Mwenge wa Uhuru kutembelea Shamba la Mananasi la Kikwete, ni Usaliti kwa Rais na Sera ya Viwanda

Boss figganigga Hauwezi kusema tupo kwenye Sera ya Viwanda bila kuwaandaa Wananchi. Isitoshe 70% ya WaTanzania ni Wakulima. Kazi ya Jamhuri na Serikali ni kuwawezesha Wananchi kutoka kwenye Sera ya Kilimo Kwanza na kuwapeleka kwenye Viwanda. Waweke mazingira ya Wananchi kuanzisha Viwanda.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 imetengewa Tsh. 267.8b kama Bajeti Kuu. Huku Wizara ya Uchukuzi ikitenga Bil 500 katika ununuzi wa ndege. Hii inaonesha kama taifa hatujui tunataka nini.

Mimi hamna Sera nlipenda kama Kilimo kwanza, sababu ilikuwa ilikuwa inahimiza kilimo cha Kisasa na Watu Waliwekeza kweli kweli. Hii ndo Sera ambayo Mheshimiwa Kikwete aliisimamia kidete. Lakini mwenzake alomfuata akaachana nayo, akataka tuwekeze kwenye Viwanda sio Kilimo tena. Hata siku moja hutasikia rais anasema tuwekeze kwenye Kilimo. Ambacho kiliendana na Matokeo Makubwa Sasa.

Kwangu Mimi naona huu ni Ujumbe Kikwete anatoa kwa rais. Wewe ukiangalia kwa jicho la kawaida utasema ni mfano. Hakuna mwenye mfano bora kwenye kulima kama Mkapa na waziri Mkuu wa Zamani Mizengo Pinda. Wana mashamba makubwa acha hizo nanasi, lakini hajaita mwenge kuyatembelea.

Kikwete bado analilia Sera yake ya Kilimo kwanza na BRN ambayo Serikali ya Magufuli haitaki kusikia. Ameamua kuongea kwa Vitendo kwamba watu tulime na tuachane na Viwanda. Kitu ambacho naona ni Usaliti. Kwangu Mimi Utajiri wa Kikwete alitakiwa atujengee Kiwanda sio Nanasi. Asipojenga yeye nani atajenga? Wanamwangusha rais. Ni picha mbaya. Wenzake runaenda kulia yeye anaenda kushoto si picha nzuri.
 
We kweli hamnazo! Sasa viwanda bila kilimo unataka kutengeneza nini? Kwani katika akili yako unaona hakuna kiwanda cha vinywaji barid vitokanavy na zao hlo? Akili zako ulikozikopa huko umepewa za bandia rudisha kwa mwenyewe
Hapa naona mnataka kuleta mchezo wa yai na kuku ni nn kilianza? Kwa sasa dira kuu ya serikali ni viwanda. Hata mm nilitarajia mwenge ujikite kufungua na kuhamasisha viwanda hata kama ni vile vya vyerehani 4.

Unapoanza sera ya Viwanda maana yake una malighafi ya kutosha ndiyo maana serikali inakomaa na Accasia kuwa ijengwe smelting plant hapa nchini ili waprocess makanikia. Sitegemei mwenge uende Buzwagi au Bulyankuhulu ukatembezwe kwena hips za makinikia maana hicho sio kiwanda. Mwenge ukienda kupiga mbio kuzunguka zile hips za makinkia itakuwa sawa na ulivyofanya kwenda kuzunguka mananasi ya JK.
 
Ndo hivyo hivyo ulivyosema.... ROHO MBAYA inamsumbua.
Mkuu, jitahidi kuongea point yako bila matusi wala kudhalilisha mtu. Sababu haisaidii wala siwezi kubishana na wewe kwa matusi wala siwezi kukutukana. Tangu mwanzo unatukana tu. Bado naamini unao uwezo wa kuandika mambo mazuri ya kujenga bila matusi. Kwani kumkosoa mtu hadi umtukane? Elezea unachokiamini na watu watakakuunga au kukupinga kuliko kutumia matusi. Unaidhurumu nafsi, naami hata nafsi yako haikubaliani na matusi unayonipa. Acha matusi.
 
