Nani anagharamia matumizi ya Lema, Msigwa na Mbowe huko Nairobi?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Habari Wanajamvi,

Kwanza natanguliza pole na kumtakia mema Kamanda wetu Tundu Lissu. Lakini najaribu kufikiri kwanini Msigwa na Lema bado wako Nairobi?

Kwa gharama za nani? Kama za kwao kwanini wasirudi nyumbani kisha hizo fedha wachangie kwenye matibabu?

Tena lile jopo limeambatana na Wake na wenza wao, WHY?

Yawezekana na wao ni sehemu ya matumizi ya fedha zinazochangwa na Watanzania walalahoi........

Jamani rudini nyumbani tuhamasishe michango maisha ya Nairobi ni ghali sana......
 
Hivi unategemea mtu kama Lema aliyesaidiwa kwa hali na mali na Tundu Lissu hadi akarejeshewa ubunge wake leo ashindwe kuishi Nairobi kwa gharama zake binafsi za kula kulala na kusafiri kwenda hospitali? Wala hashindwi! Yule kule Nairobi anaishi kwa gharama zake na vilevile mchango anatoa. Msigwa yeye alikuwa miongoni mwa wabunge wawili walioondoka na mgonjwa na hawezi kurudi yeye wala Mbowe mbali na kwamba wanatumia gharama zao binafsi.

Mimi mwenyewe naelekea huko na sitashindwa kuishi kule hata kwa mwezi mzima kwa gharama zangu na michango ya matibabu naenda kutoa. Roho ndogo kama hiyo muachie Magufuli mkuu, wewe hutakiwi kuwa nayo!
 
Kwani wakiwa Tanzania huwa wanaishi kambini labda au wanalishwa na Serekali?
Tatizo unadhani Msigwa na Lema ni masikini kama baba yako pole sana.
Pepo la umasikini limekushika mpaka unalala ukiwaza wanaoumuuguza mgonjwa wangerudi ili mchawi wewe ukafanye yako
Najua sio masikini lakini kwanini hizo fedha wasichangie kwenye matibabu kuliko kukaa huko Nairobi bila sababu ya msingi?
 
Hivi unategemea mtu kama Lema aliyesaidiwa kwa hali na mali na Tundu Lissu hadi akarejeshewa ubunge wake leo ashindwe kuishi Nairobi kwa gharama zake binafsi za kula kulala na kusafiri kwenda hospitali? Wala hashindwi! Yule kule Nairobi anaishi kwa gharama zake na vilevile mchango anatoa. Msigwa yeye alikuwa miongoni mwa wabunge wawili walioondoka na mgonjwa na hawezi kurudi yeye wala Mbowe mbali na kwamba wanatumia gharama zao binafsi.

Mimi mwenyewe naelekea huko na sitashindwa kuishi kule hata kwa mwezi mzima kwa gharama zangu na michango ya matibabu naenda kutoa. Roho ndogo kama hiyo muachie Magufuli mkuu, wewe hutakiwi kuwa nayo!
Najua hashindwi wala sijasema anashindwa lakini juhudi na upendo wake umedhihirika katika anga la Tanzania lakini kwanini asirejee nyumbani na hizo fedha akaziwekeza katika kuokoa maisha ya Lissu? Huoni kama atakuwa amefanya kitu Positive zaidi?
 
Habari Wanajamvi,

Kwanza natanguliza pole na kumtakia mema Kamanda wetu Tundu Lissu. Lakini najaribu kufikiri kwanini Msigwa na Lema bado wako Nairobi?

Kwa gharama za nani? Kama za kwao kwanini wasirudi nyumbani kisha hizo fedha wachangie kwenye matibabu?

Tena lile jopo limeambatana na Wake na wenza wao, WHY?

Yawezekana na wao ni sehemu ya matumizi ya fedha zinazochangwa na Watanzania walalahoi........

Jamani rudini nyumbani tuhamasishe michango maisha ya Nairobi ni ghali sana......
Wewe ulichangia kiasi gani mpaka zikuume au umejitekenya?
 
Najua sio masikini lakini kwanini hizo fedha wasichangie kwenye matibabu kuliko kukaa huko Nairobi bila sababu ya msingi?
Mkuu, kwa nini pesa ya bando usingechangia matibabu badala ya kuja kulalamika hapa?!
Na kama wangekuwa hapa kuna ambao wangehoji kwa nini hawamjali mgonjwa! Na watu wasingekubaliana na hiyo hoja kuwa wachange tu halafu wao wabaki kukimbizana na polisi maana hao wasingeogopa kushiriki maombi ya kumuombea Lissu.
 
Aliyekwambia bando nalipia nani?
 
Najua hashindwi wala sijasema anashindwa lakini juhudi na upendo wake umedhihirika katika anga la Tanzania lakini kwanini asirejee nyumbani na hizo fedha akaziwekeza katika kuokoa maisha ya Lissu? Huoni kama atakuwa amefanya kitu Positive zaidi?
Sasa unataka mgonjwa aachwe kule Hospital mwenyewe ili kuokoa gharama? Mkuu naona unashindwa kujua umuhimu wa uwepo wa watu karibu na mgonjwa! Kumbuka kuwa Lissu alishambuliwa na wanaosadikiwa kuwa ni wa mhimili mrefu hivyo ni lazima kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ukaribu wa watu wanaoweza kujitoa pale patakapokuwa na hatari! Lissu bado hayuko salama mkuu. Twende zetu Nairobi tukampe faraja mzalendo wetu wasiye mnafiki na asiye na chuki wala roho ndogo kama ya "Bwana yule"
 
Back
Top Bottom