Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,147
- 21,166
Huu ni ukweli ambao kama Nape angeutafakari basi angekuwa ana heshima kubwa sana kwa Watanzania na kuepuka kutenda au kuongea mambo yenye kuleta karaha kwa wananchi. Nape katika maisha yake yote ya nafasi za uongozi hajawahi kuteuliwa kwa sababu ana uwezo wa kuwa kiongozi, bali ni kwa sababu ya heshima ambayo viongozi waliomteua walikuwa nayo kwa baba yake Moses Nnauye. Hii ni heshima ambayo Kikwete na Mkapa walimpa kutokana na connection waliyokuwa nayo na Mzee Mozes Nnauye. Hii ni connection ambayo Magufuli hakuwa nayo hivyo hakuona shida kumtoa Nape kwenye uwaziri. Samia yeye kamrudisha kwa sababu ya kivuli cha Kikwete na Kinana, sio kwa kutambua uwezo wa Nape.
Nape, na vijana kadhaa kama yeye walioko kwenye nafasi kama za Nape na nyingenezo, jaribuni kukumbuka hampo kwenye nafasi hizo kwa sababu ya uwezo wenu au kwa kuwa mnatuzidi uwezo sisi ambao hatupo kwenye hizo nafasi. Hatupo hapo kwa sababu sisi baba zetu sio kina Mzee Moses Nnauye, na sio kwa sababu mnatuzidi uwezo wa kuwa viongozi wa taifa hili. Bila baba zenu, mama zenu, hizo nafasi msingezipata. Tunakumbuka kazi kubwa ya Mzee Moses Nnauye kuhamasisha askari, hasa mgambo, kuendelea kupigana wakati wa vita vya Kagera, pale mizinga ya Idd Amin ilipopigwa wakawa wanakimbia kwa woga. Kuteuliwa kwa heshima ya baba na mama zenu ni hisani za viongozi wapya wanapoingia madarakani, sio kwa sababu CCM au serikali ina wenyewe ambao ni baba zenu, mama zenu, na hivyo na nyie muwe na tarajio la watoto wenu kuwa viongozi wa taifa hili. Tanzania sio taifa la kifalme.
Kwa hiyo msijione mna uwezo au akili kutuzidi na kutoa matamko mkidhani sisi mnaotuongoza ni watu mbumbumbu. Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika kwa sababu waliokuwa madarakani waliona serikali ya Zanzibar ya wakati huo ilikuwa ina wenyewe. Mkiendelea na mentality mliyonayo itabidi tujikumbushe na kutafakari, kwa nini mapinduzi ya Zanzibar, tunayoyakumbuka kila mwaka, ilikuwa ni lazima yafanyike.