Naona si sahihi mtu kuweka plate namba ya Jina lake

nilichojifunza maskini tuna katabia fulani ka kijinga sana yaani vile vitu tusivyoweza kumudu kutokana na umaskini wetu basi huwa tunaviundia namna vionekane vibaya au ni ushamba kufanya....... mtu ana ndinga yake ya over 300m alafu kaweka jina lake pale ww maskini unawezaje kusema ni ulimbukeni wakati gharama ya plate number na gari vikibadilishwa kuwa pesa mnagawana ukoo mzima hadi mpigane mkafie mbali......


maskini tuache kujitwisha mizigo mingi hapo mtu hajala kitu ya kueleweka ni mzigo wa kwanza pili anaishi pasipoeleweka ni mzigo wa pili bado umebeba mizogo ya kufuatilia watu ambao muda mwingine hata huwajue ubebe mzigo wa chuku uvivu wivu na huenda muda mwingine unaloga kwahyo mizigo ipo kibao.

relax chukulia vitu kwa upande chanya zaidi
Bado ni ulimbukeni... Tetea vile uwezavyo hata uniite masikini mara elfu. Bado haibadiliki kwamba huo ni ulimbukeni.
 
Ulimbukeni ni wewe hapo kupangia matumizi halali ya wanaume wenzio wakati hela hukuwasaidia kutafuta. Tabia hizi wanatakiwa kuwa nazo wanawake kwenye ndoa tu.

Ungekuwa na gari la hadhi hiyo ila hukuweka private plate hapo angalau, ila sasa ukute gari lenyewe huna alafu unaleta maoni.
Inawezekena kweli gari sina. Ila bado ni ulimbukeni. Ushamba. Mtu mwenye pesa hawagi na hizo mambo. Malimbukeni tu ndo tabia zao hizo.
 
Back
Top Bottom