Naomba kuuliza kwani Siku hizi tunavishana Nishani za JWTZ kwa Unguja na Pemba au ni kwa Utanzania wetu kumaanisha Umoja wetu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,948
119,225
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob Mkunda kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali majenerali, maafisa na askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) kutoka Pemba na Unguja - Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Oktoba 25, 2024 .

Nishani hizo ni za utumishi uliotukuka, utumishi mrefu, tabia njema, miaka 60 ya muungano pamoja na nishani ya miaka 60 ya JWTZ.

Aidha, Jenerali Mkunda amewavisha nishani ya Jumuiya ya SADC maafisa na askari walioshiriki ulinzi wa amani nchini Msumbiji chini ya mwavuli wa jumuiya hiyo.

Chanzo: azamtvtz

Ukiona hata Mtu anayetakiwa Kujiamini mno mahala alipo nae anaanza Kujipendekeza jua Hatari imejificha mahala.
 
Back
Top Bottom