John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 5,534
- 12,274
Tangu muda mrefu nimekuwa nikiwiwa kutaka kuanzisha Taasisi au Kampuni Binafsi ya Upelelezi hapa nchini Tanzania ili kufanya uchunguzi juu ya masuala mbalimbali ambayo yanahitaji kuchunguzwa.
Kikwazo kikubwa kinachoikabili hii dhamira yangu ni kutokufahamu namna au utaratibu rasmi ambao ninapaswa kuufata ili sasa niweze kuanzisha taasisi hiyo ambayo itakuwa legally recognized hapa nchini. Kuhusu mahitaji ya msingi ya kuanzia, yaani "manpower" na "logistics", hakuna kikwazo au changamoto kubwa sana kuhusu hilo.
Tatizo kubwa lipo kwenye utaratibu au namna ya kuanzisha na kuendesha mchakato wa kuweza ku-officiate hiyo taasisi ili itambulike rasmi na kuweza kufanya kazi zake kama tunavyodhamiria. Nimejaribu kufanya utafiti katika nchi zingine naona taasisi kama hizo zipo lakini sijafanikiwa kupata taarifa sahihi juu ya namna gani wenzetu wamefanyaje hadi kufanikisha kuwepo kwa taasisi hizo katika nchi zao.
Nafahamu humu tupo watu wengi wenye uelewa, utaalamu na ujuzi tofauti tofauti ktk nyanja mbalimbali, naomba mchango wenu kuhusu suala hili kwani penye wengi haliharibiki neno. Je, hatua zipi au utaratibu upi ninapaswa kufuata ili niweze kusajili taasisi ya aina hii? Mamlaka ipi hasa ambayo inahusika na suala hili?
BRELA? Au RITA? Au nyingine zipi? Sheria gani hasa (endapo kama zipo) ambazo zinahusika na suala hili?
Ushauri wenu ni muhimu sana katika hili ili niweze kufanikisha lengo langu hili. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
Karibuni.