Naiona CCM ikifanikiwa na kudumu zaidi ya miaka 20 Ijayo

Sasa kama wapinzani hawaeleweki na wametawanyika hawajui wanachokipigania wapo wapo tu! woga wa malaika mkuu hadi kuamua kujificha nyuma ya mgongo wa polisi ili kuendesha nchi kidikteta kauli za vitisho kila kukicha na visasi juu unatoka wapi!? Si ndiyo angeona hawa wapinzani hawajitambui hivyo uchaguzi anashinda kirahisi kabisa! Anapitisha katiba mpya ya rasimu ya Warioba na pia kuruhusu Tume huru ya uchaguzi. Thubutu! anajua Watanzania tutafanya kweli na kuipiga chini CCM milele. Hapo kwenye rangi neno halisi ni gharama hatuna neno ghalama kwenye lugha yetu ya Taifa.
Watanzania wa nyuma ya keyboard, Ila hawa wanaopiga kura wakifanya maamuzi sahihi, kesho utakuja na thread WATANZANIA HAWAJITAMBUI ngoja waisome namba kumbe wewe ndio unashindwa kuona mambo kupitia jicho la uhalisia
 
Idumu milele wengine hatuna cha kupoteza, watoto wanasoma International school, naishi nyumba nzuri tu *classic bangaluu* familia ina bima ya afya tena AAR natibiwa East Afrika bure.... kipato siyo haba! Endeleeni kuwanyonga wanyonge lakini mkumbuke kuna maisha baada ya hii dunia
 
Nimeandika kuhusu katiba na Tume huru ya uchaguzi umeamua kupotezea! Achana na ubashite. Watanzania wanajitambua sana ndiyo sababu MACCM wanaiogopa katiba mpya ya rasimu ya Warioba na pia Tume huru ya uchaguzi. CCM imechokwa kupita kiasi miaka 56 madarakani nchi ina utajiri wa hali ya juu. Mafisadi wachache ndani ya Serikali na MACCM wanakuwa mabilionea lakini Watanzania kwa asilimia kubwa sana wanaishi katika maisha ya ufukara wa kutisha hata mlo mmoja tu hawajui wataupata wapi. Kila kitu chetu nchini ni shaghala baghala imefikia mahali MACCM yanapeana rushwa ili kupitisha muswaada wa kihuni ili kuminya uhuru wa habari nchini. Tafakari kwa kina Mkuu achana na kudumaza akili yako.

Watanzania wa nyuma ya keyboard, Ila hawa wanaopiga kura wakifanya maamuzi sahihi, kuesho utakuja na thread WATANZANIA HAWAJITAMBUI ngoja waisome namba kumbe wewe ndio unashindwa kuona mambo kupitia jicho la uhalisia
 
Ninazitabiria Harakati za CCM zinazoendelea sasa Dodoma kukifanya kuwa Chama chenye nguvu ya kuendelea kubaki Madarakani kwa miaka mingine zaidi ya 20.

-->Ninaona watu wenye mitazamo tofauti na CCM ya awali wakimiminika kujiunga na CCM

---->Mabadiliko ya sasa na Fukuzafukuza hii, Siioni ikiidhoofisha CCM hata chembe badala yake inaonyesha CCM kama chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kikomavu.

----> Ninaona CCM maslahi wakiachana na siasa, na kuanza kujaribu vitu vingine vya kufanya nje ya siasa maana Chama Sio tena sehemu salama ya kutimizia ndoto zao kimaslahi.

---->Ninaona Hakuna Vuguvugu lolote nje au ndani ya chama cha Mapinduzi likiibuka na kufanikiwa kuidhoofisha .

WAPINZANI wa CCM kama wasipobadilika na kuja na mbinu mpya zaidi ya kudandia matukio, mfano leo masikio yamesimama yameelekea DODOMA badala ya UFIPA kwenye meza ya mipango kujiandaa kupambana na CCM mpya ambayo Muda sio mrefu kishindo chake kitapokewa kwa shangwe nchi nzima Wataendelea kudumu zaidi ya miaka 20 ijayo wakiwa na ushawishi huuhuu ulio chini ya wastani...
We endelea kutabiri ivoivo
 
Jamaa kagundua hana mvuto ndani ya chama hivyo imebidi kutumia polisiccm ili wampe kinga vinginevyo chaliii! awamu moja tu. Ngoja tusubiri tuone hawa waliofukuzwa na wale wote ambao hawataki mabadiliko anayoyataka malaika mkuu ili kumpa nguvu zaidi kuelekea 2020 wataamua kupambana naye vipi. Angalia hapa picha ya jana kashindwa kumuangalia Membe usoni kwa unafiki wake.

17202720_1752041818459688_1257049282776818419_n-jpg.479911
mkuu picha haifunguki...i-upload kwa kupitia mobile phone...uki-upload toka ktk laptop au desktop huwa inaleta shida kufunguka ktk android phone.

hili sidhani kama wahusika wa hii forum kama wamelibaini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ninazitabiria Harakati za CCM zinazoendelea sasa Dodoma kukifanya kuwa Chama chenye nguvu ya kuendelea kubaki Madarakani kwa miaka mingine zaidi ya 20.

-->Ninaona watu wenye mitazamo tofauti na CCM ya awali wakimiminika kujiunga na CCM

---->Mabadiliko ya sasa na Fukuzafukuza hii, Siioni ikiidhoofisha CCM hata chembe badala yake inaonyesha CCM kama chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kikomavu.

