo watu wengi tu wenye uwezo hawapati nafasi na wanakatishwa tamaa na hawa watu wenye elimu za kutia shaka.
 
1721386512088.png


Okay, legally speaking:D
 
Na huo mfumo ndio unawapa false confidence kuona wanaweza kufanya chochote, kusema chochote na hakuna wa kufanya kitu. Tumefikia mahali ambapo wanaokosoa hawa watu ndio wanaofunguliwa mashitaka na Polisi. Tunaenda wapi?
Lawama zote zipelekwe kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Hao ndio chanzo HALISI cha Matatizo ya nchi yetu. Wanawalinda na kufuata maagizo ya ovyo toka viongozi wa ovyo. Halafu wanatumika kuiba kura.


Na mwisho wa siku ccm wanakula pensheni zao.
 
Kwani alichoongea nape ni habari ya uongo? Shida ya watanzania tunapenda kujidanganya wenyewe hata Kwa mambo ya ukweli Alichokisema nape ndio ukweli

Hakuna ushindi wa Kura Kwa inchi za Africa Not only Tanzania ni Africa yote
Hatujasema kaongea uongo - kila Mtanzania anajua kaongea ukweli. Tatizo letu ni kwamba anatamba katika kushiriki uovu na uozo huo unaofanywa na chama chake kwa namna ambayo anatudharau na anatuona sisi ni wajinga sana pamoja na kujua kwamba yuko pale kwa heshima ya baba yake. Ingekuwa ni bora sana kama angekaa kimya kuliko kutukebehi kwa namna aliyofanya
 
Lawama zote zipelekwe kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Hao ndio chanzo HALISI cha Matatizo ya nchi yetu. Wanawalinda na kufuata maagizo ya ovyo toka viongozi wa ovyo. Halafu wanatumika kuiba kura.


Na mwisho wa siku ccm wanakula pensheni zao.
Mkuu, ungepitia jeshini ungewahurumia tu hawa watu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Mfano ni sawa na kusema mbwa mlinzi hatamheshimu na kumtikisia mkia mwenye kummiliki kwa sababu amekuwa kibaka katika mtaa na mbwa yuko kwa ajili ya kufukuza vibaka. Kesho pakiwa na mamlaka nyingine ya serikali, wataitii kama wanavyoitii hii iliyopo, hata kama nayo inafanya upoyoyo. Wanachofanya ni nature ya kazi yao, wanaapishwa kufanya hivyo. Wahurumie tu.
 
Mkuu, ungepitia jeshini ungewahurumia tu hawa watu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Mfano ni sawa na kusema mbwa mlinzi hatamheshimu na kumtikisia mkia mwenye kumliki kwa sababi amekuwa kibaka katika mtaa na mbwa yuko kwa ajili ya kufukuza vibaka. Kesho pakiwa na mamlaka nyingine ya serikali, wataitii kama wanavyoitii hii iliyopo, hata kama nayo inafanya upoyoyo. Wanachofanya ni nature ya kazi yao, wanaapishwa kufanya hivyo. Wahurumie tu.
🤣
Yaani wanavyokuwa serious na silaha zao kuwalinda ccm na kufanikisha wizi wa kura unaweza ukadhani ni matrilionea 🤣.

Ndio maana huko nchi za west Africa wanapinduana tu 🤣
 
Mzee Moses Nauye alikuwa na hekima na akili hawezi leta duniani bumunda la Hivi
 
% kubwa ya viongozi wetu wengi hawana uwezo, hata Prof. Assad majuzi hapa katuambia.
Nchi yetu ina mfumo mbovu sana wq namna ya kupata viongozi.
 
Hatujasema kaongea uongo - kila Mtanzania anajua kaongea ukweli. Tatizo letu ni kwamba anatamba katika kushiriki uovu na uozo huo unaofanywa na chama chake kwa namna ambayo anatudharau na anatuona sisi ni wajinga sana pamoja na kujua kwamba yuko pale kwa heshima ya baba yake. Ingekuwa ni bora sana kama angekaa kimya kuliko kutukebehi kwa namna aliyofanya

Mzee mnauye alikuwa na Heshima kubwa kuliko Nyerere?

Au mzee nauye alikuwa na Heshima kuliko mkapa? Mbona watoto wa mkapa sio wabunge wala mawaziri?

Point yangu ni kuwa nape Yuko pale Kwa Elimu yake na uwezo wake

Na alichokiongea ndio uhalisia wa uchaguzi wa Africa
 
Back
Top Bottom