Naiona CCM ikifanikiwa na kudumu zaidi ya miaka 20 Ijayo

Nimeandika kuhusu katiba na Tume huru ya uchaguzi umeamua kupotezea! Achana na ubashite. Watanzania wanajitambua sana ndiyo sababu MACCM wanaiogopa katiba mpya ya rasimu ya Warioba na pia Tume huru ya uchaguzi. CCM imechokwa kupita kiasi miaka 56 madarakani nchi ina utajiri wa hali ya juu. Mafisadi wachache ndani ya Serikali na MACCM wanakuwa mabilionea lakini Watanzania kwa asilimia kubwa sana wanaishi katika maisha ya ufukara wa kutisha hata mlo mmoja tu hawajui wataupata wapi. Kila kitu chetu nchini ni shaghala baghala imefikia mahali MACCM yanapeana rushwa ili kupitisha muswaada wa kihuni ili kuminya uhuru wa habari nchini. Tafakari kwa kina Mkuu achana na kudumaza akili yako.
Nyie bakini tu kwenye keyboard Lakini watanzania wanapiga kura ccm
 
We bado kweli! Ni hasara kubwa kwa Taifa kuwa na watu kama wewe. Aliyesema nchi inaenda kama gari bovu haina sukani aliwahi kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, aliyetamka kwamba nchi imepoteza mwelekeo aliwahi kuwa Jaji Mkuu na pia Waziri Mkuu wa nchi hii, lakini mpuuzi wewe na mahaba yako yaliyopitiliza kwa dikteta uchwara bado tu unapiga debe na kuandika pumba humu!
Wewe tukana uwezavyo, povuka utakavyo...ukweli ni kwamba ccm kinabadilika na kitaendelea kutawala mpaka nyie wapinzani uchwara mjifunze kusimamia kanuni na maadili na muache usanii
 
CCM wamethubutu na kama kweli wakiwa objective na kutafuta vijana ambao siyo opportunists basi hata nchi itapona.

Imani ya wengi itarudi kama wataacha mambo ya nepotism, ku recruit watu bila criteria na kupunguza partiality...

Hamphrey Polepole baada ya hapo anza sasa programs za ku recruit vijana kuanzia mashuleni bila kuvuruga elimu...Tafuta vijana waliopo makazini walio na chakuonyesha katika jamii objectively na jaribuni kuwaenzi wazee walioonyesha uzalendo kwa Taifa hili kwakumaanisha kuanzia ngazi ya shina na siyo wale wa kitaifa tu.
Wapinzani hawataki tu kujifunza. Ccm sasa wanaendesha mambo yao kimkakati na kisayansi. Kelele kama zile za Nape hazina nafasi tena. Ni uwajibioaji na utendaji ndani ya kanuni na maadili
 
Ninazitabiria Harakati za CCM zinazoendelea sasa Dodoma kukifanya kuwa Chama chenye nguvu ya kuendelea kubaki Madarakani kwa miaka mingine zaidi ya 20.

-->Ninaona watu wenye mitazamo tofauti na CCM ya awali wakimiminika kujiunga na CCM

---->Mabadiliko ya sasa na Fukuzafukuza hii, Siioni ikiidhoofisha CCM hata chembe badala yake inaonyesha CCM kama chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kikomavu.

----> Ninaona CCM maslahi wakiachana na siasa, na kuanza kujaribu vitu vingine vya kufanya nje ya siasa maana Chama Sio tena sehemu salama ya kutimizia ndoto zao kimaslahi.

---->Ninaona Hakuna Vuguvugu lolote nje au ndani ya chama cha Mapinduzi likiibuka na kufanikiwa kuidhoofisha .

WAPINZANI wa CCM kama wasipobadilika na kuja na mbinu mpya zaidi ya kudandia matukio, mfano leo masikio yamesimama yameelekea DODOMA badala ya UFIPA kwenye meza ya mipango kujiandaa kupambana na CCM mpya ambayo Muda sio mrefu kishindo chake kitapokewa kwa shangwe nchi nzima Wataendelea kudumu zaidi ya miaka 20 ijayo wakiwa na ushawishi huuhuu ulio chini ya wastani na unaotiliwa mashaka kila kukicha...
Labda wabadilishe na jina hii njia inaweza kusaidia maana hata mabus yanayochinja watu inafika hatua wanabadilisha majina.
 
Ninazitabiria Harakati za CCM zinazoendelea sasa Dodoma kukifanya kuwa Chama chenye nguvu ya kuendelea kubaki Madarakani kwa miaka mingine zaidi ya 20.

-->Ninaona watu wenye mitazamo tofauti na CCM ya awali wakimiminika kujiunga na CCM

---->Mabadiliko ya sasa na Fukuzafukuza hii, Siioni ikiidhoofisha CCM hata chembe badala yake inaonyesha CCM kama chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kikomavu.

----> Ninaona CCM maslahi wakiachana na siasa, na kuanza kujaribu vitu vingine vya kufanya nje ya siasa maana Chama Sio tena sehemu salama ya kutimizia ndoto zao kimaslahi.

---->Ninaona Hakuna Vuguvugu lolote nje au ndani ya chama cha Mapinduzi likiibuka na kufanikiwa kuidhoofisha .

WAPINZANI wa CCM kama wasipobadilika na kuja na mbinu mpya zaidi ya kudandia matukio, mfano leo masikio yamesimama yameelekea DODOMA badala ya UFIPA kwenye meza ya mipango kujiandaa kupambana na CCM mpya ambayo Muda sio mrefu kishindo chake kitapokewa kwa shangwe nchi nzima Wataendelea kudumu zaidi ya miaka 20 ijayo wakiwa na ushawishi huuhuu ulio chini ya wastani na unaotiliwa mashaka kila kukicha...

Sana mmeiga toka vyama vya upinzani hamna lolote CCM,mmewatoa akina Sophia SImba Kafara hakuna mlichofanya,ningewaona nyie wanaume kweli kweli kama mngewatimua wote Nchimbi ,pamoja na Majaliwa.
 
Ccm wamecopy na kupaste tu kwa wapinzani hawana jipya,na wasitegemee mapya kabisa,tena sasa hivi ccm ndo inaakwenda kufa kabisa,mwafaaaaa
 
Kinachoibeba ccm ni mfumo wa uchaguzi na sheria zake kiujumla. Tunahitaji tume huru, polis wawe neutral, madaraka ya rais yapunguzwe. Ikiwa hivyo ndo uje ujitape hapa kuwa ccm inajiimarisha lakini kinyume na hapo nawe unajua jinsi ccm inavyobebwa na tume yake, polis, vyombo vya habari vya serikali na pia mahakama. Kumbuka kilichotokea zanzibar na hata huku bara jinsi kura za ubunge na urais zilivyochakachuliwa kupitia mabavu ya polis na tume ya uchaguzi. Nikiona mtu wa ccm akijisifu eti upinzani hauna nguvu namuona kama mtoto wa miaka miwili kujifanya hajui kilichopo hapa nchini.
Embu chukua idadi ya wanachama wa vyama vyoote vya upinzani alafu chukua na idadi ya wanachama wa chama cha mapinduzi, linganisha uone kama upinzani mnalingana kwa idadi ya wanachama na ccm!
 
Back
Top Bottom