Naomba kujua tofauti ya kazi za Afisa Mipango na Mchumi kwenye taasisi au halmashauri?

GOSSO MZEKEZEKE

Senior Member
Dec 13, 2013
172
195
Habari wanaJF,

Naomba kujua utofauti wa kazi au majukumu ya afisa mipango(Planning officer) na mchumi kwenye maeneo mbalimbali ya halmashauri au taasisi mbalimbali za serikali.

Anayefahamu naomba anijuze.
 
Hakuna utofauti mkuu ila kuna baadhi ya taasisi hasa Halmashauri wanapenda kuwaita Afisa mipango. Idara ya Mipango inajumuisha Watakwimu, Wachumi hawa kazi zao ni moja tu na huwa wanakua Idara moja. Ndomana wanawaita afisa Mipango sometimes ila hakuna tofuauti mkuu.

Kazi zao ni kuandaa proposals za research au projects, kufanya monitoring na evaluations ya miradi mbalimbali, Kukusanya data za uchumi/takwimu, kuandaa bajeti, vyanzo vya mapato nknk. Mambo yanayohusu uchumi na takwimu, tafiti na Miradi hizo ndo kazi zao afisa Mipango.
 
Asante kwa ufafanuzi. unajua kuna mtu aliniambia kuwa maafisa mipango wanatoka chuo cha mipango IRDP dodoma na kwa sasa ndio ambao wanaajiriwa kama planning officer na hasa waliosoma kozi inaitwa regional planning(kama nimekosea). Sasa nikafuatilia kuna watu waliwahi kuajiriwa kama planning officer ila wamesoma uchumi na takwimu, nikadhani kazi zao zitakuwa zinafanana tu kama ilivyo kazi za uchumi na takwimu maana zinaingiliana. Hivyo zilinichanganya. Na pia juzijuzi walitangaza kazi za uchumi TRA nikaona watu wa mipango wanaomba, nikauliza mnaombaje wakati nyie ni maafisa mipango, ndio wakanijibu maafisa mipango na wachumi ni walewale na kazi zao ni zilezile isipokuwa inategemea na ikama(muundo) wa ofisi umewaeka kama wachumi au mipango,. Kwa hiyo kwa majibu yako nashukuru sn.
 
Afisa mipango na wachumi ni watu wawili tofauti ingawa baadhi ya taasisi wanakaa kweny ofisi moja kama halmashaur, ila ata halmashaur afisa mipango ni mipango tu,mchumi ni mchumi na mtakwimu ni vilevile but wanakaa kweny ofisi moja kwa maana baadhi ya majukumu wanaingiliana. Lakini hao ni watu wawili tofauti.
 
Back
Top Bottom