Mzazi asiyejielewa ndiye atampeleka mtoto wake Pre-form one

Shule za seminary hasa za Kanisa katoliki huwapitisha wanafunzi wake pre form one na imeonyesha matokeo mazuri sana kwa wanafunzi wao kitaaluma na hata kwenye activities zisizo za kitaaluma.

Mtoa mada huna hoja.
Chuo hakuna tuition kwanini iwe muhimu huku chini
 
Hiyo pre sasa, vijukuu vya kike vipo juu juu vimevaa vitop, si mama umeshajihimu huko kutafuta,

Sasa hapo ndo shetani anaanza kujiinua, shetani mwenyewe ni hao hao bodaboda oo saa mbili umfuate binti yangu umpeleke pre kwa mwalimu fulani.

Shetani mwingine wanakutana naye huko kwenye mabus,

Shetani mwingine hao hao asiowapenda yule mwana jf.

Hapo sasa ndo shida inapoanzia
Bibi mpare upoo
 
Huko Prefirm ine nani anawaangalia? Hahaa huko ndio balaaa kama ulikuwa hujui, by the way mtoto anatakiwa apumzike akili ubongo upunzike, sio kunshindilia ujinga.

Hizi pre form one ni ujinga, ni uhuni hakuna kitu hapo, unazani kuna kitu atagain hizo miezi 3 zaidi ya ile kampani yake ya Darasa la Saba kukutana wote hapo kwenye kituo cha preform one?
Kule wanakuwa vikundi na wengi wao wanajuana kwahiyo itakuwa ngumu kufanya upumbafu
 
Pre form ine ni upuuzi, mtoto anatakuwa kumpumzika, shida umasikini unatusumbua watoto wa kishua kwa sasa unakuta watoto wanaenda Vacation
wacha cc kayumba day masikini wakwetu waende pre-form iwe vacation yao, nilisha wahi peleka mtoto english course cjawahi juta kwa hao walimu wangu
 
Bongo bwana of course kiuhalisia tuition nyingi za sasa na hzo pre form one na pre form five ni uzushi hazna impact kubwa sn kwa watoto lkn twende mbele turud nyuma wengi wenywe hizi tuition centre ni wasomi wetu waliokosa ajira so hyo ni njia mojawapo ya wao kujiajili so watu wanapambania ugali wao... si wenywe kipndi tunasoma walikuwepo kina mudy physics, ally abdallah, mtiga, mbuga ambao walifanya masomo ya sayansi tuyaone mepesi
 
Na chekechea nao wanapelekwa Tuition, Kuna Mtu Jana nimemsikia mahali anamtumia Mwalimu pesa ya tuition ya Mtoto wa chekechea

Kwa chekechea unaweza kuta mzazi uyo hana mda wa kukaa na mwanae sasa solusheni ni nn kumtaftia mwalimu

Kuna ttzo kubwa sana kwa familia za kitanzania kutokua na ratiba ya kueleweka sasa kutokana na sababu km izo wazazi weng hukosa mda wa kukaa na kufundishana na watoto wao
 
Ni vitu gani wanajifunza huko Preform one ambavyo hawatajifunza Secondary?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna shule boss hazina mwalimu wa physics au math au kama yupo yupo mmoja au wawili so kama mtoto anaenda centre nzuri inamsaidia ila shida hyo kada ya elimu ishavamiwa na wapigaji wengi..

Mtoto anaanza pre form one mwez mzima anaishia kufundishwa how to introduce yourself na debate za kiduwanz wengne mpk disco wanawawekewa
 
Elimu kwa mtoto ni ufunguo wa maisha.
Watoto wanatofautiana uelewa, na kila mmoja wetu humu ana uelewa wa namna yake. Sio wote wakaa darasani watamwelewa mwalimu afundishapo kila kitu, kuna wengine akielekezwa tu hata kabla mwalimu hajamaliza kuandika mwanafunzi huyo ashatoa jibu la swali husika, kuna wenginee hadi swali lirudiwe mara kadha ndo atatoa jibu.

Na ikawe kheri kwa kila mzazi/mlezi kuwekeza kwa namna yake kwa mwanaeee
Binafsi kama mwanangu anakichwa kizur na najua sekondari ntampeleka private kwangu siwez kumpeleka pre form one ila kama najua kipato chang cha kati au chini kwamba sekondari ataenda st kayumba ntamtaftia mwalim mzur amshushie madude kama mbuga au mudy physics..

Ila ni vema mtoto ukampeleka veta short course apate skills yyte ya ufund au ata kujifunza short course za computer
 
Pre form one ni wizi tu japo kla mtu anamaamuzi ya kufanya na familia yake tena mbaya zaid unakuta mtoto katoka private school.
 
Wote tuna ubongo sawa ila akili tofauti mkuu

Ubongo hata wanyama wengine wanao mkuu.

Katika hali ya kawaida, binadamu wote huzaliwa na kiwango fulani cha akili.

Tofauti inakuja kwenye kinachofanyika katika kuendeleza hiyo akili na kwa kiasi fulani, kiwango cha akili ambacho mtu amezaliwa nacho au kurithi kutoka kwa wazazi wake.
 
hili suala ni subjective, mtoa mada upo sahihi kwa upande mmoja na wanokupinga wapo sahihi kwa upande wao, kila mmoja abaki na anachoona ni nafuu kwake
 
Enzi zetu kipindi hiki disco toto litakoma, uko mabwawani kuogeleea sana ikifika jioni mtacheza cha ndimu mpakq jasho linakauko, giza likings ile michezo ya kujificha nampenda mpenda ndio pahala pale yani mtaa unachangamka, ikifika mda wa kulala mmechoka wote
 
Back
Top Bottom