----> Ninaona CCM maslahi wakiachana na siasa, na kuanza kujaribu vitu vingine vya kufanya nje ya siasa maana Chama Sio tena sehemu salama ya kutimizia ndoto zao kimaslahi.

---->Ninaona Hakuna Vuguvugu lolote nje au ndani ya chama cha Mapinduzi likiibuka na kufanikiwa kuidhoofisha .

WAPINZANI wa CCM kama wasipobadilika na kuja na mbinu mpya zaidi ya kudandia matukio, mfano leo masikio yamesimama yameelekea DODOMA badala ya UFIPA kwenye meza ya mipango kujiandaa kupambana na CCM mpya ambayo Muda sio mrefu kishindo chake kitapokewa kwa shangwe nchi nzima Wataendelea kudumu zaidi ya miaka 20 ijayo wakiwa na ushawishi huuhuu ulio chini ya wastani...
Mkuu umesahau kuwa wananchi ndio tunaamua chama gani kibaki madaraki japo sina uhakika kama huu mfumo unafanya kazi kwenhe nchi nyingi za afrika na kingine..mabadiliko ya CCM yana manufaa gani kwa wananchi..
 
Huko kwenye dola umeenda mbali , Uwepo wa wapinzani ambao wanaoperate chini ya viwango na hawaeleweki wanachokipigania wakiwa wametawanyika kama wajenzi wa mnara wa babeli na kukaa kusubiri tukio walifanyie amplification ni tiketi isiyo na ghalama ya kuendelea kuwepo kwa ccm, hilo ni pambano katika phase ya chini kabisa
Siasa ya Tanzania ni matukio, mkipuyanga upinzani lazima watawasema tu, na upinzani wakipuyanga hadi matusi mtawatukana kuonesha furaha iliyopitiliza ila kimsingi mmepuyanga na ndo mda wa wapinzani kuwachokonoa na kuwakejeli, na mkae mkijua watanzania wanasubili hatma ya bashite.
 
Jamii imeridhishwa na utendaji wake? Mfumuko wa bei, suala la upendeleo (Bashitism), unyanyasaji kwa wahanga wa majanga na kwa watumishi wa umma. Hivi Ndio vya kukiweka chama salama.
 
Huko kwenye dola umeenda mbali , Uwepo wa wapinzani ambao wanaoperate chini ya viwango na hawaeleweki wanachokipigania wakiwa wametawanyika kama wajenzi wa mnara wa babeli na kukaa kusubiri tukio walifanyie amplification ni tiketi isiyo na ghalama ya kuendelea kuwepo kwa ccm, hilo ni pambano katika phase ya chini kabisa

Kifupi kabisa

CCM inaishi kwa nguvu za dola

1. Mikutano ya wapinzani imewekwa kolokoloni

2. Wapinzani wanakatwa na kutishwa popote

3. CUF inayumbishwa kutwa kucha na CCM kupitia akina MUTungana na Reprofer Pumba

4. Tumeshuhudia wakuu wa majeshi wastaafu wakipewa vyeo kemkem ndai ya ccm wanapostaafu eg ukuu wa mkowa ni cheo cha ccm

5. Wanasheria kuingizwa CCM ilikukilinda.... Mfano Tulia Atikison

6. Kuiba kura na kulazimisha matokeo kutumia majeshi au mahakama

7. Kuiba fedha za umma kuzitumia kujenga ccm yao

Sisiemu bila utapeli kupitia dola na Mahakama weupe kabisaaa....mara kumi ccj wanajiweza
 
Jamii imeridhishwa na utendaji wake? Mfumuko wa bei, suala la upendeleo (Bashitism), unyanyasaji kwa wahanga wa majanga na kwa watumishi wa umma. Hivi Ndio vya kukiweka chama salama.
Hapo ongezea na bomoabomoa ilofanyika juzi usiku huko buguruni, kweli wana imani na ccm
 
ZIMERUDI ZAMA ZA "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZIIIIIII,ZIDUMU FIKRA(SAHIHI)ZA MWENYEKITI WA C-C-EM.
 
We uko upande wa wengi au wachache?!
kwa heshima ya democrasia na kuwajibika pamoja,kitakachoamriwa na wengi maana yake CCM ndio imeamua.
mkuu ndio maana hatuna marais wawili aliyejaguliwa na wengi ndio wa wote hadi utakapoitishwa uchaguzi mwingine.
Hao wachache wananafasi mbili
1:Kutafuta mahala pengine pa kuimpliment mawazo yao
2:Kuungana na maamuzi ya wengi hadi pale itakapotokea nafasi tena ya kushawishi wanachoona ni sahihi na kikikubalika na wengi kitafuatwa, vry simple.
 
Kwahiyo ndiyo kusema kofia mbili mwiko zimeanzia kwa MWENYEKITI TAIFA?na kama ndiyo anaacha kipi?chama au jumba la enzi?
 
kwa heshima ya democrasia na kuwajibika pamoja,kitakachoamriwa na wengi maana yake CCM ndio imeamua.
mkuu ndio maana hatuna marais wawili aliyejaguliwa na wengi ndio wa wote hadi utakapoitishwa uchaguzi mwingine.
Hao wachache wananafasi mbili
1:Kutafuta mahala pengine pa kuimpliment mawazo yao
2:Kuungana na maamuzi ya wengi hadi pale itakapotokea nafasi tena ya kushawishi wanachoona ni sahihi na kikikubalika na wengi kitafuatwa, vry simple.
Umejibu vizuri, lakini nasikitika kusema hujajibu nilichouliza
 
Back
Top Bottom