Napata pesa ila mapenzi yananifanya narudi nyuma hatua milioni moja

Nimekuwa ni mmoja wa watu ambao nikiwa na pesa nakuwa mwepesi sana kupata totozi na nawaburuza kweli kweli ila yote hii ilikuwa ni kwa sababu napata vihela vya kawaida kwa hyo skuwa na malengo makubwa zaidi ya kuhitaji kuongeza kipato changu, ila kwa sasa kipato changu kimekuwa na ugonjwa wangu wa wanawake unaongezeka kwa kasi ya ajabu maana kila nikipata pesa nashindwa kuhifadhi mimi nikutumbua tu kwani nakuwa na msukumo mkubwa sana kutoka ndani yangu unaotaka nitumie hiyo hela kwa matumizi ya wakina dada, je wenzetu mnafanyaje kuweza kuhifadhi fedha na kutumiza malengo yenu???
Pesa haikai kabisa na mwaka ndo unakaribia katikati hata vile vimalengo vidogo vidogo vinaanza kunishinda naona hadi aibu maana maisha niliyonayo hayaendani na kipato changu.
Tupo njia moja, mi ni mwanamke mmoja tu ndo anaenisumbua na mimi npenda kupita kiasi, na amejua udhaifu wangu, bt nafanya juu chini lazma nitatue ili tatizo na nipo kwenye hatua,,,,,,,
 
Sababu za kuwaepuka unazo, nia ya kuwaepuka unayo uwezo wa kuwaepuka 'eti' huna. Kwanza acha kutuzuga, rekebisha kauli....unataka njia ya kujiepusha sio kuwaepuka maana we ndio unawatongoza.

Njia ya kwanza tafuta mke weka ndani ili akusaidie kukupa akili maana mpaka hapo we huna akili za kutosha. Ukishaoa usiwe mkorofi, acha mkeo akuongoze katika mipango ya maendeleo....ndio,...maana kama huna akili ya kujiongoza huwezi kumuongoza!

Njia ya pili jifanye kama umechanganyikiwa vile usitishe urafiki na hao marafiki zako ambao hawana maendeleo wala hawana story za maendeleo. Acha kabisa kampani za wanawake maana walio wengi (sio wote) hawana tabia ya kutoa ushauri kwa wanaume wasio waume zao!, Kwa kifupi sio wepesi wa kutoa ushauri na hawafanyi maendeleo mpaka wanapokua na familia!, wengi wanatunza cash na huwezi kujua ukajifunza mbinu zao!
 
Njia nzuri ni kuwaepuka hao wadada na kuhakikisha unapata kitu mbadala cha kufanya kwa muda ule ambao ungetumia kuwa nao
 
Utakuwa na pepo mkuu sio bure, yaani kahela kangu nipate kwa jasho hivi then nihonge tu kirahisirahisi ...hapana aisee
 
Pole sana kaka, naona kama vile tunafanana japo mim si kuhonga wadada ila ni starehe sana kwa kwenda mbele, yani million kwangu marufuku kukaa wiki mbili, ili hali mshahara wangu siyo mkubwa lakini navyo spend waweza shangaa, mfano mwingine nashindwa hata kuoa kwa sababu naona harusi ni gharama sana wakati huo huo namaliza pesa zote kwenye starehe, aisee Mungu anahitajika sana kwenye suala hili,
Ukipata suluhu ya hili pliz let me know ili nami ni copy and paste kwangu
 
Naamini tutatoka salama kwenye hili jaribu
 
mtume muhammad rehema na amani zimshukie aliwah kusema ktk mafundisho yake kuwa hakika uzinifu unaleta ufakiri ( umasikini).
 
Pole sana kaka, naona kama vile tunafanana japo mim si kuhonga wadada ila ni starehe sana kwa kwenda mbele, yani million kwangu marufuku kukaa wiki mbili, ili hali mshahara wangu siyo mkubwa lakini navyo spend waweza shangaa, mfano mwingine nashindwa hata kuoa kwa sababu naona harusi ni gharama sana wakati huo huo namaliza pesa zote kwenye starehe, aisee Mungu anahitajika sana kwenye suala hili,
Ukipata suluhu ya hili pliz let me know ili nami ni copy and paste kwangu
Naamini tutatoka salama kwenye hili jaribu
 
Utakuwa na pepo mkuu sio bure, yaani kahela kangu nipate kwa jasho hivi then nihonge tu kirahisirahisi ...hapana aisee
Kwako hili ni jipya?? Watu wanabeba zege ila wakitoka hapo jioni anapeleka hela kwa mademu, hii ni kawaida san muombe mungu sana nakumshukuru kwa kukuepusha na hili janga
 
Back
Top Bottom