Sijakuelewa Ndugu, kuona nini na kuanza kuiga nini?
Mwenge kwa agenda yake ni kuleta matumaini, hivyo Kama Mstaafu analima shamba na kulitunza vizuri ni rahisi hao wenye mwenge kuona na kuiga yaliyofanywa ili na wengine waweze kufanya hivyo hivyo kupitia huo mwenge ambao huzunguka Tanzania nzima! Hope umenielewa
 
Hahahaaaa... Anasema amekuwa akilima miaka mingi ila anakumbana na tatizo la mazao kukosa soko.
Kama alianza kulima zamani na hakuwa na soko kama ilivyo sasa je! !
Alifanya jitihada gani alipokuwa madarakani kuhakikisha sokoni linapatikana?
 
Mwenge kwa agenda yake ni kuleta matumaini, hivyo Kama Mstaafu analima shamba na kulitunza vizuri ni rahisi hao wenye mwenge kuona na kuiga yaliyofanywa ili na wengine waweze kufanya hivyo hivyo kupitia huo mwenge ambao huzunguka Tanzania nzima! Hope umenielewa
Asante, sasa nmekuelewa. Ujumbe nlomanisha ni kauli mbiu ya mwenge yahusu Viwanda. Basi waseme Viwanda vya kuzindua vimekosa wameamua kwenda kutembelea shamba. Kumbuka hawajaenda kuzindua wala kufungua. Wameenda kutembelea shamba. Just kutembea tu.
 
Ni Usaliti. Kwani angejenga kiwanda asingetoa ajira? Ameshindwa jenga hata kiwanda cha vijiti vya kuchokonolea meno? Tuacheni utani. Hatuna mpango wa kumuunga mkono Magufuli.
usaliti upi tena! Ndio huwa Wanadamu tulivyo angejenga kiwanda cha juice wangesema alikuwa fisadi! Sijui lipi ni jema? Hivyo kwa kidogo alichofanya ndio mwanzo wa kuwa na kiwanda cha matunda
 
Asante, sasa nmekuelewa. Ujumbe nlomanisha ni kauli mbiu ya mwenge yahusu Viwanda. Basi waseme Viwanda vya kuzindua vimekosa wameamua kwenda kutembelea shamba. Kumbuka hawajaenda kuzindua wala kufungua. Wameenda kutembelea shamba. Just kutembea tu.
Kuiga na kupeleka matumaini kwingineko
 
Hilo shamba tuliombee sana , kwa kadiri nijuavyo hakuna mradi wowote uliotembelewa na kuzinduliwa na mbio za mwenge uliodumu hata miezi 6 tu .
 
Kwa uelewa wangu viwanda bila kilimo jibu ni zero!. Hata walioendelea kea viwanda walianza na kuimarisha kilimo. Waka stabilize uzalishaji ndipo wakaenda kwenye viwanda. Ruhsa kutafakari kabla yankutoa mada
 
Kwa uelewa wangu viwanda bila kilimo jibu ni zero!. Hata walioendelea kea viwanda walianza na kuimarisha kilimo. Waka stabilize uzalishaji ndipo wakaenda kwenye viwanda. Ruhsa kutafakari kabla yankutoa mada
Hivyo nipo sahihi nikisema rais Magufuli kakosea kutupeleka Serikali ya Viwanda na kuachana na Sera ya Jakaya kikwete ya Kilimo kwanza na BRN?
 
Huu mwenge unazunguka kwa kodi yangu. Imeniuma sana kuona mwenge unatekeleza kitu kicho nje ya Malengo. Kauli mbiu ya mbio za Mwenge kwa mwaka huu inasema, “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU.” Je hivi ndo Viwanda Mwenge umeenda kushiriki kukuza? Ndo maana hatuendelei sababu hatuna dira wala Uelekeo
Figganigga unatia aibu ndugu daaaa!
 
usaliti upi tena! Ndio huwa Wanadamu tulivyo angejenga kiwanda cha juice wangesema alikuwa fisadi! Sijui lipi ni jema? Hivyo kwa kidogo alichofanya ndio mwanzo wa kuwa na kiwanda cha matunda
Ni bora hela zikafichwe uswisi ili asionekane fisadi. Uongo?
 
Back
Top Bottom