Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,233
- 39,236
Jacob Masawe, Nahodha wa timu ya Namungo akihojiwa baada ya mchezo amesema alikwenda kumuuliza refa Smart "mchezaji wake" (Derick Mukombozi) kafanya kosa gani lililopelekea kupewa Kadi nyekundu ya moja kwa moja? Anasema refa alimjibu kampiga ATEBA.
Hapa tuwe wakweli kama sababu ni hiyo basi tuone Kamati ya waamuzi ikichukua hatua dhidi ya Mwamuzi. Kwa sababu kitendo cha mchezaji wa timu inayozuia kufanya madhambi dhidi ya mchezaji wa timu inayoshambulia ndani ya eneo la 18 mbali ya Kadi ilitakiwa kutolewa penati dhidi ya timu ya mchezaji aliyempiga mwenzake.
Kama hili halikufanyika na mbali ya marudio ya TV kitendo anachosema refa hakikuonekana mpaka baadhi ya wachambuzi wakaanza kubuni kwamba Mukombozi alimtukana refa (Shafii Dauda) na wengine alimtia dole ATEBA kitendo ambacho hakijaonekana kwenye picha Mjongeo zaidi ya Wachezaji hao kusukumana wakati Kona ikipigwa.
Mbali ya tukio la Jana bado ni Wazi waamuzi limekuwa janga katika Mechi zote na si ya Jana pekee. Wakati Mambo mengine yakiboreshwa ili ligi iwe Bora zaidi hili la Waamuzi lilisahaulika kuboreshwa.