Nani alisema kuwa serikali haifanyi biashara? Hii ni ajenda ya viongozi majambazi ya mali za umma

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,343
13,014
Hii kauli ya kuwa Serikali haifanyi biashara wala haipaswi kujihusisha na biashara binafsi sifurahishwi nayo hata kidogo.

Ajabu kwamba inatolewa na taifa linalo jitanaibisha kuwa linafuata sera za ujamaa na kujitegemea kwa mujibu wa katiba yake.

Mpaka unajiuliza huo ujamaa na kujitegemea upo wapi kama mali na rasimali karibu zote za nchi wanagawiwa watu binafsi wazisimamie huku serikali ikijiweka mbali, ni lini huko kujitegemea kutawezekana.

Hii kauli ya kuwa serikali haifanyi biashara ni kauli ya kitapeli na ya kijambazi ili kupumbaza wananchi na kuwa aminisha ujinga kuwa serikali haiwezi fanya biashara huku viongozi majambazi wakinufaika na makampuni binafsi kufyonza mali za umma vile watakavyo.

Haiwezekani rasimali zote za nchi tuwakabidhi watu binafsi wageni wavune vile watakavyo halafu tutegemee tutafanikisha huko kujitegemea kwenyewe kama katiba inavyoimba.

Uzembe, ufisadi na madili hautimbiwi kwa kuwapa mali za umma wageni bali unatibiwa kwa uwajibikaji na kuwajibishana.

Swali la kujiuliza hao wajamaa wenzenu ambao kila uchwao mnaenda kujifunza huko China wao wamefanikiwaje kuendesha utitiri wa mashirika ya umma yanayo simamia rasimali zao zote kwa ajili ya kunufaisha nchi yao na kujitegemea wamefanikiwaje ?

Kwa nini wao hawafanyi ubinafsishaji kwa fujo kwa kigezo cha kwamba serikali haifanyi biashara ?

Au ni kwetu tu ndio kuna ufisadi, wizi, uzembe na madili ndani ya mashirika ya umma ?

Haya majambazi ya mali za umma yanayo vaa suti yanayopiga kelele kuwa serikali haifanyi biashara yana agenda yao kubwa kuwa aminisha wananchi ujinga wao ili wawaibie vizuri wananchi kupitia watu binafsi.
 
Engine ya uchumi wa China ambao ndio wajamaa wenzenu ni mashirika ya umma ambayo yameshirkiria sekta zote.

Wana mashirika ya umma zaidi ya laki moja

Tena zile sekta nzito yanatikisa mpaka dunia.

Sisi wajamaa uchwara engine ya uchumi wetu ni ujambazi wa ubinafsishaji inasikitisha sana.

Haya majambazi ya mali za umma yanayo vaa suti yanapaswa kupigwa mawe.
 
Back
Top Bottom