Pre GE2025 Naibu Waziri Mipango na Uwekezaji: Maswa tutampa kura za kishindo Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,009
1,627
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo, amesema hana wasiwasi kuhusu ushindani katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, akiamini kuwa maendeleo yaliyotekelezwa jimboni kwake yanampa nafasi kubwa ya kushinda.

Nyongo alitoa kauli hiyo Machi 28, 2025, mjini Maswa, wakati wa kikao cha Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Stephen Wasira. Akizungumza mbele ya viongozi wa chama na wanachama wa CCM, alisema kuwa kazi aliyoifanya kwa wananchi wa Maswa Mashariki katika kipindi cha miaka 10 anachohudumu kama mbunge inazungumza yenyewe, hivyo ana imani kubwa kuwa ataendelea kupewa ridhaa ya kuwaongoza.

Mbunge huyo, ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na kuthibitishwa tena mwaka 2020, ameahidi kuendeleza juhudi za kuwaletea wananchi wake maendeleo endapo atachaguliwa tena. Kura za maoni ndani ya CCM zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku wagombea wengine wakihimizwa kujitokeza kuwania nafasi hiyo, aidha Nyongo amesema Wilaya ya Maswa yenye majimbo mawili Maswa Mashariki na Magharibi yatampa kura za kishindo Rais Samia kwakuwa yote aliyoahidi ametekeleza kwa asilimi kubwa

 
Back
Top Bottom