JMF
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 1,753
- 2,751
Mfumo wa malipo kwa njia ya westernunion ukoje mkuu?Kuna thread kibao zilishawekwa humu jins ya kufanya manunuzi Ebay, ila kwa faida ya wengine nitarudia kwa kifupi ambavyo mimi natumia / naelewa, naamin wengine wataongezea kutokana na uzoefu wao.
kwanza kabisa kun online retails site kibao tofaut tofauti mfano Alibaba, Ebay , Amazon, Wadi na hata siku hiz bongo tuna Kyamu, anyway ziko nying ila utofauti unakuja na utendaj wao. hapa nitazungumia kuhusu Ebay na Amazon ambao nina experience nao wa miaka zaid ya mi nne
kwa kifupi online retails nying zina act as a middle man kati ya muuzaj na mnunuaji, kuna online shops chache ambazo pia zinauza product wanazotengeneza wao wenyewe mathalan Amazon. ambao pamoja na kuwa kama mtu wa kat lakin pia wanauza baadh ya product wanazotengeneza wenyewe kama vile Amazon TV, Amazon Tablet, Amazon E reader maarufu kwa jina la kindle , Amazon Phone inaitwa fire na vitu vingine vingi, lakin pia wanaruhusu watu kuuza bidhaa zao mpya ama used kupitia mtandao wao,
Ebay wao hawana bidhaa wanazotengeneza ila wanaruhusu muuzaj kuweza kutangaza na kuuza vitu kwenye webiste yao kwa malipo ya ada kidogo,
Ebay wanatumia Paypal katika swala la malipo ( ebay na paypal walikuwa kampuni moja ila ss hv wamesplit kwa sababu za kibiashara lakin bado ni sisters companies)
Amazon wao wanamfumo wao pia wa malipo
Muuzaj na Mununuaj wote wanatakiwa kuwa na Account kwenye hizi online shoopings website wakiweka details zao zote kuanzia physical Address had jinsi watakavyofanya malipo, kwenye malipo ni lazima ulipe kwa kutumia Credit card ya Master card, Visa ama nyinginezo wanazozikubali, unaweza ukafungua account ya hiz credit card kupitia Local bank yako, mfano Exima wanatumia Mastercard, CRDB , NBC wanatumia VISA card. ziko za madaraja tofaut kuania Silver had Gold
Kinachofanyika ni kuwa kama ww ni muuzaj unafungua Account na hiz retails Ebay , Amazon na nyinginezo, unatangaza Bidhaa zako iwe used ama Mpya, unakuwa unalipa kias kidogo cha fee kwa wao kukuruhusu kutangaza na kuuza bidhaa yako pale, ikitokea umeuza then pia kuna percent inaweza ikabak kwao. unapojisajili na kujaza namba yako ya credit card Ebay kupitia Paypal , na Amazon pia watajaribu kucharge kiasi kidogo za fedha ( mara nyingi ni Dola moja) kwenye hiyo account ilikujua kama ni legit na pia ww ndio mhusika, charges zikikubaliwa then ndo wata kuaccept kama legit seller ama buyer, na hiyo dola moja wanairudisha kwenye account yako.
MUUZAJI ANATAKIWA AWEKE TAARIFA KAMILI NA ZA KWEL KWA BIDHAA ANAYOUZA IKIAMBATANA NA PICHA IKIWEZEKANA, Ebay ama Amazon Watatumia hizo taarifa na mawasiliano kati ya Muuzaj na Mnunuz kuweka kutafuta suluhisho kama kutakuwa na Dispute kat yao
Mnunuaji ukinunua bidhaa online kinachotokea ni kuwa Ebay ama Amazon wanact kama vile broker wa mnunuzi na muuzaji maana yake ni kuwa kama mnunuaji unalipa kupitia Amazon ama paypal kwa Ebay, then Amazon ama Ebay huwa hawamlipi muuzaj had pale utakapokuwa umepokea mzigo wako, ama anaweza kulipwa kabla lakini ikitokea mnunuaj akacomplain na wakajiridhisha kuwa muuzaj ana makosa unarudishiwa pesa yako na wao wana deal na muuzaj na ndio maana hawaruhusu makabidhano ya mkono kwa mkono hata kama mnakaa mtaa mmoja wanarecomend itumike njia ya kutumiana kupitia shiping agencies kwani kule kutakuwa na proof of delivery,
Amazon na Ebay they are very secure and reliable ,
NB: KUMBUKA KUSOMA DETAILS ZOTE ZA BIDHAA UNAYOTAKA KUNUNUA KAMA UNA WAS WAS MUANDIKIE EMAIL MUUZAJ KUPATA UFAFANUZI, EBAY NA AMAZON WATATUMIA MAWASILIANO YAKO NA DETAILZ ZA BIDHAA ILI KUPATA SULUHU YA DISPUTE YOYOTE NDO MAANA MAWASILIANO YA EMAIL YANAKUWA RECOMEND NA WALA SIO KUWASILIANA KWA NJIA YA SIMU, Kwenye Website zote kuna jinsi ya kuwasilina na wauzaj kwa njia ya Emali ambapo Amazon ama Ebay wanapata copy ya kila Email exchange kat yenu kwa hiyo hata kama muuzaj aliongopa kwenye maelezo bas anakuwa kajifunga, na usifanye biashara na mtu anayetaka malipo yafanyike nje ya Amazon ama Paypakl kwa upande wa Ebay, mathalan kutumia Western Union
nawakilisha
CC:
KikulachoChako, Echililo, lovebitelol